Did Mwalimu die a natural death?

Mwalimu Nyerere alianza kusigana na utawala wa Mkapa mara tu ya kuwepo kwa hoja ya kuiuza NBC kwa makaburu.Ilivyotokea ni kwamba Mwalimu aliwaita Gavana wa BOT (wakati huo akiwa Idris Rashid),Waziri wa Fedha na wasaidizi wengine wa mambo ya Finance ili kupata ukweli wa suala hilo.Hawakuudhuria mwito huo ndipo alipomtuma msaidizi wake Bw.Batao kumwita Mkurugenzi wa NBC wakati huo Bw. Kimori kwenda Msasani na wakati wa kikao hicho,Mkurugenzi huyo alimweleza Mwalimu ni jinsi gani serikali ingefanya makosa makubwa kuiuza NBC ingali kwamba serikali inapokuwa na uhaba wa fedha za kuendesha mambo katika idara nyeti kama Jeshi na Usalama wa Taifa ilikuwa inachukuwa fedha toka katika Benki hii.

Alimweleza mengi kiasi kwamba Mwalimu alishusha pumzi na kusema "kumbe nimewasomesha wataalamu wazuri hapa eeh!".Mwalimu akamuaga mkurugenzi huyu na kumshukuru kwa taarifa hiyo.Baada ya hapo Mwalimu aliomba kuonana na Rais Mkapa kule Msasani baada ya kumaliza shughuli zake ikulu.Mkapa alipelekewa taarifa hiyo na kujibu kwa kifupi tu "Ok...nimesikia"Mkapa hakutimiza hilo haraka ila alisubiri kwa siku moja.siku aliyokwenda msasani jioni alikuwa amelewa na hata ilikuwa ni kazi ya ziada kushuka kwenye gari kwani mpambe wake Kanali George simule na walinzi walipata kibarua cha kuhakikisha kwamba hakuna aibu ingetokea.Alifika sitting room na kukaa.Mwalimu aliposhuka toka katika chumba chake cha kulala aliiona hali ile ya Mkapa ilivyo.Hakusubiri kitu na hakuongea chochote na alirudi alikotoka.Hali hii ilifanya waliokuwepo kupata wakati mgumu licha ya kwamba Mama Maria kujaribu kumshawishi mumewe kuzungumza na ugeni ule...Mwalimu aligoma.

Asubuhi ya siku iliyofuata aliomba aonane na Kadinari Pengo.Mwalimu alikuwa akiheshimu sana viongozi wa dini hivyo alikwenda yeye ofisini kwa Pengo na hakutaka kadinari aende nyumbani kwake.Alpoingia ofisini kwa kadinari,kwa jinsi Mwalimu alivyokuwa na kawaida ya tabasamu na ucheshi wa hapa na pale,siku hiyo hata Pengo alishangaa kwa jinsi hali ya Mzee ilivyokuwa.Ilibidi kuwaomba radhi watu wengine waliokuwa mle ofisini kutoka na Mwalimu kubakia na mlinzi mmoja na kadinari namsaidizi wake mmoja.

mwalimu alianza kumweleza Pengo nia ya ujio wake na mambo aliyoelezwa na jitihada zake za kutaka kuzungumza na Mkapa juu ya suala hilo.Alipofika hapo Mwalimu alishindwa kuvumilia na kutoa machozi.."yaani leo Ben ananijia mimi amelewa??..mimi?" akamtazama Msaidizi wa Pengo huku macho yamejaa machoziakamwambia "Kamuulizeni nimemkosea nini Mimi kunifanyia hivyo?".Kwa jibu fupi lakini zito na huku amesononeka Pengo akasema "Mwalimu...nitalifanya hilo personally"...Baada ya hapo walipoona hali ya Mwalimu imekuwa ya kawaida baada ya kulitoa dukuduku lake,Mwalimu alimuomba radhi Pengo kwa hali ile na kuomba ruhusa kuondoka.

Ujumbe ulimfikia Mkapa kupitia kwa Pengo na hili alilifanya kama kiongozi wa kiroho.lakini bado katika hali ya kushangaza Mkapa hakwenda tena nyumbani kwa Mwalimu kumuona.

Wiki hiyo hiyo mwalimu baada ya kutoka kanisani kanisa la St Peter Oysterbay alikwenda nyumbani kwake Msasani na baadya ya kifungua kinywa alimwambia msaidizi wake kuwa anahitaji kwenda ikulu mara moja....

JE BAADA YA KUFIKA IKULU NINI KILIENDELEA?...KWA NINI MWALIMU ALIENDA BILA MIADI NA OFISI ILE? NA KWA NINI ALIENDA BILA KING'ORA NA GARI LA WALINZI TU? TUWE NA SUBIRA...
3.KIZAA ZAA NDANI YA IKULU
Katika msafara ule ni watu wachache waliofahamu ujio wa Mwalimu Ikulu.Wakati Mwalimu anafika nje wa viwanja vya Ikulu,Mkapa alikuwa na wageni kutoka shirika la Oxfam la Uingereza ikiwa ni moja ya shughuli zilizokuwa kwenye ratiba ya rais kwa siku ile.Hivyo kwa kipindi hicho anawasili Mwalimu mazungumzo ya Mkapa na ugeni wake yakiendelea ndipo alipofuatwa na mmoja wa makatibu wa Rais na kumnong'oneza juu ya kuwepo kwa Mwalimu pale ikulu kitu kilichomfanya Mkapa kuomba radhi kwa wageni wake na kutoka kwa haraka na kumfuata Mwalimu katika Private Office ya rais(OBR 1).Baada ya salamu tu Mwalimu aliomba kuwa na mazungumzo ya faragha na Rais hivyo walibaki tu wale wanaoruhusiwa na itifaki kuwepo katika mazungumzo ya aina hiyo.

Inasemekana katika maisha ya serikalini siku hiyo mwalimu alikuwa ni mkali sana.Alimweleza sehemu alizopita na kuzungumza suala hili na kutaka kujua sababu za Mkapa kumdharau kiasi hicho na isitoshe pamoja na ujumbe toka kwa kardinari Pengo bado alionyesha kutokujali wito wa Nyerere.Inasemekana Mkapa wakati wote wa mazungumzo hayo alikuwa kimya na kujibu kwa uchache sana maswali ya Nyerere tena kwa kutazama chini na kila wakati kujifuta jasho pamoja na viyoyozi vilivyokuwepo.Mwisho wa mazungumzo yale Mwalimu alimweleza Mkapa,

"Ben ! umenidhalilisha sana,umenisaliti...sijui nitaweka wapi uso wangu"...sasa nasema hivi maliza kiporo chako hiki ukapumzike...tumpate mtu serious hapa..!" Alimaliza kuzungumza akiwa tayari wima na kutoka nje ya ofisi ile.Kwenye korido za ikulu mwalimu alionekana akitembea kwa haraka kuelekea nje tayari kupanda gari lake na hakusalimiana na yeyote wala kuzungumza lolote zaidi ya kutoa ishara ya kupunga mkono kwa waliokuwa wakimsalimia.
Alirudi Msasani akionekana kuwa na mawazo na macho kuwa mekundu,nywele kuwa katika hali ya kuvurugika kiasi fulani....
Kuna la kujifunza tena hapa
 
Aiseee 😲😲
 
KIFO CHA BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE, SIRI ZAVUJA- GAZETI LA JAMHURI

*Ndugu walitaka apelekwe China, Mkapa akagoma

*Profesa Mwakyusa alimtelekeza, Gachuma akajitosa

*Mazingira ya kutia mashaka yaelezwa, hali inatisha

Na Waandishi Wetu, Musoma

Baada ya Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere (Chadema), kumtaka Rais mstaafu Benjamin Mkapa aeleze kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kilitokana na nini, ndugu mwingine ameibuka na kuishutumu Serikali ya Mkapa kuwa ilimtesa Mwalimu Nyerere kwa kutompa matibabu ya uhakika kutoka kwa daktari wake, Profesa David Mwakyusa.

Ndugu huyo aliyezungumza kwa masharti ya kutotajwa jina, amesema Profesa Mwakyusa, hakupata kwenda kijijini Butiama kumtibu Mwalimu wakati akiumwa, badala yake alimtumia daktari mmoja aliyetajwa kwa jina la Malima, kumtibu Mwalimu Nyerere. Dk. Malima anatajwa kuwa mmoja wa madaktari waliopendwa mno na Mwalimu na wakazi wengi wa Butiama.

Mwalimu aliugua, hali ikawa mbaya, Profesa Mwakyusa hakupata kwenda Butiama kumtibu, badala yake akawa anamtumia Dk. Malima. Alikuwa akitibu kwa kutumia simu. Huyu ndiye mtu ambaye tunaweza kusema alimsaidia Mwalimu kuongeza siku za kuishi.

Dk. Mwakyusa alienda Butiama siku alipoambiwa hali ya Mwalimu inazidi kuwa mbaya, ndipo akapanda ndege, wakaja wakamchukua na kwenda naye Dar es Salaam.

Lakini wakati huo mfanyabiashara, Christopher Gachuma, alishakwenda kumjulia hali Mwalimu. Akamkuta anataabika kweli kweli. Nakumbuka nilikuwapo na Gachuma alilia machozi. Akamweleza Mwalimu, naomba Mwalimu nikupeleke Nairobi ukatibiwe. Mwalimu akakataa kata kata, akasema; "kama hawataki... hawa hawataki kunitibu niache nifie hapa hapa nyumbani kwangu". Gachuma alimbembeleza sana, lakini Mwalimu alikataa, amesema ndugu huyo.

Ndugu huyo amesema kwamba siku chache baadaye, walimu wawili waliomfundisha Mwalimu Nyerere - Mwalimu James Irenge na Mwalimu Kirigini - walifika nyumbani kwa Mwalimu, Mwitongo kumjulia hali mwanafunzi wao (Mwalimu Nyerere).

Nakumbuka siku hiyo walikwenda moja kwa moja hadi chumbani. Wakakuta Mwalimu anateseka kwa maumivu makali. Walimu wale walilia machozi. Wakamwuliza Mwalimu kuhusu matibabu, akawajibu kuwa mipango inafanywa apelekwe Uingereza. Wakakataa wakisema huko ni hatari, bora apelekwe China, amesema ndugu huyo.

Mwalimu Kirigini alifariki dunia miezi kadhaa baada ya Mwalimu Nyerere kufariki dunia.

JAMHURI lilipowasiliana na Gachuma, alisema yeye alitoa wazo la kumpatia matibabu baada ya kukuta yupo kitandani anaumwa, na yeye kama Mjumbe wa NEC alikuwa na wajibu wa kumjulia hali kiongozi wake.

Nilikwenda kumuona, alikuwa anaumwa. Kimsingi nilichomwambia nikasema Mwalimu kuliko kukaa hapa nyumbani ni bora ukatafuta 'second opinion' ya madaktari, akaniambia tayari serikali imekwishamfanyia 'appointment' ya kumpeleka nje, alisema Gachuma na kuongeza:

Alikuwa kitandani anaumwa, ila baada ya siku moja au mbili nilipotoka pale [nyumbani kwa mwalimu] ndipo alipopelekwa nje ya nchi.

Jamhuri ilipowasiliana na Profesa Mwakyusa aliyekuwa daktari binafsi wa Mwalimu Nyerere kwa njia ya simu jana, lakini baada ya salamu mambo yalienda hivi:

Mwandishi: Profesa baadhi ya wanafamilia ya Mwalimu Nyerere wanasema ulimtelekeza baba yao, ulikuwa humpi matibabu inavyostahili.

Prof. Mwakyusa: Sikusikii vizuri, naongea na nani?

Mwandishi: Profesa naitwa Balile

Prof. Mwakyusa: Unasemaje? Nipo kwenye gari Ruvu sikusikii.

Baada ya kusema hivyo, Mwandishi alimtumia ujumbe (SMS) huu: Profesa shikamoo. Naitwa Deodatus Balile, Mhariri Mtendaji wa gazeti la JAMHURI. Muda mrefu nakutafuta. Tumepata taarifa kutoka familia ya Mwalimu Nyerere na wanasema wakati Mwalimu anaumwa ulimtelekeza ukawa unamtuma Dk. Malima badala ya kumtibu wewe kama daktari wake. Unasemaje? Asante.

Ujumbe huo ulionyesha kumfikia, na mwandishi alipompigia tena simu baada ya muda akapokea simu, na hata kabla ya kuitikia akasema: Nipo kwenye gari sikusikii vizuri naongea na nani? kisha akaiacha simu hewani huku zikiwapo sauti za matangazo ya mpira kuashiria alikuwa karibu na redio iliyofunguliwa sauti ya juu.

Kwa upande wake Dk. Malima, simu yake ilipokewa na mtoto, aliyeikimbiza kwa mtu mwingine aliyezungumza kwa sauti ya kike na kusema; Bado yuko hospitalini. Alipoulizwa angerejea nyumbani saa ngapi, mtu huyo alisema hajui. Baada ya muda siku ilizimwa.

Mwalimu wa Mwalimu Nyerere azungumza

Baada ya kauli ya Mbunge Nyerere kumtaka Mzee Mkapa aeleze chanzo cha kifo cha Mwalimu, Mwalimu Irenge amejitokeza na kusema amefurahishwa mno kusikia kuwa amepatikana kiongozi jasiri wa kuhoji namna Mwalimu alivyougua hadi kufariki dunia.

Mfikishieni pongezi nyingi Mbunge Nyerere... huyo mtoto amefanya jambo la maana sana kuuliza jambo hili, miaka yote nalia kwa sababu naamini Mwalimu aliuawa.

Kwa kuwa suala hili limeulizwa hadharani, sasa nipo radhi kufa. Nikifa nitakwenda moyo wangu ukiwa na furaha kwa sababu nimekuwa nikijiuliza ni nani anayeweza kuhoji namna Mwalimu mwanafunzi wangu alivyokufa, amesema Mwalimu Irenge mwenye umri wa miaka zaidi ya 120.

Mwalimu Irenge alianza kumfundisha Mwalimu Nyerere katika Shule ya Mwisenge kuanzia mwaka 1934 hadi 1936. Alistaafu kazi mwaka 1977. Tangu wakati huo anaishi jirani na shule hiyo. Mwanzoni mwa miaka ya 2000, Mwalimu Irenge alihojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) na kusema binafsi hakuafiki Mwalimu kupelekwa kutibiwa nchini Uingereza.

Alisema alipinga kwa sababu alijua Waingereza si marafiki wa kweli wa Mwalimu kwa kuwa aliongoza harakati za kuwangoa katika Tanganyika na katika mataifa mengine, hasa Afrika Kusini na Zimbabwe ambako Serikali ya nchi hiyo ilikuwa ikiunga mkono utawala wa kidhalimu wa Wazungu wachache.

Vincent Nyerere amkomalia Mkapa

Mbunge wa Musoma Mjini, Nyerere (Chadema), ametetea uamuzi wake wa kumtaka Rais (mstaafu) Mkapa aeleze mazingira ya kifo cha Mwalimu Nyerere, akisema ni Watanzania wengi ambao wamekuwa wakitaka kupata majibu hayo.

Katika mahojiano maalumu na JAMHURI yaliyofanyika Arumeru mkoani Arusha, Nyerere amesema Watanzania wanachotaka ni majibu ya swali alilomwuliza Mkapa.

Hapa hakuna ugomvi kama baadhi ya watu wanavyodhani, nilichofanya ni kuuliza swali, sasa ni wajibu wa Mkapa na wanaohusika kutoa majibu, tena majibu yanayojitosheleza. Kama Mzee Mkapa amekuwa akidanganya kwa miaka mingi, ajue sasa wananchi wanataka majibu, na mimi nimeanza kuingiwa na shaka juu ya uadilifu na ukweli wa Mzee Mkapa.

Kwenye msiba wa baba yangu Josephat Kiboko Nyerere, ndiye aliyenikabidhi ubani, sasa anaposema hanijui, hii inanipa shaka juu ya ukweli wa yale ambayo mara zote ameyasimamia, amesema Nyerere.

Amekiri kuwa kaka yake, Joseph Butiku amempigia simu na kumtaka amwache Mzee Mkapa.

Butiku ni kaka yangu, amenipigia simu, lakini nashukuru kwamba ametambua kuwa nilichofanya kwanza ni kujibu uongo uliotolewa jukwaani, kwamba mimi sina uhusiano na familia ya Baba wa Taifa. Mimi Mwalimu ni baba yangu mkubwa huo ndiyo ukweli hata kama Mkapa anataka au hataki.

Butiku akaniambia kuwa kama nilichokozwa nilikuwa na haki ya kujitetea. Kwa kweli nilichofanya ni kujitetea maana kama Watanzania wangeamini uongo kuwa mimi si wa familia ya Nyerere, hiyo ingeniathiri maana wananchi wasingeniamini. Lakini sasa ukweli umejulikana.

Uchunguzi wangu umebaini kuwa Mkapa alidanganywa na viongozi wa CCM. Yupo kiongozi alimwambia kuwa Nyerere ni mwiba jukwaani kwa hiyo atafute namna ya kumzima, hasa kwa kuwa anatumia jina la Nyerere.

Mzee Mkapa naye bila kujua akaingia kichwa kichwa, baadaye nasikia anasema huo ulikuwa utani. Jukwaani hakuna utani, sisi Chadema hatuna utani, kama wao (CCM) wanafanya utani, sisi hatujui utani, amesema.

Tendwa naye apigwa kombora

Nyerere alimgeukia Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, na kumtaka asiingilie masuala ya ukoo, badala yake aendelee na masuala ya vyama.

Tendwa kasema eti kumzungumzia Baba wa Taifa ni kuhatarisha amani katika taifa. Lakini anajua kuwa mimi nilishambuliwa kwa hiyo nilikuwa na kila sababu ya kujitetea. Yeye ni Msajili wa Vyama vya Siasa, si msajili wa ukoo.

Kwangu mimi kumzungumzia Mwalimu ni haki kwa sababu zaidi ya kuwa Baba wa Taifa, ni mlezi wangu. Nimesomeshwa kwa kutumia fedha za akaunti maalumu ya Mwalimu katika benki ya NBC. Akitaka kujua aende apitie rekodi za fedha zilivyokuwa zinatolewa ili nilipiwe ada. Hana mamlaka ya kunizuia kumtaja baba yangu mkubwa. Sasa hivi kuna sala maalumu, kwa hiyo anataka hata nisisali hiyo sala ya kumwombea Mwalimu? Amehoji.

Kwa siku kadhaa sasa, Nyerere ameibua mjadala mkali ndani na nje ya nchi kwa uamuzi wake wa kumtaka Mkapa aeleze ukweli wa kifo cha Mwalimu Nyerere.

Alisema Mkapa hawezi kutamba kuwa ni miongoni mwa watu wanaomuenzi Mwalimu, kwa vile baada ya kushika madaraka alihakikisha anauza viwanda na mashirika yote ya umma, vitu vilivyoasisiwa na Mwalimu.

Alitoa mfano wa Benki ya NBC iliyokuwa ya umma ambayo Mkapa aliiuza kwa bei ya kutupa kwa makaburu wa Afrika Kusini. Mwalimu aliongoza harakati za kuzuia kuuzwa kwa benki hiyo, na hadi anafariki dunia alikuwa haelewani na Mkapa juu kuuzwa kwa benki hiyo.

Mashirika ya umma zaidi ya 400 yaliyoachwa na Mwalimu yaliuzwa chini ya uongozi wa Mkapa wa miaka 10.

CHANZO:Gazeti la Jamhuri

Aiseee🤔🤔
 
JULIUS NYERERE, hakufa kifo cha kawaida.Aliuawa kwa sumu iliyopandikizwa ndani ya mwili wake.Siri hiyo anaijua Daktari wake na baadhi ya maofisa na wasaidizi wake.Alilazimishwa kwenda "kuangaliwa" afya yake na mara baada ya kutoka katika hospitali kwa "checking" hiyo na kuwasili alipofikia Guest wing London alianza kujisikia vibaya na hatimaye alianguka ghafla na kudakwa na mlinzi wake aitwaye Mkanzabi.Ndipo yalipofanyika mawasiliano ya haraka ili kumuwahisha hospitali.cha ajabu wakati anaondoka Tanzania, Mkapa alikuwa akijiandaa kwenda katika mkutano mmoja huko ulaya.alipozidiwa Mwalimu,Mkapa alipitia london kutokea Zurich,lakini kwa mujibu wa madai yake huyu bwana alidai hakuweza kumwona kwa karibu,ila alimwona kwa mbaaali.Hii inadhihirisha wazi kwamba alienda kumsanifu mzee huyo wa miaka 77 akiwa kitandani hoi.Aliporudi Tanzania alikutana na waandishi wa habari na kudai ikulu itakuwa ikitoa taarifa za maendeleo ya Mwalimu huku akisema kwa maneno ya mafumbo kuwa "Mwalimu is recovering slowly"(Dying slowly!).Wakaona mtu wa kumtuma kudhibiti yanayoendelea London ni Kingunge Ngombale Mwiru.Mzee huyu alipewa cheo kuwa mshauri wa Mkapa kuhusu siasa na mbunge wa kuteuliwa.
Mwalimu alifariki dunia na kuzikwa kwao butiama.
Mwaka mmoja baadaye (2000),mkapa alienda Butiama kuhani katika kaburi la Mwalimu.Yaliyotokea pale ni mauza uza ya ajabu ikiwa ni pamoja na kuvunjika kimaajabu kwa msalaba katika kaburi la Mwalimu!!.Yaliandikwa katika magazeti,lakini yalifichwa na kufunikwa.Toka Musoma,Mkapa alienda Mwanza na pale mnakumbuka palitokea ajali mbaya ya basi lililoacha njia na likawa linafuata gari alilopanda Mkapa.Walikufa watu wengi!
Miezi kadhaa baadaye Mkapa alianza kuugua maradhi yaliyomfanya akae nje ya Tanzania kwa muda wa miezi kadhaa kabla ya kurudi akitembelea magongo!!
Ikumbukwe kwamba baada tu ya Nkapa kwenda ulaya kwa matibabu ,nyumba ya Rais ikulu iliungua.Majanga haya ni matokeo ya aliyoyasimamia Nkapa juu ya kifo cha Mwalimu.
Yapo mengi wanayojua watanzania ila kwa hili tuishie hapa kwanza.

🤔🤔🤔 Aiseee!!
 
Duh nimepakua uzi woote huu tangia saa moja ndio nimemaliza sasahivi saa nne nimejifunza kitu,hakuna wakumuamini duniahiibzaidi ya mungu na mamayako tu
Hata mama anaweza kukugeuka

Hasa kama wewe sio kipenzi chake nambari moja
 
I have always failed to be convinced that Mwalimu Julius Kambarage Nyerere died "A natural death!"
Wakuu, mi nimelewa kabisa! Aliyeanzisha thread hii, ilikuwa tarehe 19/11/2010. Na ni siku hiyo hiyo ndiyo aliyo jiunga hapa JF. Kinachonishangaza, ni kuwa hajawahi kuandika chochote kingine, si kwa kuchangia kwenye thread za wengine, au kuongezea chochote kwenye hii thread yake. Yaani kwa miaka yote iliyopita, akaunti yake inasoma 1 tu. Au naye baada ya kuandika tu hii thread yake, naye AKAMFUATA MWALIMUUU!!!?
 
I have always failed to be convinced that Mwalimu Julius Kambarage Nyerere died "A natural death!"

Kuendelea kuficha sababu za marehemu kufa hasa kwa Corona na HIV, kutokujali umuhimu wa huduma za coroner, kutokuwepo na inquests kujiridhisha na sababu za vifo - kutawezesha hao wanaoficha kuendelea kuwa ndiyo washukiwa wa uchawa #1.
 
Back
Top Bottom