Diploma Vs Bachelor

unclebk

Member
Joined
Mar 6, 2019
Posts
44
Reaction score
115
Wandugu wa Jf, habarini za majukum,

Naomben ushaur hapa, nategemea kumaliza stashahada ya Medical Lab hapo mwakan kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, ila hapa nina mgogolo wa nafsi.

Kuna wakati naona kher niishie kwanza hapa then ntafute maisha, na baada ya kutoboa nitajiendeleza mwenyewe.

Lkn upande mwingine najisikia kuendelea na bachelor, kwa lengo la kumalizana kabisa na maswala ya shule kwa level hii. Wazo hili la kuendelea linapata nguv sana pale napowaza swala la mkopo likitiki.

Naomben msaada wenu wa mawazo. Lkn pia mnipe uzoef wa maswala ya mshahara + makato ya kulipa mkopo endapo ntapata.
Asante.

Nawasilisha.
 
Mkuu binafsi nakushauri em tafuta mahala Kwanza ujiegeshe huku unasoma upepo.

Maisha ukiwa shule yana utofauti na ukiwa mtaani niamini mimi.

tafuta mchongo ,ukipata we endelea ufungue vimiradi vyako vidogo vidogo huenda vikakusaidia Kwa sasa kuliko kuongeza mashule japo Lina umuhimu pia.

kibongo bongo Kwa sasa kadiri unavyozidi kwenda juu kimashule ndo possibility yako ya kupata kazi inakua ngumu japo sifa za kusifiwa zinazidi kuongezeka.

Mchawi pesa mkuu .....mashule labda kuelimika tu.

za kuambiwa.
 
Daaah,,,,, aisee nashukurun kwa mashaur,,,
 
Mzee watu wengi hawaelewi unakuta mtu anahangaika kuitafuta digrii mpaka miaka 30 hana mbele wa nyuma anabaki kuwa na stress tu.
[emoji419]
Hapa ndipo paliponifanya niishie diploma
 
Binafsi naona bora uvumilie umalize diploma yako maana medical laboratory ni marketable sana unaweza jiajiri au ukaajiiwa umebaliza muda mchache tu uanze kula cake ya taifa so piga spanner bro utatoboa.
 
Soma alama za nyakati ,, alafu angalia upepo unasemaje

Ushauri ukimaliza dip yako na ukaona mambo ya kazi hayasomeki unga Bach ila endelea kufukuzia michongo ikikaa poa hairisha mwaka komaa na job baada ya muda unarudi shule tena

Jamaa zangu wengi wamekifanya hiki kitu na wame graduate Mwaka huu 2020

Ila walitakiwa tumalize nao 2018.
 
Angalia umri wako pia kama umri umeenda kidogo ni bora uingie mtaani kwanza upate kasehemu ujiweke sawa kwanza then ndio uendelee na kusoma.

Ila kama umri unaruhusu ongeza cheti mapema kama vipi
 
Naendelea kuwashukuru kwa mawazo mazur na yenye kufanana.
 
Mzee watu wengi hawaelewi unakuta mtu anahangaika kuitafuta digrii mpaka miaka 30 hana mbele wa nyuma anabaki kuwa na stress tu.
Mm namaliza diploma nikiwa na miaka 25 aisee bora mambo mengine yafuate kuliko kuendelea kusoma
 
Jambo la maana hilo boss tfuta hela kwanza...mimi nina umri huo nilimaliza Diploma nikiwa na miaka 23...nilipoingia kitaa nikalisoma gemu nikaona hapa shule nitarudi ila baadae sana.
Mm namaliza diploma nikiwa na miaka 25 aisee bora mambo mengine yafuate kuliko kuendelea kusoma
 
Ukimaliza jijenge kwanza.

Vyuo vipo na degree zipo, utasoma tu
 
Halafu kuchukua bachela ya medical lab naona kama vile kupoteza hela hasa kama tayari una diploma,kupitia diploma unaweza ganya mambo mengi sana na hiyo Medical lab na ukawa una soko bado dispensary kibao zinataka diploma wa medical lab ili waopareti dispensary zao kupitia cheti chako hata kama ufanyi kazi unaweza vuta 150k+ kwa kupitia tu cheti...

Nb;kupanga ni kuchagua
Binafsi naona bora uvumilie umalize diploma yako maana medical laboratory ni marketable sana unaweza jiajiri au ukaajiiwa umebaliza muda mchache tu uanze kula cake ya taifa so piga spanner bro utatoboa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…