Tetesi: Diaspora wajipanga kuhakikisha kumtetea Rais Samia

FbUser

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
431
626
Kundi la Watanzania wanaoishi nje ya nchi kupitia mtandao uitwao Green Advocates limejipanga kuhakikisha Rais wa sasa Dk Samia Suluhu Hassan anakuwa ndio mgombea wa CCM na kupata ushindi mkubwa 2025.

Green Advocates ambalo lilianza kundi la What's App 2017 likionyesha msimamo wa kuwa neutral kwenye siasa za Tanzania ndio kundi pekee la Diaspora ambalo lilitoa tamko la kulaani kupotea kwa Ben Saanane.

Kundi hili linaundwa na Watanzania wa nchi za Marekani Ubelgiji Ufaransa,Canada, Uingereza,Ujerumani,Kenya Afrika Kusini Norway Japan na China.

Taarifa za awali kuhusu hatua hiyo ambazo zimevuja ni kwamba ni kwamba kikao cha wajumbe kupitia zoom cha tarehe 22 Novemba mwaka jana kamati ya watu 15 ikiongozwa na Mwenyekiti Injinia Tumaini Kitogo kutoka China ilifikia maamuzi ya kumsaidia Rais Samia baada ya kujuvujishiwa siri kuwa serikali inajipanga kupeleka muswada wa uraia wa nchi mbili Bungeni kabla ya 2025 au baada ya hapo.

Tayari mikakati ya kuhakikisha jambo hilo halikwami kwa upande wa Tanzania Green Advocates wameunda kamati nyingine hapa nchini yenye watu 11 ikiongozwa na Mwenyekiti mwandishi Albert Kawogo na Katibu Anna Gwambasa na kiasi cha bajeti kinatengwa kwa ajili ya propaganda za online media Tv na magazeti.

Habari zinaeleza kuwa chokochoko za baadhi ya wanaCCM kuhusu nafasi ya Mama Samia kwenye Urais 2025 zimefanya Diaspora hao kuona umuhimu wa kuingia moja kwa moja kwenye kampeni japo bado mipango yao hii ina usiri mkubwa hasa kwakuwa baadhi ya wahusika wa mpango huu ni viongozi wa vyama vya upinzani kwenye matawi ya Diaspora huko ughaibuni.

Kiasi cha zaidi ya Trilioni moja kichoweza kuwekezwa na Diaspora kimekwama kutokana na vikwazo vinavyoletwa na uraia pacha ambapo Tanzania haijaridhia sheria hiyo.
 
Back
Top Bottom