Dini inapokuwa jibu la kiuchumi

Asovene

JF-Expert Member
Jan 7, 2017
213
216
Nimefuatilia dini za siku hizi hawa wachungaji wetu wa kisasa wengine wanapiga hadi wanachana mistari ya bongo flava nimemsikia mmoja akichana,wacha mameno weka muziki bamba to bamba.

napenda kujua kwa nini siku hizi dini inageuzwa biashara mchungaji anapiga hela na washiriki wanafundishwa kutafuta hela zaidi ya kumtafuta MUNGU hii si sahii kabisa dini ni imani na siyo njia za kiuchumi njia za kiuchumi ni mfumo wa maisha na siyo imani.

Inakuwaje kanisani mnaanzisha vikundi vya saccos na kukopeshana sadaka?
 
Haya mambo yalianza kushika moto katika historia ya karibuni na kitu kinachoitwa "Liberation Theology" kwa habari zaidi soma Liberation theology - Wikipedia

Badala ya watu kukubali umasikini maisha haya ili wapate uzima wa milele mbinguni, watu wakaanza kutaka utajiri hapahapa.

Ukichunguza sana utaona ni habari zinazoonyesha uongo wa dini tu.

Waingereza walisema "You can fool some people for some time, you can even fool some people all the time, but you can't fool all the people all the time".

Hawa wachungaji wameona kuahidi uzima wa milele mbinguni tu hakutoshi, watu watawashitukia kwa sababu ya kutaka maendeleo hapa hapa duniani kwanza.

Wakaona ni bora waende na nyakati kama wanataka kubaki kuwa relevant.
 
KWA MFANO DINI YANGU YA KIKRISTO SIJAWAHI KUONA SEHEMU YOYOTE MITUMI WAKIFANYA BANKING AU SACCOS,
 
KWA MFANO DINI YANGU YA KIKRISTO SIJAWAHI KUONA SEHEMU YOYOTE MITUMI WAKIFANYA BANKING AU SACCOS,
Ukishaambiwa "toa ndugu toa ndugu ulichonacho wewe, bwana anakuona mpaka moyoni mwako" tayari ni banking hiyo.

Kama Yesu kasema ndege hawapandi wala kuvuna, lakini hawakosi riziki, kwa nini makanisa yanaomba sadaka?

Mungu kashindwa kuyashushia manna kutoka mbinguni na sisi wengine tusioamini tujue utukufu wake kwamba yupo kweli?
 
Mada nzuri,mkuu ebu dadavu zaidi kuhusu Liberation Theology Al-Watan
Kimsingi Liberation Theology inataka kumpa mwanadamu uhuru kutoka umasikini hapahapa duniani badala ya kuhubiri habari za kusema mkristo vumilia shida za dunia hii na umasikini wake kwa kuwa utapata uzima wa milele mbinguni.

Inaruhusu kuuliza kwa nini nisipate maisha mazuri kwanza hapa hapa duniani.

Uzuri au ubaya wa Ukristo/ Biblia na vitabu vingi vya dini ni kwamba vina upana unaoruhusu mambo mengi sana, ni tafsiri ya mtu tu.

Mtu akitaka kusema kwamba Wkristo wanatakiwa kuishi kimasikini na kuukana ulimwengu huu kwa sababu ulimwengu huu si wao, wao ni ule unaokuja, kuna maandishi mengi sana ya ku support hilo.

Mtu akitaka kusema kwamba Mungu kasema nendeni mkaitawale dunia, na hilo maana yake ni kwamba tunatakiwa kuwa matajiri kwa kuitawla dunia hii hata kama tunatarajia kwenda mbinguni kupata uzima wa milele, hilo nalo lina mistari mingi sana ya kuli support.

Binafsi siamini dini wala Mungu literaly, kwa hiyo habari za kungoja mbinguni ili nifurahi siikubali, nataka nipate ninachoweza hapahapa duniani, huko mbinguni hata sijui kama kupo.

In that regard liberation theology inawafaa watu kwa kuwafungua minyororo ya kukubali umasikini.

Tatizo linakuja wapigaji wengi wanatumia makanisa kama miradi ya kujinufaisha binafsi.

Unakuta kanisa la watui masikini, wanakamuliwa sadaka, halafu mchungaji na askofu wanaishi maisha ya juu sana.

Huo ni utapeli tu.
 
Back
Top Bottom