Diamond azindua Pafyum yake ya Chibu, bei yake ni balaa

Safi nimeipenda hii tena angefanya hata laki 3 kabisa

Nasema hivi kwa sababu ingekuwa ya bei ya chini kila mtu angenunua matokeo yake watu mkitembea mnakuwa mnanukia harufu moja kila mtu kitu ambacho sikipendi

Bora allivyofanya hivyo,wale watanashati tunaojua kutupia tutanunua tu ila wale wazee wakuunga unga waendelee ni spray zao za buku 5 tano
Teh teh
 
Mkuu labda ungeshauri atoe bidhaa kwa watu wote wachini wawe na bidhaa zao za chini na wajuu tuwe na bidhaa zetu za juu (Hahahahah), sema soko la watu wa chini lina masimango sana, usiombe masikini atoe buku afu asiridhike na hiyo bidhaa,
 
Utajiskiaje siku upo mbele ya kadamnasi halafu unakuta watu kama 20 mnanukia harufu moja?
Tatizo lenu ni kwamba hata kama ninyi ndiye washauri wa huyo bwana basi mtazidi kila siku kumshauri vitu ambavyo sana sana vitamchelewesha kufika akutakako..

Subiri nikupe mfano mdogo tu ambao hata yeye kama atasoma hapa naamini atauzingatia.. Diamond nasikia ana zaidi ya mashabiki Million 2 kwenye mitandao. Kati ya hao almost 90% ni vijana below 30 yrs na kati ya hao 90% ambao ni vijana karibia 70% yao ni wanafunzi na vijana wasio na uwezo/kipato cha kueleweka.. Kwahiyo tunaweza sema 80% ya mashabiki wake sio watu wenye vipato vya kueleweka.. Sasa hauwezi ku ignore 80% ya mashabiki wako udili na 20% ambao pia huna hakika kama watapenda kile unachokiweka mezani kwa sababu mbalimbali, either bei au prestige ya hao mashabiki (unafahamu matajiri wetu wanavyohusudu vya nje).

Sasa tuanze kudili na hao 90% ambao ni almost 1.8 Million ambao kila siku wako kwenye mizunguko either ya kishule au kutafuta maisha. Ukiweka kinywaji ambacho utauza kwa shilling 500 tu na kila siku kati ya mashabiki wako hao 1.8M, asilimia 10 pekee ndio wakanunua (hizi ni estimation za chini kabisa pia tumeignore ambao sio mashabiki na wale ambao hawako kwenye mitandao) kwahiyo angalau kwa siku akawa anauza bottles 180,000 kwa hao watu 180,000 kwa shilling 500/- ina maana kwa siku atatengeneza kiasi cha shilling 90,000,000/-.. Hiyo Turnover ya million 90 kwa siku kwa profit margin ya 10% (mostly common to many fast moving products) itamletea faida ya 9,000,000/- kila siku.. Yaani kila mwezi anakuwa na uhakika wa faida ya Million 270.

Hizo perfume hao 20% wakinunua wanaweza kutumia hata mwaka mzima.. Yaani mtu anapulizia akiwa ana special event/occasion ya kuattend na si kupulizia kila siku akiwa kwenye mizunguko ya kawaida.. Unaweza kuta kwa mwaka faida ya hizo perfumes pamoja na bei kuwa kubwa wala isizidi Million 100 wakati akiweka cheap product ambayo kila shabiki ataafford kama mfano wangu hapo juu anatengeneza Million 270 kwa mwezi mmoja tu..
 
Safi nimeipenda hii tena angefanya hata laki 3 kabisa

Nasema hivi kwa sababu ingekuwa ya bei ya chini kila mtu angenunua matokeo yake watu mkitembea mnakuwa mnanukia harufu moja kila mtu kitu ambacho sikipendi

Bora allivyofanya hivyo,wale watanashati tunaojua kutupia tutanunua tu ila wale wazee wakuunga unga waendelee ni spray zao za buku 5 tano
Well said na kama mtu ni mtumiaji mzuri wa perfume 100k ni very reasonable.

Wanaoweza watanunua.
 
Hii pafum ni nzuri sana nimenunua Leo inarufu nzuri Na inaonekana inakaa mwilini vizuri haimsumbui hats yule aliekaa jirani yako kama ile kursumu ya kariakoo
 
Nilikuwa napata elimu kidogo ya kibiashara sehemu, na jambo kubwa lilikuwa namna ambayo Diamond kaja nayo juu ya Perfume yake, nimemfikiria Diamond kwa sababu ni staa kama wanavyoweza kuwa mastaa wa michezo pia wakaanzisha biashara zao.

Swali kubwa lilikuwa bei lakini pia Chapa (brand) aliyoingia nayo sokoni.

1. Bei ya Perfume ya Diamond ni 105000, yaani laki moja na elfu tano. Hii ina maana kuwa wenye uwezo wa kununua hii ni kwa kiasi kikubwa nusu ya wale walioweza kulipa Elfu Hamsini kuingia kwenye show yake Mlimani City. Nasema hivi kwa sababu kwa bei hii kuna brand kubwa Ulaya zenye bei jirani na hiyo ambazo watu wataendelea kuzinunua.

2. Washabiki Wengi wa Diamond ni watanzania. Kipato cha siku cha Mtanzania wa kawaida ninaambiwa hakizidi elfu 70 kwa siku kama tukiamua kukadiria juu sana, lakini wengi wanaishi chini ya Dola 5, yaani elfu 12 hivi. Hii ni changamoto.

3. Biashara ya msanii au staa yoyote ni nadra kuhusishanishwa na kazi yake. Kwa mfano Rihanna viatu vya Fenty vipo chinii ya kampuni kubwa za Puma, sio kwamba hawezi kuanzisha kampuni yake. Air Jordan zipo chini ya Nike, sio kwa sababu hakuweza kuanzisha kampuni, Ronaldo na Pestana Hotels aliingia ubia na wafanyabiashara wakubwa. Msingi wa hili ni kuondoa fikra za watu wanaonuua kuendana na mziki au kipaji chako, ili siku ukishuka ubaki katika soko.

Mikataba ya ushirikiano hii uweka mlinganyo wa kudumu zaidi. Hapa Diamond angeweza kuja chini ya nembo ya kampuni yoyote kubwa, na Fragrance zake zikaitwa hata Armani Chibu, na hii ingefanya Giorigio Arman wafungue kampuni yake nchini.

4. Lakini pia huwa namkubali Diamond kwenye promotion. Sidhani katika hii chibu kama alifanya maandalizi sahihi. Ile amusement na excitement (kufurahia na kuitamani) bidhaa hajaiweka kipindi hiki. Hata yeye mwenyewe hajaonekana katika promo hata kujaribu kuonyesha ina harufu gani, inafaa chumbani kwa namna gani, mtu atafeel vipi akiwa nayo ofisini na mambo mengine ambayo yangevuta wateja wake.

5. Mwisho, bado naamini Diamond ni mpiganaji, kijana wa kipekee na ambaye anajaribu kuleta utofauti wa kufikiri katika kila jambo na kuweka misingi ya fikra za ujasiriamali. Lakini nahisi hili hapa lilichangiwa kwa kiasi kikubwa kuamini katika jina lake kabla ya kufanya utafiti wa walaji wake. Hii ingeambatana na Deodorant na Spray ambazo zingekuwa bei rahisi, angewachota wa Masaki na kwa bibi yangu Magu pale Mwanza.

Mwisho wa siku, bado anahitaji kupongezwa, ni uthubutu wa kipekee huu. Akili yake nimeshindwa kuifananisha na staa yoyote wa Tanzania kwa sasa, katika sekta zote. Hawapo jirani yake, lakini alipoelekea sasa, Menejimenti yake inatakiwa kuwa makini. Uwekezaji huu sio wa muziki sasa, misingi ya uchumi, biashara izingatiwe. Sio kipaji tu huku, ni mahesabu kwelikweli.

Ni mimi mpendasoka Nicasius Agwanda (Coutinho). Nimeandika baada ya kupewa elimu pia.

COPY AND PASTE
 
Attachments

  • 18014070_233247517153242_1649901035239505920_n.jpg
    18014070_233247517153242_1649901035239505920_n.jpg
    84.2 KB · Views: 38
Tatizo lenu ni kwamba hata kama ninyi ndiye washauri wa huyo bwana basi mtazidi kila siku kumshauri vitu ambavyo sana sana vitamchelewesha kufika akutakako..

Subiri nikupe mfano mdogo tu ambao hata yeye kama atasoma hapa naamini atauzingatia.. Diamond nasikia ana zaidi ya mashabiki Million 2 kwenye mitandao. Kati ya hao almost 90% ni vijana below 30 yrs na kati ya hao 90% ambao ni vijana karibia 70% yao ni wanafunzi na vijana wasio na uwezo/kipato cha kueleweka.. Kwahiyo tunaweza sema 80% ya mashabiki wake sio watu wenye vipato vya kueleweka.. Sasa hauwezi ku ignore 80% ya mashabiki wako udili na 20% ambao pia huna hakika kama watapenda kile unachokiweka mezani kwa sababu mbalimbali, either bei au prestige ya hao mashabiki (unafahamu matajiri wetu wanavyohusudu vya nje).

Sasa tuanze kudili na hao 90% ambao ni almost 1.8 Million ambao kila siku wako kwenye mizunguko either ya kishule au kutafuta maisha. Ukiweka kinywaji ambacho utauza kwa shilling 500 tu na kila siku kati ya mashabiki wako hao 1.8M, asilimia 10 pekee ndio wakanunua (hizi ni estimation za chini kabisa pia tumeignore ambao sio mashabiki na wale ambao hawako kwenye mitandao) kwahiyo angalau kwa siku akawa anauza bottles 180,000 kwa hao watu 180,000 kwa shilling 500/- ina maana kwa siku atatengeneza kiasi cha shilling 90,000,000/-.. Hiyo Turnover ya million 90 kwa siku kwa profit margin ya 10% (mostly common to many fast moving products) itamletea faida ya 9,000,000/- kila siku.. Yaani kila mwezi anakuwa na uhakika wa faida ya Million 270.

Hizo perfume hao 20% wakinunua wanaweza kutumia hata mwaka mzima.. Yaani mtu anapulizia akiwa ana special event/occasion ya kuattend na si kupulizia kila siku akiwa kwenye mizunguko ya kawaida.. Unaweza kuta kwa mwaka faida ya hizo perfumes pamoja na bei kuwa kubwa wala isizidi Million 100 wakati akiweka cheap product ambayo kila shabiki ataafford kama mfano wangu hapo juu anatengeneza Million 270 kwa mwezi mmoja tu..
Diamond hata alipokuwa anafanya tamasha la diamond are forever pale M-City kwa mara ya kwanza kwa kiingilio kikubwa watu walimbeza na kudai kuwa hatopata watu wengi lakini matarajio ya wengi yakawa tofauti kwani jamaa alijaza sana ingawaje kiingilio kilikuwa ni kikubwa sana

Hivyo basi hata hiyo perfume hata iuzwe kwa milioni lakini kama ina quality nzuri itanunuliwa tu kama njugu
 
Hiyo ni bei kwa chupa. Mashabiki wake mpaka leo wananunua perfume kwa mpulizo. Kama mpulizo mmoja 500, ukitaka 4 unalipa 2000
Hahaaaaa gud night usiku umekua mwema c kwa mpulizo huu itasubiri sana dukani
 
BEI yake ni 150:000/=

1..Sukari hapa kwetu na kwake Tandale BEI kwa kilo... 2600

2.. Unga wa kupikia ugali ( Dona na sembe) kilo moja ni 2000
Dagaa za Mia Nne na hamsini

3...nyanya mbili kila moja BEI yake ni shilling Mia mbili yaaani nyanya mbili ni shilling Mia 400

4.. kitunguu kimoja ni shilling Mia na hamsini ambayo jumla yake ni shilling Mia tatu

5... mboga za majan kupunguza muwasho wa dagaa za mwanza fungu Mia mbili

6... mafuta ya taa kwa Ajili ya jiko langu la mchina kuweza kupata mlo safi kwa siku ni shilling Mia sita

***** Naseeb Domo umetusahau brother
 
Hivi ile clothing line yake aliyoanzisha ya WCB inafanyaje sokoni?

Kama ile ameshindwa hivi kweli perfume nani atanunua kwa hiyo bei? Exposure yote aliyonayo pamoja na kwenda ulaya kila siku bado hajui apart from mziki nini kitampatia pesa matokeo yake yeye kila siku kujaribu jaribu tu mambo.. Mara App sijui ya kuuza mziki, huko hajafanikiwa karukia perfume..

Diamond una jina kubwa sana, clothing line sijui maperfume havijawahi kumtoa msanii yeyote mkubwa hata huko duniani. Tafuta biashara ambayo inagusa matumizi ya watu ya siku kwa siku.. Angalia biashara wanazofanya akina Mo na Bakhressa.. Ushauri tu ebu jaribu hata kutengeneza kinywaji chako, iwe Juice au Soda kama za Azam au Mo hapo utatoboa mara moja maana mashabiki wako wengi ni wanafunzi na watoto wa uswazi ambao hawana kipato kikubwa ukilinganisha na hizo bei unazoweka kwenye bidhaa zako.. Na hata biashara ya Juice mteja mmoja anaweza akawa anakunywa Juice yako angalau mara tatu kwa wiki lakini hizo Perfume na nguo anaweza purchase once in a lifetime.. Akina Pdidy na 50 Cent wao wanatajirikia kwenye liquor sasa wewe si mnywaji basi fanya hata Juice hizo au hata Non-Alcoholic drinks..

Demu wako Wema alikuja na biashara gani sijui lakini pamoja na mvuto wake kwa mashabiki wake alifeli, kuwa tofauti usifate mkumbo na usifanye biashara za sifa (kwamba perfume yangu inauzwa ghali).. Hujafikia level za kutengeneza prestigious products maana mashabiki wako ni watu wa hali ya chini..
Bonge la ushauri, yan huu anatakiwa aulipie
 
Back
Top Bottom