Dini na Siasa ni maisha ya watu. Waacheni Maaskofu wazungumze

Dini na Siasa ni maisha ya watu. Waacheni Maaskofu wazungumze

jindundu

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2025
Posts
679
Reaction score
580
Kufuatia funga ya Novena ya Kanisa Katoliki na Mahubiri ya Maaskofu wa Kanisa hilo Jumapili iliyopita, watu mbalimbali hususani wana CCM wamejitokeza kuwazodoa viongozi hao wa Dini kuwa wanachanganya Dini na Siasa na kuwataka waache mara moja.

Mi nataka niwaulize, hivi ukiwa Kiongozi wa Dini unaondolewa Ile haki ya msingi aliyopewa raia wa Tanzania katika kuwaweka viongozi madarakani? Soma Katiba Ibara ya 8: 1(a).

Kuna Sheria gani inayomzuia kiongozi wa Dini kutoa ushauri, kupongeza, kukemea na kuonya Serikali na viongozi wake inapobidi?

Kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi dhidi ya Serikali yao. Wala hakuna siri tena. Waumini wao ni wengi, wanazungumza nao wanawaeleza, mengine wanayaona kwa macho yao.

Wakati waumini wao, wakiwa sehemu ya jamii wanapiga kelele dhidi ya uvunjifu wa amani, matumizi mabaya ya raslimali za Taifa, kupungua kwa maadili ya viongozi, watu kukosa uzalendo, unataka Maaskofu wanyamaze?

Nauliza hivi Siasa siyo maisha ya watu na Dini siyo maisha hayo hayo ya watu? Hivi vitu viwili unavitofautishaje?

Kwa ninj wanapowapongeza viongozi wa Serikali hamsemi kuwa wanachanganya Dini na Siasa?

Kuna tofauti gani kati ya wajibu alio nao Kiongozi wa Serikali na ule alionao kiongozi wa Dini?

Kwa Nini mnataka kulazimisha wasitimize wajibu wao kwa Taifa na jamii kwa ujumla yaani kufundisha, kushauri, kukemea na kuonya?

Viongozi Serikali wanazo platform za kutumia kufikisha ujumbe kwa wananchi. Viongozi wa Dini platform zao ni Madhabahu. unapowazuia wasizitumie unataka wakazungumzie wapi?

Siasa na Dini ni maisha ya watu, waacheni Maaskofu wazungumze. Ni wajibu wao wa Kitume.
 
Deni limekua kwa kasi hadi 116T hadi Mr Slow ameamua kutoka mafichoni atoe neno, ingawa naskia rc pia wana andaa waraka mzito wiki hii na leo mama anajambo lake na presi...
 
Deni limekua kwa kasi hadi 116T hadi Mr Slow ameamua kutoka mafichoni atoe neno, ingawa naskia rc pia wana andaa waraka mzito wiki hii na leo mama anajambo lake na presi...
Acha aendelee
 
CCM ni mipumbavu!Yesu mwenyewe alikuwa kila siku anakinukisha kwa wafarisayo na wasadukayo.Wao ni akina nani wasisemwe? Marabooks zao!
 
Back
Top Bottom