Diaspora, Wanasiasa, Wajasiriamali... Fursa

Zainab Tamim

JF-Expert Member
Jan 15, 2015
1,293
583
Kwanza napenda ku "declare interest". Kama kuna ex-diaspora basi mimi nime qualify.

"Opportunity is rare, grab it when it appears".

Hivi karibuni tulianzisha mjadala wa tulioupa kichwa cha habari "Fursa ya kukopa kukopesha kwa faida bila riba". Mjadala huo na baada ya kukutana na wadau wengi wa maendeleo tukahitimisha kuwa tufungue "Open SACCOS" haraka iwezekanavyo kwa faida ya wengi.

"Open SACCOS" kwa maana kuwa haitakuwa na mipaka ya uanachama na kiwango cha uwekezaji.

Tumeanza mchakato wa kujiandikisha rasmi kisheria SACCOS yetu mpya.

SACCOS itakuwa haikopi wala kukopesha kwa riba kwa wanachama wake wote.

Malengo ya chama ni pamoja na;

- SACCOS kuiwezesha jamii ki maendeleo ndani na nje ya wanachama wake.
- kuelimisha jamii na wanachama fani mbali mbali kwa nadharia na vitendo.
- kuwekeza kwa niaba ya wanachama katika misingi bora ya kuzingatia nidhamu, uwekezaji kwa ufanisi.
- kuwezesha miradi ya wanachama kwa misingi isiyo na riba.
- kusimamia kiuaminifu miradi ya wanachama waliopo na wasio kuwepo au walio na kazi na hawana muda wa kusimamia miradi yao kwa ubia na au malipo tutayokubaliana.
- kunyanyua maisha ya kila mwanachama kwa kubuni njia zitakazozingatia nidhamu na uaminifu wa hali ya juu (professionalism).

Hayo ni kwa uchahe na mengine mengi yatakayoamuliwa na kukubaliwa na wanachama kuwa ni yenye faida.

Nimewataja diaspora kwa kuwa nina uzoefu wa kuishi nje ya Tanzania na ninaelewa tulivyokuwa tukitiwa "changa la macho" na wale tuliowaamini kutufanyia shughuli zetu za kimaendeleo hapa nyumbani. Wengi tulilizwa.

Kwa kuelewa hayo, napenda diaspora wajiunge kwa wingi na waelewe kuwa sasa, wana mkombozi, chama kamili, kitakacho tazama maslahi ya wanachama wake kwa faida ya wengi.

Nimewataja wanasiasa kwa kuwa ningependa wanasiasa watuunge mkono kwa jitihada zetu hizi bila kujali vyama vyao.

Tunakaribisha maswali yoyote.

Tumeshaanza kupokea wanachama wapya kuanzia tarehe 1 May 2017.

Karibuni sana.

Abdul
+255 625 249605
 
Zainab Tamim Verified User

Inakuwaje hitimisho la maelezo unamalizia na;

Abdul
+255 625 249605

FAFANUA TAFADHALI!!!!

Posts za juu huko nilielezea hilo.

SACCOS yetu mpya wamemchagua Mzee Abdul kuwa ni Mwenyekiti wa muda, mpaka chama kitakaposajiliwa rasmi, kwa sasa mambo ya saccos karibia yote anayajibu yeye, na ili kuondoa utata anapojibu yeye anaweka jina lake.

SACCOS ikishasajiliwa rasmi watajisajili humu kwa jina lao.
 
Bi Zainab Tamim na Abdul, kwa hawa wanasiasa mnajihangaisha tu, wengi wao ni wanafiki, tazama mtakapopata mafanikio mtawaona wao ndiyo kimbelembele utafikiri wameanzisha wao hiyo saccos, subiri utanambia.

Nnakushauri achana nao na kama watajiunga basi wawe kama wanachama wengine tu na wasiingize siasa zao kwenye hili.
 
Wadau wote,

Tunapenda kuwajulisha kuwa mpaka sasa tumeshasajili wana saccos zaidi ya 40 na tunaendelea kusaiili wana saccos wapya kila kukicha, kutoka sehemu mbali mbali za Tanzania na duniani kwa ujumla. Diaspora wengi wameanza kuitikia mwito wetu.

Pia tunapenda kuwafahamisha kuwa yeyote ataeungana nasi kwa sasa, tutamuingiza katika group letu jipya la "Biashara Vitendo SACCOS" (licha ya lile la "Vitendo SACCOS") ambalo unaungwa automatically unapojiunga tu na SACCOS yetu mpya.

Humo utaweza kutangaza biashara zako binafsi nasi pia tutasaidia kuzitangaza tena kwenye mitandao ya kijamii na baadae tutaziweka kwenye website yetu itakapokuwa tayari.

Karibuni sana wadau.

Ada ya kiingilo kwa sasa ni shillingi 10,000 (elfu kumi) ambazo zitatumwa kwa Mwenyekiti wa muda kwa njia ya Mpesa. Namba ni 0756803528 jina Ghafur Abdallah Mohamed.

Unaweza kupitia hapa: Fursa ya kukopa kukopesha kwa faida bila riba
 
View attachment 566354

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kongamano la nne la kitaifa la Watanzania wanaoishi nje litakalofanyika tarehe 23 na 24 Agosti hapa Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika Ikulu mjini Zanzibar.

Mkurugenzi wa PPR Pascal Mayalla akiuliza suali katika mkutano na waandishi wa habari uliozungumzia Kongamano la kitaifa la Watanzania wanaoishi nje uliofanyika Ikulu mjini Zanzibar.

Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi Bi. Adila Hilali Vuai akijibu masuali yaliyoulizwa na wandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kongamano la kitafa litalofanyika tarehe 23 na 24 Agosti hapa Zanzibar. (kushoto) Muandishi wa habari Rahma Suleiman wa Chuchu Fm Redio.
Picha na Makame Mshenga.
Wanabodi.

Declaration of interest. Japo mimi Paskali Mayalla sio mwana Diaspora, bali nimewahi kuishi nje kwa muda mfupi mfupi katika nchi mbalimbali, na nimewahi kufanya kazi tena sio kubeba box, bali kubeba zege ndani ya jiji la London, hivyo nina mwanga kidogo kuhusu diaspora, ila kwenye hili
Kongamano la Nne la Diaspora, litakalo fanyika Zanzibar, tarehe 23 na 24 Agosti, I have a role to play.

Hivyo hili ni bandiko la kuomba ushirikiano wenu, kwa ushiriki wako kwenye kongamano hili, physically or by proxy, ili kutoa mawazo yako Tanzania ikusaidiaje ili kukuwezesha wewe kuisaidia nchi yako.

Tanzania itajengwa na Watanzania wote wakiwemo wana diaspora. Kitu cha kwanza ni kuomba ushiriki wako physically kwa wale wenye nafasi to make it home, wajisajili kupitia
DIASPORA: Home Page
or
4TH Tanzania Diaspora Conference 2017 - Diaspora and SMEs ...

Kwa wale ambao hawatapata nafasi ya kuwepo physically, wanaweza kushiriki by proxy, kwa vile dunia sasa ni kijiji kimoja, wanaweza kushiriki by proxy.

Kwanza The Official Opening ya Kongamano lenyewe litatangazwa live za TV za Tanzania. Pili tutatangaza live kupitia video streaming kwenye youtube hivyo wana diaspora wote wenye nafasi wanaweza kufuatilia kupitia youtube, facebook, tweeter na mitandao ya kijamii.

Hapa naomba ushirikiano wako tujadiliane how to reach you out ili tupate maoni na mawazo yako, Tanzania ikusaidiaje wewe mwana Diaspora ili uweze kuisaidia nchi yako?.

Uzalendo sio kujiuliza "Tanzania Ikusaidie nini, bali ni wewe kujiuliza jee nimeisaidia nini nchi yangu Tanzania?". Kwa vile wana diaspora wengi wako nchi za nje na wamepata bahati ya kupata exposure kubwa, tunaomba mawazo yenu, Tanzania iwasaidieje ili muweze kuisaidia nchi yako Tanzania.

Natanguliza Shukrani.

Pascal Mayalla
+255 784 270403
pascomayalla@gmail.com
 
Mkuu kwenye hili swala huwa najiuliza maswali mengi sana sana huwa sipati jibu.

Kwanza ROI kwenye makongamano matatu yaliyopita, nini ni matokeo yake? Sbabau kila kongamano lina ajenda zake sasa matunda ya makongamano yaliyopita yako wapi?

Pia hawa diaspora kisheria wala kikatiba hawatambuliki kwenye nchi hii wala hata michango yao. Sasa tena inakuwaje tunapoteza pesa nyingi kuwanaandaliwa makongamano wakati hawaruhusiwi kuhodhi ardhi, shamba wala hata kibanda cha makuti tu cha kuuzia mkaa.

Hivi mkuu! hukumuuliza huyu bwana mkubwa Mh. Salum Maulid Salum kuwa haya mambo yanapingana na sheria pamoja na katiba ya nchi?

Kuna vivutio gani walivyowawekea ili Diaspora waje kuwekeza kwenye viwanda vidogo?

Kuna uhakika gani wa usalama wa uwekezaji wao? Ijapokuwa serikali yetu haiheshimu sheria, je hivi vitu viko kisheria na ni sheria zipi?

Kwanini nasema hivyo yule Mzee wa Msoga alitembea miji yote ya Ulaya na Amerika kuhimiza shime shime ya uwekezaji hapa nyumbani. Vijana wale wakabeba mabox ya kuvunja mgongo kuja kuwekeza nyumbani halafu ghafla alipokuja huyu bwana mkubwa wa sasa unajua kilichowapata.

Mkuu, hizi ndizo hoja wanazotakiwa kuja nazo mezani hao wana diaspora ili kupata majibu ya kina.
Karibu Zanzibar,
4TH Tanzania Diaspora Conference 2017 - Diaspora and SMEs ...

Paskali
 
Update...

Wadau,

Kwanza tunashukuru AlhamduliLlah mkutano umeenda vizuri na umeisha salama.
Tunafuraha kuwafahamisha wadau wote kuwa mkutano umeenda vizuri kabisa na umefana sana.

Tulianza kwa kukaribishwa na Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Vitendo...

Kisha nikaongea kidogo mimi kuwakaribisha wajumbe wote...

Baada ya hapo ikaanza semina ya ushirika iliotolewa na Afisa Ushirika wa wilaya ya Kibaha, Bwana Msangi. Semina ilikuwa ndefu kidogo lakini ilitoa mwangaza mpana wa nini SACCOS, vipi iongozwe, nini haki za Wana SACCOS na vipi haki zao zinalindwa na kusimamiwa na sheria rasmi za vyama vya ushirika na vipi serikali inasimamia vyama vya ushirika.

Yalizuka maswali mengi kiasi na hususan lilipoongelewa suala la kuendesha SACCOS kwa riba.

Hatimae kila mtu akaelewa kuwa hakuna tatizo kubwa isipokuwa ni namna tu ya mfumo wa uendeshaji SACCOS bila riba utavyofanyika.

Hilo na mengine yaliojiri mtajionea mkanda wa video.

Baada ya semina ukaanza mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa muda. Ulioendeshwa na kusimamiwa na Afisa Ushirika kama sheria zinavyotaka.

Hatimae tukapata kamati ya uongozi wa muda ya uanzilishi wa Vitendo SACCOS Ltd., kwa mujibu wa Sheria na chini ya usimamizi wa Afisa Ushirika wilaya ya Kibaha.

Kamati hio ya muda ikamteua Katibu wa kwanza wa muda wa Vitendo SACCOS Ltd., chini ya usimamizia wa Afisa Ushirika wilaya ya Kiabaha.

Mambo yote hayo yapo kwenye video na picha. Zitakapokuwa tayari, tutapandisha video YouTube na kwenye tovuti yetu (inayoanadaliwa kwa sasa) tutapandisha video na picha.

Tunakaribisha maswali.

Asanteni na karibuni kujiunga na Vitendo SACCOS Ltd. kwa faida ya wengi.

Abdul Ghafur
Mwenyekiti
Mobile / Whats-app 0625249605
 
Wadau...

Tumeanza kupokea wanachama kiukamilifu, kiingilio, hisa na akiba. Na uwekezaji kwenye miradi mbali mbali.

Kwa maelezo zaidi whatsapp au piga 0625249605
 
Wanachama na Wana hisa wa Vitendo SACCOS wanategemea kuzindua na kuanza kazi miradi yao mitatu mipya hivi karibuni.

Miradi hiyo mitatu yote iliyo nje ya Vitendo SACCOS lakini imebuniwa na Wana VTS na itaendeshwa kwa njia ya kuchangiana mitaji na kugawana faida kwa muda maalum.

Miradi inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ni, mradi wa ukumbi wa sinema na mikutano, unaoweza kukaa watu 100, unatambulika kama mradi wa Vitendo Cinema Hall. Huu ni mradi wa muda mfupi kwa waliowekeza. Inatarajiwa kuwa mara tu utakapoanza hivi karibuni, wote waliowekeza kwenye mradi huu kuanza kupata mafao yao na faida ndani ya miezi sita.

Mradi mwingi unaotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni unaojulikana kwa jina la Vitendo Bricks, mradi huu ni wa muda wa kati. Mradi huu utajumuisha utengenezaji wa matofali ya aina tofauti tofauti na pia kwa siku za mwanzoni unatarajiwa kuwa na bidhaa tofauti zinazotokana na mchanga, kokoto na simenti.

Mradi huo pia unatarajiwa kuwa na uwezo wa kutengeneza bidhaa zote za ujenzi zinazotokana na simenti, kokoto na michanga.

Mradi mwengine kuanza hivi karibuni ni mradi wa kijiko (excavator) ya kuchimba na kupakilia mchanga. Mradi huu upo kwenye matayarisho ya mwisho na unategemewa kuanza hivi karibuni. Huu ni mradi unaotarajiwa kuanza kulipa mafao ya wawekezaji na kukamilika ndani ya siku 365 za kazi.

Tunawakaribisha nyote kujiunga na Vitendo SACCOS Ltd. Kwa faida ya wengi.

Vitendo SACCOS imedhamiria kufanya mabadiliko ya uwekezaji Tanzania. Na sasa unaweza kuanza kuwekeza na VTS kwa kuanzia Shillingi 10,000 tu.

Kwa maelezo zaidi, wasiliana nasi kwa simu au whatsapp namba 0625249605.

Ahsanteni sana.
 
Back
Top Bottom