Diamond awashukuru Membe na timu yake! Nini kinaendelea?

Diamond awashukuru Membe na timu yake! Nini kinaendelea?

"Eeh Mwenyez Mungu Nakushkuru sana kwa kuweza kunipa ujasili na Moyo wa kuyavumilia yote niliyo yapitia.

Asante sana Mh. Benard Membe, Joseph Kusaga, Haroun na Kampuni Nzima ya Spice, Mh Nchimbi, Dk Dossaj , Uongozi wangu, jamaa na Marafiki, Mashabiki zangu pamoja na Familia yangu pendwa kwa kuwa nami bega kwa bega katika kipindi chote cha Miezi hii Miwili Migumu kwangu.Nawashkuru sana''

Ameandika hayo kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Watanzania wanachojiuliza mbona hii team Membe aliyoitaja ipo karibu sana na huyu dogo?

Diamond hana impact kwenye siasa za CCM.... Anashukuru dili la kupewa kufungua hoteli ya Naf iliyojengwa kwa fedha za Ghadafi
 
i think membe ni mtu safi na ana integrity ukiacha chama chake naamini ivo.

Fedha za Ghadafi, za Comoro, za Congo..... Ukiza kuhusu padre Komba, uliza kuhusu Balozi wa Libya...... Ukishapata majibu urudi tujadili kwa pamoja..
 
Pengine dogo alipata wasaha mzuri wa kumvushia powder mamtoni nn,all in all inawezekan
 
Ndio pengine walikuwa nae kwenye matatizo...Lakini kwa nini iwe team Membe pekee?

Nadhani ukisoma vizuri alimaanisha timu yake yeye--yaani ile inayoitwa WASAFI au WCB. Anaishukuru hiyo timu yake kwa kumsaidia au kumfariji wakati akiuguliwa na mamake. Na Membe nadhani anamshukuru labda amemsaidia katika masuala ya kupata viza ya India! Sina hakika anyway. But kama jamaa alivyosema ni jambo jema kuwashukuru watu wakikusaidia katika matatizo. Bwana mdogo ni muungwana tu.
 
Fedha za Ghadafi, za Comoro, za Congo..... Ukiza kuhusu padre Komba, uliza kuhusu Balozi wa Libya...... Ukishapata majibu urudi tujadili kwa pamoja..
hizo story nazisikia tu juu kwa juu sasa sijui kwa undani wake ebu tupe ukwel acha porojo vinginevyo ni unafiki lete evidence ww unaejua mm naangalia utendendaji wake kwa wananchi moja kwa moja sioni kama uonavyo ww
 
ila kale kamaembe kanafiki sana.kanajiona kasafi wakati ni kachafu kama choo.
 
Membe alifanikisha suala mama ake Diamond kwenda kutibiwa India hapo ndo anatoa shukran, hata mwaka juz Membe alishawahi kumchukua dogo na kwenda kupiga show uwanja wa Ilulu-Lindi.
 
Back
Top Bottom