Diallo atamba kurudisha heshima ya CCM Mwanza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Diallo atamba kurudisha heshima ya CCM Mwanza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PROFESA KYANDO, Aug 24, 2012.

 1. PROFESA KYANDO

  PROFESA KYANDO Member

  #1
  Aug 24, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [h=2][/h] Ijumaa, Agosti 24, 2012 05:46 Na waandishi Wetu, Mikoani

  KINDUMBWENDUMBWE cha kuwania nafasi ya uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimezidi kushika kasi huku baadhi ya wagombea wakiweka wazi mikakati yao.

  Hata hivyo mchuano mkali ukitarajiwa kuwa kati ya Mwenyekiti wa sasa anayemaliza muda wake Clement Mabina na aliyekuwa Mbunge wa Ilemela (CCM), Antony Diallo.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kurejesha fomu ya kuwania nafasi ya Uenyekiti Mkoa wa Mwanza, Dk. Antony Diallo, alisema endapo atafanikiwa kuwa Mwenyekiti wa chama hicho atapiga marufuku matumizi ya magari ya chama kutumika kwa shughuli binafsi.

  Alisema hatua hiyo itakuwa ni njia ya kukipunguzia chama gharama za uendeshaji.

  Diallo, ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), anayemaliza muda wake alisema kuna baadhi ya viongozi wamekuwa wakitumia mali za chama yakiwemo magari kwa ajili ya shughuli binafsi badala ya magari hayo kutumika kukiimarisha chama.

  "Kama wewe ni Mwenyekiti gari hilo linapashwa kukuchukua siku ya vikao rasmi na shughuli rasmi, Mwenyekiti wa chama sio Mwenyekiti mtendaji gari la nini unataka ukae nalo na ulitumie kwa shughuli zako binafsi,huku ni kunibebesha chama mzigo wa gharama.

  “Chama kinahitaji mtu ambaye atakiongoza kama taasisi na sio kama mali yake binafsi,pia inahitajika mtu ambaye atawaunganisha wanachama na sio kuwagawa na mtu huyo ni mimi Dk Diallo,” alisema.

  Katika hatua nyingine Katibu wa ccm wilaya ya Nyamagana Deogratius Rutta amekwaa kisiki baada ya kuangushwa vibaya katika kuwnaia nafasi ya ujumbe wa mkutano mkuu wa ccm taifa kupitia nafasi tatu za wazazi.

  Katibu huyo aliibuka na kura 71 ambapo washindi watatu waliopatikana ni Samson Ntambi, Raphael Shilatu pamoja na Emanuel Nzungu.

  Dk. Kigwangalla: Uongozi siyo mvi

  Kwa upande wake mbunge wa Nzega mkoani Tabora, Dk. Hamisi Kigwangalla (CCM), amesema uongozi unahitaji uwezo na hekima ya mtu na siyo kigezo cha umri mkubwa.

  Dk. Kigwangalla ambaye amejitosa kuwania nafasi ya Uenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ALISEMA ana uwezo wa kuiongoza Jumuiya hiyo ambayo hivi sasa ina taswira ya watu ‘waliokula chumvi’.

  “Uongozi siyo mvi, bali ni jambo linalohitaji uwezo na hekima ya mtu bila kujali umri wake wa uzee au ujana,” alisisitiza Dk. Kigwangalla ambaye ni kijana mwenye umri wa miaka 37.

  Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya CCM Mkoa wa Mwanza, mara baada ya kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na CCM kugombea nafasi ya uenyekiti wa Jumuiya hiyo ngazi ya Taifa.

  Wakati hayo yakiendelea Watanzania wametakiwa kuelewa kuwa ufisadi haupo ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) peke yake bali hata katika vyama vya Upinzani pio.

  Kauli hiyo ilitolewa Mjini Dodoma jana ,na Katibu wa Fedha na Uchumi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Haidery Gulamali wakati akichukua fomu ya kugombea ujumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho ngazi ya taifa.

  Gulamali alisema ipo tabia imejengeka kuwa ufisadi upo ndani yaCCM pekee jambo ambalo sio la kweli na kuwa ufisadi ni hulka ya mtu binafsi.

  “Kwa kuwa CCM ndicho chama kinachotawala na ndicho chenye wanachama wengi nchini,ufisadi lazima uonekane pamoja na kwamba hata katika vyama vya upinzani upo,” alisema.

  Gulamali alimpongeza Rais Jakaya Kikwete na uongozi wa Chama hicho kwa uamuzi wa kuwaondoa wabunge na wafanyakazi wengine wa Serikali katika uongozi ndani ya chama kwa kuwa kufanya hivyo chama kitaweza kuisimamia Serikali vizuri ikiwemo kupambana na ufisadi.

  Alisema ameamua kugombea nafasi hiyo kwa sababu anatimiza wajibu wake kama mwanachama wa kushika nafasi mbalimbali za uongozi kuwakilisha watanzania.

  Naye mwandishi wetu kutoka mkoani Mara anaripoti kuwa wana CCM watakiwa kukubaliana na matokeo ya uchaguzi kama njia ya kuimarika kwa demokrasia ndani ya chama hicho.

  Kauli hiyo imetolewa na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) kutoka Mkoa wa Mara Vedastus Mathayo, ambapo alisema njia ya kukubali matokeo ya uchaguzi itaepusha kuepusha makundi ambayo yanaweza kujitokeza na kuibua malumbano yasiyo na msingi.

  Kauli hiyo aliitoa hii jana, alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa uchaguzi wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM Musoma Mjini (UWT) katika ukumbi wa mikutano wa CCM katika Makao makuu ya chama hicho Mjini Musoma.

  Alisema mwanachama yeyote anapoingia katika kinyang'anyiro cha uchaguzi ni budi kukubaliana matokeo ya namna mbili kushinda na kushindwa na kuacha kujiingiza katika makundi ya kutafuta mchawi mara baada ya uchaguzi.

  Katika hatua nyingine Mjumbe huyo wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Vedastus Mathayo alichukua fomu ya kutetea nafasi yake katika Ofisi ya CCM Musoma Mjini na kusema kila Mwanachama wa Chama hicho anayo haki ya kuomba nafasi yeyote ya uongozi ndani ya Chama.

  Habari hii imeandikwa Na John Maduhu na Christopher Gamaina, Mwanza, Debora Sanja, Dodoma na Shomari Binda, Musoma.
   
 2. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Captains fighting for a drowning ship
   
 3. Mbwiga88

  Mbwiga88 JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 640
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Huo udokta kaupata wapi?
   
 4. Quicklime

  Quicklime Senior Member

  #4
  Aug 24, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  :A S-baby:kila la kheri diallo ila ajipange na changamoto za M4C
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,818
  Trophy Points: 280
  ...la kuvunda.....
   
 6. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #6
  Aug 24, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mambo yamekuwa mambo
   
 7. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Blame game ikianza ujue mambo si salama.
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Amesharudisha heshma yake yeye mwenyewe kabla ya kukimbilia chama? Tanzania tuna tatizo kubwa sana la watu kutafuta vyeti kwa njia za mkato.

  Anthony Diallo / Alumni Achievers / Alumni / The University of Newcastle, Australia
  [h=2]ANTHONY DIALLO[/h]Consultant, Chairman and CEO of Sahara Media Group, Tanzania, Africa.
  Master of Aviation Management, 2009
  Doctor of Business Administration, 2008
  Master of Business Administration, 2005
  Graduate Certificate in Business, 2004

  2010 FINALIST - ALUMNI AWARD FOR INTERNATIONAL LEADERSHIP
  Dr Diallo has had 12 continuous years in public service and 20 years in management in manufacturing and industrial production and has been the CEO of successful companies. He has been a member of parliament for Mwanza rural and Ilemela constituencies for five and ten years respectively.

  As a Government Minister, he has served as: Deputy Minister, Ministry of Industries and Trade (2000-2001); Deputy Minister, Water and Livestock Development (2001-2005); Minister for Natural Resources and Tourism
  (Jan 2006-Nov 2006); and the Minister, Livestock Development (Nov 2006- Feb 2008).

  He has participated (and on more than five occasions chaired) the Group of 77 Council of Trade Ministers for the WTO Doha round of preparatory negotiations, coordinating the African forum under the auspices of the South African Development Countries and the Group of 77.
   
 9. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #9
  Aug 24, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  tehetehe lakuvunda halikosi ubani mambo zako bak
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Halina ubani!
   
 11. D

  Deogratius Mosha Member

  #11
  Aug 24, 2012
  Joined: Aug 3, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hashindwe kurudisha heshima kwa kurudi bungeni...!!!!!!!, arudishe heshima ccm, yeye mwenyewe gamba ndo maana alishindwa rudi mjengoni....arudishe heshima kwa kuvua magamba
   
 12. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #12
  Aug 25, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  He is a con man!!
   
 13. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #13
  Aug 25, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kwani nani alipoteza heshima ya ccm mwanza? Ubunge ndo amestafu au amepima upepo?
   
 14. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #14
  Aug 25, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 180
  weekend buridani kabisa KAMANDA,huu uzi namwachia mkwongwe RITZ
   
Loading...