Habari, naomba kutoa mchango wangu jamani....tafadhalini sana naomba mniruhusu.......
Ipo hivi, dunia ya leo mambo mazuri ya asili yanavurugwa na mambo yasiyo asili ya kibinadamu ambayo tumeyageuza misingi ya kuishi badala ya mambo ya kimsingi kabisa.
Dini haijawahi na haikuwahi kuwa msingi wa upendo wa ndoa. Wakati Adam na Eva wanaundwa pale Eden, na ule upendo walipewa na MUNGU ni wapi dini ilikuwa jamani tujiulize?!
Si tu dini, kuna rangi(race), kabila, uwezo wa kiuchumi( Financial status) na kadhalika ndivyo vimekuwa standard ya kupimia mizani ya upendo katika jamii za kileo.
Haya ni maamuzi ya kimapokeo ambayo leo hii yamekuwa chanzo cha watu kushindwa kuelewa ukweli juu ya upendo katika kujenga familia imara.
Mwanamke huwa ana ana andamana na mume wake na kuanza nae maisha na ndio maana tunasisitizwa kuwa makini sana pale tunapochagua wenza ili tupate ambao wanajua miiko ya kistaarabu na wanajitambua kwa kile wanafanya katika maisha na waziwe mvurugo katika maisha yetu.
Thamani ya mtu haipo katika kujionyesha anaijua dini yake au imani yake maana kuwa hivyo na matendo yako yakawa ni mabaya haina faida yoyote.
Ni wangapi leo wanajifanya washika dini ila wanachombeza wake za watu, wanadhulumu, wanachukia wengine, wanachonganisha watu, wanadhulu wengine na maovu ya kila aina....
Me naomba nishauri jambo hili, huyo dada anapashwa kufahamu kuwa ndoa ni safari ya maisha na si kitu cha kupanda na kushuka kama daladala....
Msingi wa ndoa ni upendo wa dhati usiobagua....yule ashikaye amri ya upendo basi ajue ameshashika dini ndani yake....pasipo na upendo wa dhati basi dini ni maigizo tu.
Dada anatakiwa kutambua kuwa mama ndie chem chem ya upendo katika familia, kwanza kwa mumewe then kwa watoto wake. Dini huwa haina msaada wowote kwa mwanamke mjuaji na mbishi....ila huwa silaha ya ushindi pale mwanamke anapokuwa msikivu, mpole , mnyenyekevu na mwenye subira.
Kubadili dini haina madhara kwa mwanamke kwasababu unafuata imani ya familia yako mpya ambayo mumeo atakuelekeza na utajifunza pia na ukiisimamia vema itakuwa ni dini yako mpya na utaendelea kubarikiwa na MUNGU yule yule ambaye mwanzo ulikuwa ukimtegemea.....
Huwa siwaelewi watu ambao wanatabia ya kumini mwanaume kaandikiwa kufa kwanza, maana hata mke anaweza kufa kwanza katika haya maisha.....hivyo acheni hizo fikra mbaya na za uchuro kwa wanaume shenzi....
Ongea na huyo dada, muwashirikishe na wataalamu wa saikolojia waliofunzu sio hawa uchwara. Someni pamoja maandiko ya mitandaoni ambayo yanazungumzia namna ya mwanamke anavyoweza kupambana na hisia za ubaguzi wa dini, rangi, jamii au kabila pale anapokuwa na wakati mgumu kuamua kubadili imani yake kwaajiri ya mume wake na kufanana naye maisha yake yote.
Kumbukeni haya ni maisha yanu ninyi tu, so maamuzi yanawataka ninyi wawili tu kuridhiana na si marafiki, ndugu wala wazazi watawaingilia.
Achaneni na mitazamo ya kidunia ya kibaguzi.....zingatieni sana hisia zenu za kweli.
Kama mtatengana katika hili basi ninyi hamkuwahi kupendana na ilikuwa ni puppy love tu ya kupotezeana muda. Upendo wa kweli una nguvu kuliko kitu chochote hapa duniani......kama hauamini tafuta wanaoujua.....na kwa bahati mbaya dunia ya leo ukiwa na upendo wa kweli huwa unaonekana mjinga na hauna akili sawa sawa.....hii haipo sawa hata kidogo!
Kaa na huyo msichana na umwambie huu ukweli bila kumuhofia na mtoe hofu ya yeye kuamini akibadili dini atakuwa amekukosea wewe....
Na kama utahitaji muongozo zaidi na msaada zaidi namna ya kusolve hii changamoto nicheki inbox na namba yako ya sim
Sent using
Jamii Forums mobile app