Diaspora Property Management Company in Tanzania

MAISAKI

Member
Apr 10, 2012
9
5
TERRANOVA COMPANY (T) LIMITED

www.terranova.co.tz

Great thinkers, I recently came across this real estate company in Tanzania that does property management for Tanzanians living abroad. There are many problems that we Tanzanians who live or have lived abroad get when we leave our most valued assets/properties to kith and kin. You find your property vandalised, washed out and in near zero value. I remember when I came back to Tanzania and found the garden at my house dried out. They also sold a big part of my plot which I had plans for. I wish I knew these guys before.

Katika pita pita zangu nimekutana na hii kampuni ya real estate iliyopo Tanzania ambayo inasaidia kuangalia nyumba na hata viwanja vya watanzania wanaoishi nje ya nchi. Kuna adha nyingi sana tunazipata sisi Watanzania tuliowahi kuishi nje na kuachia ndugu au jamaa mali zetu za thamani kama hizi na mwisho wa siku unakauta nyumba imechakaa, imenyofolewa vitu, imegeuka hadi rangi. Nakumbuka nilirudi kutoka nje nikakuta hadi garden yangu haipo kabisa, ilikauka kama jangwa flani. na kiwanja changu waliuza sehemu kubwa na kubakisha hapo kidogo tu. Kwakweli unaweza kugombana na ndugu zako kisa mali zako. Natamani sana ningewaju hawa watu kabla.
 
View attachment 566354


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kongamano la nne la kitaifa la Watanzania wanaoishi nje litakalofanyika tarehe 23 na 24 Agosti hapa Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika Ikulu mjini Zanzibar.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kongamano la nne la kitaifa la Watanzania wanaoishi nje litakalofanyika tarehe 23 na 24 Agosti hapa Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika Ikulu mjini Zanzibar.

Mkurugenzi wa PPR Pascal Mayalla akiuliza suali katika mkutano na waandishi wa habari uliozungumzia Kongamano la kitaifa la Watanzania wanaoishi nje uliofanyika Ikulu mjini Zanzibar.

Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi Bi. Adila Hilali Vuai akijibu masuali yaliyoulizwa na wandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kongamano la kitafa litalofanyika tarehe 23 na 24 Agosti hapa Zanzibar. (kushoto) Muandishi wa habari Rahma Suleiman wa Chuchu Fm Redio.
Picha na Makame Mshenga.
Wanabodi.

Declaration of interest. Japo mimi Paskali Mayalla sio mwana Diaspora, bali nimewahi kuishi nje kwa muda mfupi mfupi katika nchi mbalimbali, na nimewahi kufanya kazi tena sio kubeba box, bali kubeba zege ndani ya jiji la London, hivyo nina mwanga kidogo kuhusu diaspora, ila kwenye hili
Kongamano la Nne la Diaspora, litakalo fanyika Zanzibar, tarehe 23 na 24 Agosti, I have a role to play.

Hivyo hili ni bandiko la kuomba ushirikiano wenu, kwa ushiriki wako kwenye kongamano hili, physically or by proxy, ili kutoa mawazo yako Tanzania ikusaidiaje ili kukuwezesha wewe kuisaidia nchi yako.

Tanzania itajengwa na Watanzania wote wakiwemo wana diaspora. Kitu cha kwanza ni kuomba ushiriki wako physically kwa wale wenye nafasi to make it home, wajisajili kupitia
DIASPORA: Home Page
or
4TH Tanzania Diaspora Conference 2017 - Diaspora and SMEs ...

Kwa wale ambao hawatapata nafasi ya kuwepo physically, wanaweza kushiriki by proxy, kwa vile dunia sasa ni kijiji kimoja, wanaweza kushiriki by proxy.

Kwanza The Official Opening ya Kongamano lenyewe litatangazwa live za TV za Tanzania. Pili tutatangaza live kupitia video streaming kwenye youtube hivyo wana diaspora wote wenye nafasi wanaweza kufuatilia kupitia youtube, facebook, tweeter na mitandao ya kijamii.

Hapa naomba ushirikiano wako tujadiliane how to reach you out ili tupate maoni na mawazo yako, Tanzania ikusaidiaje wewe mwana Diaspora ili uweze kuisaidia nchi yako?.

Uzalendo sio kujiuliza "Tanzania Ikusaidie nini, bali ni wewe kujiuliza jee nimeisaidia nini nchi yangu Tanzania?". Kwa vile wana diaspora wengi wako nchi za nje na wamepata bahati ya kupata exposure kubwa, tunaomba mawazo yenu, Tanzania iwasaidieje ili muweze kuisaidia nchi yako Tanzania.

Natanguliza Shukrani.

Pascal Mayalla
+255 784 270403
pascomayalla@gmail.com
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom