Ndugu Muheza, siyo lazima uwe na gari bomba kusema kuwa jamaa fulani kanunua mkweche. Ndo maana Dr Remmy aliwahi kuandika kwenye mkweche wake kuwa, "ETI IMECHAKAA, BABA YAKO ANAYO?". Kwa hiyo usianze kumzuia ndugu Masa kuongea eti kwa sababu hajagundua. Vinginevyo wote itabidi tunyamaze. Wapo watu hapa wanamsema vibaya Kamala kwamba kashindwa kuongoza wizara, ila ni kwa sababu yeye amejaribu na ndiyo maana tunaweza kutoa maoni kama kashindwa au kaweza. Je, tusiongee hadi tuwe Wakuu wa mikoa, mawaziri n.k; au wote tugundue mwezi mwingine? Kuna watu humu hawajawahi kuongoza hata kundi la watoto au kufanya jambo la maana kwenye jamii. Je hao nao wanyamaze?