Dibaji ya kitabu cha visa na mikasa ya kesi maarufu duniani na hukumu zake toleo la kwanza

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
upload_2018-1-31_17-29-45.png

Visa na Vikasa ya Kesi Maarufu Duniani na Hukumu Zake ni mwanzo wa vitabu nitakavyokuwa nikivitoa kwa awamu ambapo vitabu hivyo vitakuwa na mkusanyiko wa kesi mbalimbali zilizowahi kutokea katika nchi mbalimbali duniani na kuvuta hisia za watu wengi.

Katika kitabu hiki cha toleo la kwanza kuna kesi nyingi za mauaji ambapo mengi yanahusisha masuala ya mapenzi na mahusiano pamoja na sababu nyingine za kibinadamu. Zipo kesi za mauaji zilizosababishwa na malezi ya watoto wetu kutokana na mkengeuko wa mahusiano ya kingono na mitandao ya kijamii.

Kesi hiyo inayowahusu mabinti wawili, Rachel na mwenzie Sara wa nchini Marekani inatufumbua macho kuchunguza mienendo ya watoto wetu katika mawasiliano ya teknolojia yanayohusisha mitandao ya kijamii. Kwetu sisi tunaweza kuchukulia kama jambo lisiloweza kutokea, lakini visa na minyukano ya kwenye mitandao ya kijamii inaweza kuhama kutoka vita vya nyuma ya simu za viganjani na kuwa vita vya uso kwa uso.

Zipo kesi nyingi ambazo zinatufumbua macho kuhusu jinsi upelelezi wa kesi mbalimbali unavyofanywa kwa umahiri mkubwa na hatimaye wahusika kukamatwa, kushitakiwa na kutiwa hatiani. Wakati mwingine mtu anaweza kupanga kufanya uhalifu kwa umakini mkubwa akidhani kwamba hataweza kukamatwa, lakini alama moja tu itakayoachwa na mhusika ni chanzo kizuri kitakachowezesha kukamatwa kwake. Teknolojia hivi sasa imerahisisha sana kupatikana kwa wahalifu wengi wa mauaji tofauti na miaka ya nyuma.

Miongoni mwa mikasa iliyopo katika kitabu hiki ni tukio la kuvutia la genge la Tupac Amaru na mateka ubalozi wa Japan nchini Peru. Katika utawala wake, Rais wa wakati huo nchini Peru, Alberto Fujimori, alifikia wakati jamii yake ikaamini amefanikisha kazi ya kukabili ugaidi nchini humo. Lakini haikuwa hivyo, Desemba 17, mwaka 1996 Peru, ndani ya mji mkuu wake wa Lima ilikumbwa na taharuki, baada ya magaidi hao kurudi kwa kishindo kikuu.

Ilikuwa imebaki wiki moja kabla ya kusherehekea Sikukuu ya Krismas ya mwaka 1996 ndipo balozi wa Japan nchini humo, Morihisa Aoki, akafanya uamuzi wa kuandaa sherehe ili kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mfalme wa nchi hiyo.

Bustani iliyoko katika jumba la kifahari katika viunga vya Jiji la Lima alipokuwa akiishi balozi huyo, ilikuwa imejaa wageni waalikwa wenye nyuso za furaha, wakiwa na matumaini ya kumaliza mwaka salama.

Wakati sherehe ikiendelea, ghafla ulitokea mlipuko. Kikosi cha wavamizi hao 15 kilivamia jengo hilo alilokuwa akiishi balozi wa Japan wakitokea jengo la jirani kwa kutoboa ardhi chini kwa chini na kuibukia katika jengo la balozi huyo, wakiibukia sebuleni. Kitendo hicho kilibatizwa jina na na wananchi wa Peru kama “El Sequestro del siglo” yaani utekaji nyara wa karne. Kwa undani zaidi utaweza kuyapata haya kwenye kitabu hiki.

Lakini vile vile kuna kisa cha profesa wa wadudu namna alivyofanikisha upelelezi wa kesi ya Vincent Brothers wa New York- Marekani. Hii ilichapishwa gazetini Agosti, mwaka 2013.

Vincent alifunga ndoa na Joanie Harper. Hata hivyo, ndoa yao ilivunjika mwaka mmoja baadaye kutokana na kile kinachodaiwa Vincent kutokuwa mkweli kwa Joanie aliyedai mumewe huyo hakumweleza kuhusu ndoa zake mbili zilizovunjika huko nyuma. Hata hivyo, walioana tena mwaka 2003, lakini Vincent alihama katika nyumba waliyokuwa wakiishi na mkewe huyo, April 2003.

Maisha yao ya ndoa hayakuwa ya amani, ingawa Joanie Harper alikuwa akimpenda sana Vincent na alitamani siku moja ndoa yao iwe imara. Inadaiwa Vincent aliua wanafamilia wake. Kitendawili ambacho wapelelezi wa kesi hiyo walitakiwa kukitegua ni kuthibitisha kama Vincent alikuwa Bakersfield, California wakati mauaji ya familia yake yakitokea au alikuwa Ohio kama alivyodai. Polisi walikuwa na uhakika Vincent ndiye aliyeua familia yake na hiyo ilitokana na taarifa kutoka kwa jirani yake mmoja aliyedai kumuona Vincent akiwa nje ya nyumba inapoishi familia yake hapo Bakersfield muda yalipotokea mauaji.

Askari upelelezi walianza kufuatilia safari ya Vincent kutokea Barkersfield hadi Columbus Ohio. Askari hao waliamini Vincent alipanga safari hiyo makusudi ili kutengeneza mazingira kwamba wakati mauaji yanatokea hakuwapo katika mji husika.

Waligundua Vincent alisafiri kwa ndege hadi Ohio Julai 2, 2003, alikodi gari aina ya Dodge Neon katika Kampuni ya Doller Rent –A-Car. Polisi walipofuatilia kampuni hiyo waligundua wakati gari hilo likiwa mikononi mwa Vincent liliendeshwa umbali wa maili 5,400, umbali ambao unatosha kabisa kwa Vincent kwenda Bakersfield na kurudi Ohio na ziada. Pia Polisi hao walibaini Vincent aliendesha gari hilo kwa umbali wa maili 4,500 kwa siku tatu. Lakini Vincent alizidi kusisitiza hakuwahi kutoka nje ya Ohio.

Vincent alidai wakati mauaji yanatokea alikuwa umbali wa zaidi ya maili 2,300 na kuhoji ingewezekana vipi awepo katika mji wa Bakersfield mchana wa Julai 6, 2003 auwe familia yake na kisha kurudi Ohio jioni ya Julai 7, Julai wakati hata kaka yake anakiri siku hiyo ya mauaji alikuwa Ohio?

Iliwachukua polisi takriban miaka mitatu kukusanya ushahidi wa kumtia hatiani Vincent. Askari wawili wa FBI walikuwa na uhakika Vincent ndiye muuaji, lakini ilikuwa vigumu kwao kuthibitisha Vincent alikuwa Bakersfield Califonia siku yalipotokea mauaji na si Ohio.

Ilibidi kumhusisha Profesa wa wadudu katika upelelezi. Askari wa upelelezi wa FBI walipata wazo la kupeleka rejeta na air filter ya kuchuja hewa ya gari alilokuwa amekodi Vincent alipokuwa Ohio kwenye kituo cha uchunguzi wa wadudu cha Bohart Museum Entomology ambako Profesa Lynn Kimsey, aliongoza kazi hiyo ya uchunguzi ambao ndio uliotegua kitendawili hicho.

Wapelelezi hao wa FBI waliamini kwamba Profesa Kimsey angeweza kuwaambia aina ya wadudu waliokuwa wamenasa kwenye rejeta na air filter na wanapatikana wapi hapo Marekani. Kwa kawaida wadudu hutambuliwa na wataalamu kutokana na chimbuko lao (species) na eneo wanaloishi kijiografia.

Katika ripoti yake Profesa Kimsey alibaini baadhi ya wadudu waliokutwa kwenye vifaa hivyo wanapatikana eneo la Magharibi, na wengine waliokutwa katika vifaa hivyo hupatikana kwa wingi katika eneo la California.

Kuonekana kwa wadudu hao kulibainisha kwamba gari hilo liliendeshwa usiku kuelekea California na si mchana. Kwa ujumla Profesa huyo alikamilisha ripoti yake kwa kusema, hakuna wadudu wanaoruka mchana waliokutwa kwenye vifaa hivyo.

Huo ulikuwa ni ushahidi wa kitaalamu ulisababisha Vincent kufikishwa mahakamani na kushitakiwa kwa kosa la kuua familia yake. Matukio yote haya na mengine yamekuwa na mvuto mkubwa na bila shaka, yataendelea kubaki katika mvuto wake kwenye kitabu hiki.

Jipatie nakala yako mapema kwa bei ya TZS 10,000/= tu. Unaweza kuwasiliana na muandishi kwa namba hii- +255 782 555 709

Shaban Kaluse (Mtambuzi)

Dar es Salaam
 
10000 tuuuu
Tuuuu
Ngoja mi nitangazie tu wengine mtanipa cha bure cha tangazo hili langu
10 tuuuuuuu
Only kumi
 
Sasa kwa nini tangazo lako uweke jukwaa la sheria. Kwa nini usiweke jukwaa la matangazo. Kwa kuwa mods upo nao hapo pichani najua Uzi huu hautahamishwa ila kajamba nani nyuzi zinahamishwa tena bila taarifa.
 
View attachment 688167

Bado kipo?
 
Back
Top Bottom