Anselm
JF-Expert Member
- Nov 16, 2010
- 1,710
- 291
Wadau nilikuwa nikitokea kwenye harakati zangu binafsi nikirejea kwangu,muda niliokuwa napita Mbagala maeneo ya Dar Live ni muda ambao Helicopter iliyokuwa imemchukua Super Star wenu Diamond ilikuwa ikirandaranda hewani,nikiwa bado nasota kwenye foleni Super Star wenu akashushwa dizaini akaingizwa kwenye Benz nyeusi ikisindikizwa na Deffender 2 za Polisi,1 mbele ikimsafishia njia kwa king'ora,katikati BENZ iliyombeba yeye na nyuma Deffender nyingine ile inayobebaga Polisi wale wa kusimama huku Polisi wengine kibao wakiwa njiani mpk nikashawishika kuamini pengine "Baba Mwanaasha" labda alikuwa akijiandaa kupita,kumbe Diamond....sasa hebu mnisaidie kunielewesha hivi ni sahihi kwa Jeshi letu kutumia resources zake kwaajili ya issue za "Nimpende nani" kweli?
Nawasilisha.
Nawasilisha.