Digital poultry kutoa mafunzo ya kuunda mashine ya kutotoa mayai bure.

XOXOQY

Senior Member
Feb 7, 2011
169
225
Mafunzo haya yamekua yakitolewa kwa gharama kubwa ,Lakini Digital Poultry itatoa mafunzo haya kwa watuwote ambao wangependa kujifunza namna ya kuunda mashine za kutotoa mayai ya kuku lakini hawana uwezo,hivyo watu wote wanakaribishwa katika mafunzo kwa vitendo yatakayo husisha uunganishaji wa vifaa pamoja (assembling) na kuunda mashine hiyo.

Mafunzo haya yatajikita katika uundaji mashine hizo kwa kutumia vifaa vya gharama rahisi,vinavyo patikana katika mazingira ya kitanzania.

Digital poultry itatoa mafunzo haya bure kwa kushirikiana na Eng.Transistor,ili kutanua mawanda ya vijana kujiajiri kwa kuunda mashine hizi!

Fomu za kujiunga na workshop hii zinapatikana ofisi ya Digital poultry iliyopo Ukonga banana,au unaweza kupiga simu namba 0672704023, kwa maelezo zaidi.

Mafunzo hayo yatahusisha kuunda mashine ya mayai 320.

Wote mnakaribishwa.Mafunzo yatafanyika tarehe 21 January 2017 katika ofisi za Digital poultry Ukonga banana.


Mfano wa mashine ambayo nayo ilitengenezwa na watu wa mafunzo itazame hapa YOUTUBE

 

option

JF-Expert Member
Jan 15, 2013
1,842
2,000
Masije waambia wahusika inabidi pesa ya ukumbi mara namna gani mana wabongo kwa michongo hatare, mmesema bure iwe bure ikiwezekana muwasaidie nauli na chakula.
 

XOXOQY

Senior Member
Feb 7, 2011
169
225
Masije waambia wahusika inabidi pesa ya ukumbi mara namna gani mana wabongo kwa michongo hatare, mmesema bure iwe bure ikiwezekana muwasaidie nauli na chakula.

Sio mara ya kwanza mafunzo kama haya kutolewa mara ya kwanza yalitolewa April mwaka jana na angazo lake lilichapishwa hapa hapa jamiiforums japo wengi walipuuzia,lakini baada ya kuona machapisho hayo ya mafunzo yalivyofanyika wengi wakaanza kuulizia ni lini tena tutatoa fursa hiyo,Kwakuwa kampuni ya kwanza haikuwa tayari kufanya mafunzo hayo tena kwa mwaka jana,Tumeomba kampuni nyingine hii ya digital poultry itoe fursa hii kwa mwaka huu kwa vijana

Ukweli ni kwamba,hua tunatoa bure kabisa,ila kumsaidia mtu nauli na chakula hilo hua hatufanyi.

Kwa kawaida mafunzo haya yanatolewa baada ya mteja wa kawaida kuweka oda ya kutengenezewa mashine,kutokana na hilo hua tunatumia fursa hiyo kuwaita vijana kuona na kujifunza namna ya kuunda mashine hiyo.

Baada ya mafunzo ya mwaka jana watuwengi wamekuwa wakiulizia mafunzo hayo ya bure ni lini tena?Mafunzo hayo ya bure kwa mwaka huu ni January 21 2017

Kuthibitisha hili unaweza kutizama post hii hapa ya jamii forum mwaka jana April.

MAFUNZO YA KUUNDA INCUBATOR YALIO TOLEWA BURE NA ENG.Transistor April 2016


Na kama ukitaka kutizama matokeo ya mashine zinazo tengenezwa na vijana hawa tizama Video hii hapa.

 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom