Diallo: Rais ajaye awe dikteta mzalendo

Diallo: Rais ajaye awe dikteta mzalendo

Slaa ni mzee sana. Ikulu sio kituo cha kulelea wazee
 
Mkuu usikusumbuke kichwa na Barongo,muulize kama alishawahi kemea uchafu wa mabwana zake wa CCM

Akemee uchafu wa chama chake aka le wapi mkuu,kuna katabia cha ccm kananikera sana hiki cha unafiki,kwa kuwa wao sio wazalendo tena basi wanajua kila mtu yuko kama wao na sera za kunufaisha matumbo yao kila mtu ili mradi wasiingiliane,tumeshtuka
 
Kwanza uadlifu upi unaozungumzia nijuavyo mzee slaa hana uadilifu wowote zaidi ya kuiba mke wa mtu,kuiba pesa za kanisa,kufukuzwa kanisani na kupanga mipango kwamba nchi isitawalike.
 
Slaa ni mzee sana. Ikulu sio kituo cha kulelea wazee
Naunga mkono hoja slaa angebaki na wajukuu wa mzee mtei nyumbani awalee na kucheza nao mda wa kulea wazee ikulu haupo siyo kituo cha wazee.
 
Mmeshaambiwa mbona Mkapa alipora mke wa Mramba na hamkusema chochote?!
 
Naunga mkono hoja slaa angebaki na wajukuu wa mzee mtei nyumbani awalee na kucheza nao mda wa kulea wazee ikulu haupo siyo kituo cha wazee.

Edward Lowassa 81 11.27%
Dr. Willibrod Slaa 596 82.89%
Wote hawafai/sijaamua 42
5.84%
Voters: 719. This poll is closed
 
Full stop

Ili na sisi wananchi tufocus kwenye kazi.

Kiongozi aina ya kikwete bila kumfuatilia mnauzwa wote.
Mkuu wewe ndiyo kiazi kabisa hakuna kiongozi mwenye uzalendo na taifa lake kama jk hii ni pamoja na kuwa thabiti kwenye mipango ya maendeleo.
 
Edward Lowassa 81 11.27%
Dr. Willibrod Slaa 596 82.89%
Wote hawafai/sijaamua 42
5.84%
Voters: 719. This poll is closed
Kwahilo sinaubishi na wewe slaa na Lowasa wote magarasa tu hawafai kuongoza watanzania.
 
Kwa sasa taifa letu linahitaji mabadiliko ya kitaasisi na uongozi. Mabadiliko hayo hayawezi kupatikana kwa kubadilisha mtu badala ya chama. Hata kama tutafanya mabadiliko kwa kuweka mtu mwingine bila kubadilisha chama ni kazi bure. Tatizo la taifa letu ni la kimfumo na sio la mtu binafsi.

Ukawa bado sana labda sana sana 2025,kundi lina viongozi wa ajabu sana mfano tundu lissu kwa kutambua aina ya watu wake jimboni anawatetea wadichangie chochote kile kuanzia elimu nk,ujinga uliopo huko inasikitisha lakini cha ajabu yeye na ndugu zake wana soma na kutokana na hilo wanampenda bila kufahamu wanaangamia wao na kizazi chao yaani inasikitisha sana
 
Kwa hali ya sasa ya nchi yetu....kila kitengo kujiendesha kiholela ili tu kuwahadaa wananchi.....wizara na mawaziri kuendesha wizara pasi na ujuzi wa wanayoyafanya, wananchi kupewa elimu ambayo inawafanya hata kushindwa KUSOMA kwa MIAKA SABA (si maajabu ya dunia haya). Yaani unafundishwa kusoma kwa miaka saba NA UNASHINDWA kusoma hata jina lako. Na mtoto huyo anafaulu kuendelea na ngazi ya juu.
Kila siku mifumo ya sekta mbali inabadilishwa ili tu kuuhadaa umma kwamba MAMBO NI MAZURI MNO!!

Jamani muujiza gani huu wa kuimarisha elimu kutoka 90%FAILURE mpaka 60%PASSES.

MAAJABU.

Hebu tushauriane hapa JE KUNA HAJA YA KUANGALIA SIFA YA ZIADA KWA RAISI AJAYE??
 
namnukuu bwana kova nilisoma gazeti 1 akisema rais ajae anatakiwa awe dikteta, la sivyo tunakoelekea ni kubaya, nadhani yeye alimaanisha rais asiwachekee watu wake wa karibu, hata ikiwezekana awarestishe in peace, hapo nadhani wataogopa hawa watu, hawa huruma kabisa
 
mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (ccm) mkoa wa mwanza, dk antony diallo, amesema anatamani rais wa awamu tano awe dikteta, lakini anayepatikana kwa njia ya kura ili awatie adabu watanzania.

Dk diallo aliyasema hayo wakati akizungumza na watendaji wa ngazi za juu wa halmashauri ya jiji la mwanza, katika kikao alichokiitisha kwa ajili ya kubadilishana mawazo ya namna ya kuboresha shughuli za jiji la mwanza.

Mwenyekiti huyo wa ccm, alisema kuwa hivi sasa taifa linakabiliwa na tatizo la wananchi, hasa wanasiasa la kutotii sheria na kujiamulia mambo kiholela na hivyo kuleta hofu kwa wananchi.

“ninatamani sana rais ajaye wa awamu ya tano awe dikiteta, lakini ambaye atakuwa amechaguliwa kwa kura na wananchi, ili aje atutie adabu, kwani taifa liko katika hali mbaya, kila mmoja ni mjuaji na yote haya yamekuwa yakisababisha uvunjifu wa amani,” alisema dk diallo.

“watanzania ni waoga sana, wakisikia mlio wa bunduki wengi watakimbilia uvunguni mwa kitanda, tunataka rais ajaye awe dikteta ili ainyooshe nchi hii, kwani imefikia katika hali mbaya, kuna watu wanaichezea amani yetu na ni mabingwa wa kuhamasisha vurugu na wanazungumza mambo wasiyoyajua,” alisema dk. Diallo, ambaye pia amewahi kuwa naibu waziri na wizara katika serikali za awamu ya tatu na nne.

Mwenyekiti huyo pia alisema kuwa sheria za nchi pia zinapaswa zitazamwe upya katika kuilinda nchi hii kuepuka kupata viongozi wasiofaa na kuitaka idara ya usalama wa taifa kuhakikisha inaisaidia serikali katika kupata viongozi bora na wasio na kasoro.

Alisema kuna baadhi ya maeneo baadhi ya watu wamejipenyeza kugombea uongozi na kushinda, huku wakiwa si watu safi, hali ambayo inaiyumbisha nchi.

“kuna baadhi ya wabunge na madiwani ni x criminals, ni wahalifu sugu wamefanikiwa kushika nafasi hizo, hapa unatarajia nini na kuna kiongozi mmoja hivi sasa ni kiongozi wa chama cha siasa katika ngazi ya wilaya huyu siyo mtanzania, tatizo hapa katika siku za karibuni vyombo vyetu vimelegalega,” alisema dk diallo.

chanzo: mtanzania
steven masatu wasira, kiongozi msafi na mwenye ujasiri zaid tanzania WASIRA1.jpg
 
Back
Top Bottom