Dilemma: Simu ipi itanifaa zaidi kati ya huawei p9 vs Nokia 6?

pureView Zeiss

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
4,950
2,000
kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu,mimi ni mpenzi wa simu za nokia(smartphones).
baada ya kutumia window phone kwa muda mrefu mwaka huu nimeamua kuachana na hii jela ya mateso(window phone Os) nakumbuka mara ya mwisho kutumia android ilikuwa ni jelly bean version.kitu ambacho kimenivuta kurudi tena ondroid ni ujio wa simu zangu nokia kwenye android

nimeisubiri nokia 6 naona muda unazidi kwenda sasa nimefanya window shopping pale aggrey kwa washikaji zangu nimekutana na mashine hii HUAWEI p9 ni noma aisee kuanzia chipset,dual camera,battery endurance iko poa sana,design,RAM n.k
pia najua nokia 6 kwa upande wa bei itafika hadi laki 6 na kitu na upande wa huawei p9 bei yake ni laki 8 naomba mnisaidie simu ipi itanifaa zaidi?

msaada wenu wadau,karibuni mkekani
 
Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
54,193
2,000
Ununuzi wa gadget/electronic device yoyote unategemea sana uhitaji wa matumizi, yaani unataka simu ili ikusaidie katika lipi?

Wakati mwingine unaweza kutumia pesa nyingi kununua simu halafu mwisho wa siku ukapata haifanyi vile ulidhani itakusaidia
 
Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
49,436
2,000
Nikijiweka kwenye nafasi yako ningechukua Nokia 6. Kwasababu zifuatazo;
1. Kwanza umeisubiri kwa muda mrefu sana. Ila hiyo P9 ilikuwepo sokoni muda mrefu, kwanini hukununua hiyo toka wakati huo? Nunua Nokia tu mkuu. Usiidhulumu nafsi yako.
2. Zote zinatumia Android.
3. Utakua unamiliki brand ya kueleweka. Hiyo P9 haina utofauti na Tecno kimuonekano.
 
ndugu nimekuelewa sana tatizo naona kipenzi changu nokia naona anachelewa kuingia sokoni na pesa zetu hizi za kuungaunga itabidi nijibane nisubiri mwezi ujao na pia kumbuka nokia 6 ikitoka bei yake kibongobongo itafika hadi laki 7
 
Ngosha255

JF-Expert Member
Mar 29, 2013
402
500
Nikijiweka kwenye nafasi yako ningechukua Nokia 6. Kwasababu zifuatazo;

3. Utakua unamiliki brand ya kueleweka. Hiyo P9 haina utofauti na Tecno kimuonekano.

Aisee hapo kwenye tatu itakuwa unaonesha mahaba sio ushauri kwa ajiri ya kitu kilicho bora

Huawei kwenye mate na p-series wako vizuri design hadi performance
 
Ghadaf

JF-Expert Member
Oct 15, 2016
513
1,000
Tafuta Samsung galaxy note 4 au Samsung galaxy s7/s7 edge... Hzo ndo android devices ambazo ukinunua uwezii jutia pesa yako.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom