Leo asubuhi rafikizangu wa kijijini wameniambia kua Tanzania inaingia vita na Malawi2013 ndiyo maana serikali ina himiza haraka watu waingie kwenye Digital ili wale wenye uwezo mdogo wasijue mambo yanakwendaje.
.....duh......
....Uamuzi wa kubadili mfumo wa utangazaji wa televisheni kwenda mfumo wa digitali sio uamuzi wa Tanzania peke yake,ni uamuzi wa dunia kupitia shirika la Mawasiliano Duniani(ITU),ukizingatia kuwa mawimbi hayana mpaka hivyo mashirikiano kimataifa ni muhimu,hasa maeneo ya mipakani,mwisho wa urushaji matangazo ya analojia duniani ni 2015...
....lakini nchi za Afrika Mashariki,Tanzania ikiwemo zikaamua mwisho wa urushaji wa analojia kwa nchi hizi iwe ni 31/12/2012,ikizingatiwa kuwa kwenye nchi maskini kama zetu changamoto za kushindwa kumeet deadline zinawezekana,hivyo atleast mwisho ukiwa miaka 3 kabla ya deadline ya dunia,then miaka hiyo 3 kabla ya deadline ya dunia itatumia kuboresha mapungufu yatakayojitokeza....
...Umuhimu wa kwenda digitali kwanza ni matumizi mazuri ya masafa,kwenye analojia kila televisheni statiob ilihitaji kuwa na safa(frequency) yake,lakini kwenye digitali safa moja linaweza likabeba stations ata zaidi ya 200,hivyo kwa kwenda digitali uhaba wa masafa ya televisheni unaisha,lakini pia masafa mengine yaliyokuwa yanatumia na televisheni yatatumiwa kwa shughuli zingine,mitandao ya internet,na baadae redio za digitali,kwa ujumla wake hatua hii itaibua fursa kubwa zaidi ya kuanzishwa kwa vituo vingi zaidi vya televisheni na hivyo kuongeza ajira,kodi kwa serikali na upataji wa taarifa/habari nyingi zaidi,kwa picha bora zaidi zisizo na chenga kwa wananchi...
...Sio hivyo tu lakini pia kwa kuwa teknolojia zingine za mawasiliano kupitia simu na computer tayari ni za digitali,kwa televisheni kuwa digitali kitaalamu kuna uwezekano sasa wa kuunganisha utendaji wa vifaa hivi,huduma za kimawasiliano zinazopatikana kupitia computer na simu zitaweza kupatikana kupitia televisheni yako ya digitali..
...Na ifahamike kuwa majumbani mwetu tunapata matangazo ya televisheni kupitia sattelite aka ungo,cable au antenna aka chadema,watakaoathiriwa na mabadiliko hayo ni wake tu wanaotumia antenna kupata matangazo ya televisheni,wale wanaotumia ungo na wale wanaotumia cable wataendelea na nyungo na cable zao bila kuathiriwa kwa lolote,wale wanaotumia antenna ndio watapaswa kuwa na televisheni ya digital au kununua king'amuzi ili kiwassidie kupata matangazo ya digitali kupitia televisheni zao za analojia..