Diamond - Mdogomdogo (Video na Lyrics)

uwezo wake ndo ulipofikia mkuu, wabongo tunapenda sana ku blame kutokana na views zetu zisizo na vichwa wala miguu

mimi kwenye gari au nyumbani naweza kusikiliza nyimbo ya diamond kesho nikupeleke nyumbani, sijui jina halisi la wimbo huu na pia my number one unaleta mizuka lakini siyo huu ushuzi alioutowa wa wacheza vigodoro na kwenye harusi za wazaramo.

kama idea yake ni kwamba amekubali davido aendelee kuzoa tuzo zote na yeye ajikite kwenye soko la waswahili na mabeki tatu mimi sina tatizo ni ubunifu wa hali ya juu maana bongo movie na magazeti ya shigongo wateja wao wakubwa ni group hilo la simple minded. nadhani diamond ameiona fursa hii hongera zake.
 
Diamond itakuwa mganga wake ana nguvu sana aiseeee
 

wewe hujui muziki wala hujui unachokiongea, sikiliza nyimbo ya fally ipupa na j Martins mimi sielewi hata wanachoimba lakini ngoma ikipigwa club lazima niselebuke vya kutosha, u know why? wao wanajuwa nini mashabiki wanataka cha kwanza ni beat.

diamond kwa miaka yote beat zake ndio zimekuwa zikimbeba tungetaka waimbaji bora yeye hata kwenye top 3 three hayumo. take it or leave it.
 

Umenifurahisha kweli.sasa umesema daimond beat ndo znambeba!!!!cjui unajua hapo tunaongelea nini au umekurupuka tu..hebu chungulia mwanzo uone huyo dada aliuliza nini na nikamjibuje!!!yaan cjaelewa mantic ya mchango wako zaodi nakuona kama unakijaruba flan na daimond adi unamponda yeye anaesema beat znambeba na kumsifia ipupa ambaye unakili huelewagi anaimba.nini bt unapenda beat tu!!!!
 
Kingereza cha kinigeria ama kweli huyu domo kuna watu wanamvimbisha kichwa hajui ndio wanamppteza Yani Audio mbovu sijawahi Ona, kila kitu humo ndani ni unigeria mtupu
 

Mkuu huo ni ushauri mzuri,niliona show yake moja sikutaka tena niangalie show yake yoyote.Kwa sasa aache playback ajikite kwenye liveband na ataweza maana jamaa ana bidii sana.
 
Mkuu huo ni ushauri mzuri,niliona show yake moja sikutaka tena niangalie show yake yoyote.Kwa sasa aache playback ajikite kwenye liveband na ataweza maana jamaa ana bidii sana.

wewe unamtakia mema diamond na siyo hawa vitimbakwiri kazi kusifia ujinga tu.
 

Unadhan level alzofkia huyu ni za kushutia hko unakotaka ww? Labda co kaka ndomo naemjua mm
 
Hata nyimbo za AfroNiger tunazozipenda huku mtaani kama sekereu etc hata Hiphop ni street customs za USA - ngoma za kimtaani zaidi(battling Hiphop) so msishangae kupiga mchiriku style (ngoma imekaa poa sana)
Acheni wivu wa kijinga haters

Well said
 
Diamond awa mtanzania wa kwanza toka Tandale, kufyatua video 2 gharama ikiwa ni milioni 120.
 

Kwako hapana kwasababu ina tune ya kizaramo? subiri wengine wataimba tune kikwenu na wewe utafurahi.
 
music wa asili wenyewe ni tatu nane, inafrica band, che mundugwao, kharid tongolanga na saida kaloli. wacha kujitowa ufahamu.

wejamaa huwezi kuendelea kama unatabia kama hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…