hizi ndio speed na maeneo zinapopatikana tanzania
speed ya 2g
hapa kuna network za aina mbili
1.gprs- hii inapatikana nchi nzima na maximum ni 6kBps
2.edge- hii ni 2g ya kisasa ina speed angalau unabrowse html inapatikana karibia nchi nzima ila kuna maeneo haipo na maximum speed ni 35kBps
3. cdma- hii inapatikana kwenye mitandao ya zantel na ttcl kwenye modem na ina speed kama edge tu
speed ya 3g
3g imegawanyika makundi mengi sana na ina speed tofauti nitajaribu kuelezea makundi muhimu yanayopatikana nchini
1.wcdma- hii ndio ya mwanzo mwanzo na ndio 3g iliyopo kwenye feature phone (inaandika 3g tupu) speed yake huwa haizidi 60kBps kwa tanzania inapatikana maeneo yote yenye 3g
2.hspa(hsdpa, hsupa)- hii kwenye simu inaandika 3.5g au H ina speed zaidi kuliko wcdma na inapatikana maeneo yote yenye 3g na kwa tanzania inapita 1MBps (8mbps) hivyo modem ya 7.2mbps inakua kama haitoshi modem inayofaa hapa ni ya 14.4mbps
3.hspa+(3.75g)- hii ina speed kuanzia 21mbps hadi 42mbps so far nimeiona dar tu simu yangu ikiandika h+ si kila mtu anaweza kuipata hii speed hadi kifaa chako kiwe kinasuport hii tech, mara nyingi ni simu kubwa kubwa kama lumia na galaxy s series na note. hapa ndo panapohitaji hio modem ya 21mbps