Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 278,618
- 1,128,582
Diamond Platnumz anatarajia kuhudhuria mazishi ya Ivan Semwanga, mume wa zamani wa Zari Hassan, aliyezaa naye watoto watatu wa kiume. Diamond amesema mpenzi wake huyo ambaye wana watoto wawili, yupo kwenye wakati mgumu kufuatia msiba huo. “Kwakweli ilikuwa ni wakati mgumu na hata sasa ni wakati mgumu kwasababu nilikuwa nipo booked muda kidogo kuhusiana na Koroga Festival na msiba umetokea sasa kucancel tu ghafla show ya watu unajua inawezekana ukapata taswira tofauti, wengine wakachukulia tofauti, sikuwa na jinsi,” alisema Diamond kwenye mahojiano na kipindi cha The Trend cha NTV Kenya Ijumaa hii. “Lakini niliongea na mzazi mwenzangu akanielewa, nikimaliza hapa show tu ntaenda Uganda sababu ya mazishi kuzika baada ya hapo ndio ntarudi nyumbani,” aliongeza
MSIBANI