Mkumbuke, sasa, Muumba wako Mkuu katika siku za ujana wako, kabla siku zenye msiba hazijaja, au miaka iwe imefika wakati utasema: "Sipendezwi nayo"; [SUP]2[/SUP]kabla jua na nuru na mwezi na nyota havijawa na giza, na mawingu yamerudi, kisha mvua kubwa; [SUP]3[/SUP]katika siku ambayo watunzaji wa nyumba wanatetemeka, nao wanaume wenye nguvu wameinama, na wanawake wanaosaga wameacha kufanya kazi kwa sababu wamekuwa wachache, na mabibi wanaochungulia madirishani wameona giza; [SUP]4[/SUP]na milango inayoelekea barabarani imefungwa, wakati sauti ya jiwe la kusaga inaposhuka,+ naye mtu huamshwa na sauti ya ndege, na mabinti wote wa wimbo hutoa sauti ya chini.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.