Seneta Wa Mtwiz
JF-Expert Member
- Sep 23, 2013
- 3,643
- 4,185
Wakuu,
Huku pande za kitaa cha Ukonga kama unaelekea Ulongoni kwa mbele kidogo, ukipita Kampala International University (KIU), nd'o nilikopata chumba cha bei nafuu chenye choo ndani.
Wapangaji tupo wanne,
Hao wenzangu wawili ni askari na mmoja ni karani wa mahakama-
Hawa majirani zangu wanatumia Star Times za Antena ambazo mara nyingi ukija upepo huwa zinayumba na kutoonesha picha.
Pamoja na kuwa gheto kwangu nimeweka godoro sakafuni, nimeforce kuweka dikoka ya Azam ili kuchangamsha akili nirudipo kutoka mihangaikoni kwenye shughuli zangu za kusajili laini za Zantel mitaani.
-------
Sasa hivi karibuni hawa wake wa majirani zangu wamekuwa wakiomba kuja kuangalia tamthilia gani sijui inarushwa Azam Tv mida ya jioni (wenyewe ni mapini balaa, weupe na wana wezere za kutosha),
Ili kudumisha ujirani huwa nasogeza TV mlangoni ili waangalie, wakimaliza nairudisha.
------
Sasa jana nimeshangaa,
Nimerudi zangu gheto na mkate wangu wa buku ili nichemshe chai ninywe, nilale.
Nashangaa mlango unagongwa,
Nikasema "karibu",
Kaingia jirani yangu mmoja na hotpot,
Aniambia
"Pumzika kupika @Seneta_Wa_Mtwiz, kuwa huru, majirani tupo kwa ajili yako ..."
Nikicheck kwenye hotpot kuna Wali wa nazi, samaki rost, ndizi mbivu na pembeni kaweka chumba ya juisi ya embe_dodo.
Pamoja na kupigwa na butwaa na hofu kubwa moyoni, nikaudufua ule msosi kwa wasiwasi mkubwa- ila mapishi yake ni noumah wakuu".
-----
Sasa leo wakati naondoka kwenda kwenye mishe zangu za kusajili laini,
Jirani mwingine kaja kufunga geti-
Huku akitabasamu, akaniambia
"Leo usinunue mkate seneta, nakuletea bufee za ya alilokuletea mke wa Afande_¥ jana ..."
------
Wakuu,
Nimefanya uchunguzi wa dharura, nimebaini waume zao wamesafiri kikazi za usalama wa raia na mali zao.
Sasa wakuu,
Hawa wadada wanataka nini hawa??
Hawa wanataka kunigombanisha na ndugu maafande ??
Nitoe hii dikoda au nihame mtaa ??
Ila tatizo kodi yangu inaisha mwakani Januari wakuu.