Diamond/Olympio Pr. Schools | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Diamond/Olympio Pr. Schools

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Suzzie, Nov 19, 2009.

 1. Suzzie

  Suzzie Member

  #1
  Nov 19, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 98
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  wapendwa nahitaji kupata nafasi ya mtoto wangu katika shule za msingi za Diamond au Olympio. Tatizo kila ninaemgusa anataka pesa nyingi ili anifanyie mpango. kama kuna mtu anaeweza kunisaidia tafadhali sana naomba msaada wenu.
   
 2. Enny

  Enny JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Wanataka kiasi gani mbona hizo ni shule za serikali tu kama zingine?
   
 3. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Hiyo shule ya olympio bila kuhonga mwalimu pale, wala hawamchukui mwanao. Mtoto wako anaweza kuwa na akili na kupass vizuri ile mitihani ya awali ili uchaguliwe kuanza shule pale, lakini bila kupitisha chochote mtoto hachukuliwi. Naifahamu vizuri hii shule.
   
 4. Liz Senior

  Liz Senior JF-Expert Member

  #4
  Nov 19, 2009
  Joined: Apr 19, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Suzzie, mwaka 2002 nilikutana na hilo tatizo...mpaka leo lipo! Sitaki kukuvunja moyo ila tu baada ya purukushani nyingi na kuminywa kifedha kila upande nilipata hiyo nafasi...miaka miwili baadae ilinibidi kumhamisha kijana shule ile kwani bado nilijikuta namlipa kama si mwalimu mmoja ni wawili ili kuhakikisha mtoto anafuatiliwa darasani na kupewa home work na mara nyingine hata daftari zake kupitiwa na mwalimu. Ni miaka kadhaa sasa imepita lakini kabla hujajitosa hebu chunguza zaidi hali ikoje shule hapo. Si vyote vingaavyo ni dhahabu
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Nov 19, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hii shule iko City Centre as it is, na ndo mambo ya kishenzi hayo yanafanyika, na serikali ndo ipo huko kwenu darisalam! Sasa huku mkoani itakuwaje! Mlengesheni mwalimu mmoja mwenye tabia hiyo hela za moto, akashikishwe ukuta huko Segerea!...This is too much!
   
 6. Suzzie

  Suzzie Member

  #6
  Nov 19, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 98
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Yaani kwa kweli imekuwa kero kubwa sana, mwalimu wa kwanza alitaka 200,000 nikamuomba japo anipunguzie akakataa na kuniambia katafute ukiwa tayari njoo.
  Wa pili akapanda dau na kutaka 250,000 nikauliza kulikoni mbona pesa nyingi kiasi hicho akadai anakula na wenzie hivyo bila kiasi hicho haiwezekani.
   
 7. Suzzie

  Suzzie Member

  #7
  Nov 19, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 98
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Sasa nashindwa kuelewa kama kuna interview na mtoto anafaulu inakuaje tena mambo hayo? ina maana serikali haijui jambo hili? Ada laki moja rushwa laki mbili na nusu!!!
   
 8. Suzzie

  Suzzie Member

  #8
  Nov 19, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 98
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Enny hizo shule ni za serikali but ni English medium
   
 9. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #9
  Nov 19, 2009
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,476
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  TAKUKURU ipo na inafanya kazi, jaribu kupeleka tatizo lako huko, huenda ukasaidiwa.
   
 10. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #10
  Nov 19, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Agree.
  halafu kwani kuna ulazima wa kumpeleka mwanao huko? mbona shule kibao sku hiz za maana. tusiogope gharama jamani, kama unaweza kunywa mil3 baa kwa mwaka, ukimlipia ada mil1 mwanao kuna ubaya gani?
   
 11. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #11
  Nov 19, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mi wanangu wamesoma Mapambano toka std 1 to 7, then Kibaha sec na Tambaza mwingine alijikogoja pale makongo lakini leo hii wote wako Mlimani wawili wanasoma Bcom na mmoja anamalizia Medicine Muhimbili.

  Mi naamini shule yoyote mwanao anaweza kusoma na kufanya vizuri, unachohitaji kama mzazi/mlezi ni ufuatiliaji wa kuribu na kuwajengea tamaa ya kuwa wanataaluma bila kusahau kuwa role model. Kama wewe mwenyewe mzazi hujawahi kujisomea hata kanovel ka page 12, mtoto wako ataanzaje kusoma kitabu cha Kotler chenye pg 800???

  Wazazi na walezi tukijenga mazingira ya kukaa nyumbani na kujisomea, watoto wetu watafuata nyendo zetu!! Tukikaa bar basi tutegemee watoto wetu wote kuwa wanamuziki wa bongo flavour tu!!

  Tusiwaachie hili jukumu waalimu peke yao!!
   
 12. Enny

  Enny JF-Expert Member

  #12
  Nov 19, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Suzzie ndugu yangu jaribu kufuatilia vizuri. Zamani zilikuwa hivyo lakini sasa hamna kitu watoto wanaongea kiswahili kwenda mbele wameweka kibao tu nje SPEAK ENGLISH.
  Hazina tofauti na Upanga primary school au Bunge Primary school
   
Loading...