Diamond anapita njia za Rehema Chalamila, alikuwa anakula advance na hatokei kwenye show na matokeo yake show zilipokata akaanza kujifariji kwa kuwa teja. Simsahau Ray C alinitia hasara Norway, alikuwa advance na nikamtumia ticket za mbili za ndege na hakutokea.
Bila kujali ni tatizo la promota au Diamond, jambo lililokuwa la muhimu ni Diamond kuhakikisha kuwa yaliyomtokea Germany hayamtokei tena katika maisha yake ya muziki ili kuonesha alivyo makini kwenye kazi yake, lakini ndani ya kipindi kifupi inatokea tena, na unatolewa utetezi ule ule.
Diamond muziki ndio kazi yake, muziki ndio biashara yake, hivyo anapaswa kuilinda na kuhakikisha mtu hachezei biashara yake kwa kumchafulia sifa kwa tabia ya kutotokea kwenye maonesho. Ni sifa mbaya sana, ambayo mwenzake Ray C inamgharimu mpaka leo.
Ova