Diamond Platnumz aeleza bifu yake na Ali Kiba ilivyosukwa ‘kumuua Kimuziki’

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
12,321
11,315
images-1.jpg

Diamond Platinumz amedai kuwa uhasama kati yake na Ali Kiba ulipikwa na chombo kimoja cha habari kwa lengo la kumuondoa kwenye ramani ya muziki.

Bosi huyo wa WCB amefunguka katika mahojiano na Lil Ommy wa Times FM, ambapo amedai kuwa uhasama huo ulikuwa miongoni mwa mbinu za muda mrefu zilizoshindwa za kutaka kumuua kimuziki.

Amesema kuwa baada ya kugundua mbinu hiyo, alikutana na Ali Kiba jijini Nairobi na akazungumza naye kuhusu hilo na wakakubaliana hakuna tofauti kati yao.

Diamond ambaye anapromoti albam yake mpya ya ‘A Boy From Tandale’ alisema kuwa tofauti kati yake na Ali Kiba haiko kiuhalisia kwani inatengenezwa na watu wasiomtakia mema na kukuzwa na mashabiki.

Aliongeza kuwa njama na jitihada za kutaka kumuangusha kimuziki zilianza miaka minne iliyopita lakini haziwezi kufanikiwa. Alisisitiza kuwa hakuna anayeweza kumuua kimuziki akiwa hai, “labda unitoe uhai, lakini kuniua kimuziki haiwezekani.”

Lil Ommy alitaka kujua kama nyimbo za Ali Kiba zitachezwa kwenye vituo vya Wasafi Radio na Wasafi TV.

“Bro nisikudanganye, pale atachezwa kila msanii na yeyote mwenye talent (kipaji). Hadi sasa pale watu wanabishana kuhusu slogan (kauli mbiu), kuna wanaosema ‘Welcome Home’ na ‘Hii ni Yetu Sote’. Kwa hiyo hii ni ya wasanii na haipo kwasababu ya matabaka,” alijibu.

Chibu alisema kuwa ushikirikiano wa wasanii ndio utakaoendelea kuukuza muziki wa Bongo Fleva na sio uhasama na ushindani usiokuwa na lengo zuri.


Chanzo: Mpekuzi

PIGA KAZI KIJANA WALA USIOGOPE

 
Hayo mengine sawa lakini hiyo kusema hawezi kushuka kimuziki anajidanganya,ni swala la muda tu kwani huko nyuma kuna wasanii mbalimbali hata bendi zilikuwa juu kiasi cha kufikiria hivyo lakini hivi leo wamepotea kabisa katika ramani ya muziki na hata hawajulikani walipo.



Lazima ukubali kijana ana umiza akili mnooo,Pili hajasema hatoshuka kasema WANAOTAKA KUMSHUSHA KIMUZIKI,NDO WATASHINDWA

Msibadilishe maneno banaa
 
Nanukuu "Aliongeza kuwa njama na jitihada za kutaka kumuangusha kimuziki zilianza miaka minne iliyopita lakini haziwezi kufanikiwa. Alisisitiza kuwa hakuna anayeweza kumuua kimuziki akiwa hai, “labda unitoe uhai, lakini kuniua kimuziki haiwezekani.”
Kwa HIYO hapo hukuelewa nn sasa??

Kasema hatoshuka ama anayetaka kumshusha??


BRN mtawajua tu
 
Nanukuu "Aliongeza kuwa njama na jitihada za kutaka kumuangusha kimuziki zilianza miaka minne iliyopita lakini haziwezi kufanikiwa. Alisisitiza kuwa hakuna anayeweza kumuua kimuziki akiwa hai, “labda unitoe uhai, lakini kuniua kimuziki haiwezekani.”
Sasa ina maana hujaiona hiyo tofauti?!

Kuna KUSHUKA kimuziki na KUSHUSHWA... kushushwa kwa staili ya fitina huku mdau wa kushuka kwako akiwa KAA!!

KUSHUKA kimuziki ni natural death, inayoweza kusababishwa na uzembe wako mwenyewe au wakati wako tu kuwa umefika kama ilivyo kwa wengi!
 
Mond ndio kila mara anaonekana anakuza bifu kati yao mara maneno ya vijembe kwenye mitandao mara kwenye nyimbo alizoshirikishwa anapiga vijembe. Halafu akihojiwa anasema hataki bifu.
anatafuta pa kushika, mana kashatelezaa.
leo siku ya tano nyimbo haijafikisha 2M viewers? tena collabo na msanii waarekani??

Kweli Clouds nawapa salute
 
anatafuta pa kushika, mana kashatelezaa.
leo siku ya tano nyimbo haijafikisha 2M viewers? tena collabo na msanii waarekani??

Kweli Clouds nawapa salute
kwani clouds ndo wanasaidia wasanii kupata viewers wengi?.imeandikwa wapi na tokea lini
ikiwahi kufikisha mnasema amenunua viewers ikichelewa mnasema kafulia hahahaha halafu mnawataja clouds kwamba wao ndo wana control viewers you tube...
 
Back
Top Bottom