Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,773
- 730,052
Wiki hii ngoja tuimalizie na hizi post zinazohusu laana...kwenye ile mada kuhusu ukoo wa Gwajima naona wengi hawakuelewa neno laana kwa muktadha wake
Laana ni kinyume cha baraka na kubarikiwa kwenye kazi za mikono yetu kwenye matendo yetu kwenye fikra na mustakabali wetu
Laana ni dhana pana unapata pesa nyingi lakini hufanyi lolote la maana huna maendeleo! Unakuwa una kila kitu lakini unakuwa huna amani huna furaha una maadui kila kona na matukio hayakuishi na kila tukio likihitaji pesa Ila kwakuwa unazo unakuwa huoni shida ilipo
Kuna kazi za laana Udalali ni mojawapo! Madalali wapo wa aina mbili hawa wa kulipwa kwa makubaliano akishakufanyia kazi yako hawa wana nafuu
Kuna hawa madalali wa kuuza vitu vilivyowekwa dhamana hawa wana laana kubwa pamoja na wale watu wanaonunua vitu vya dhamana
Mtu anayeshindwa kulipa deni mali yake inapouzwa huumia sana huathiri maisha yake na family yake....athari ni kubwa na maumivu pia
Mali zinazonadishwa pia zina yake iwe ni vifaa vya ofisini Biashara nyumba magari nk, huwezi jua mmiliki wa kwanza kapita wapi na wapi kafanya nini! Vingi vina mambo yasiyoeleweka
Nitarejea =====
Tuendelee====
Tuna mifano mingi ya watu waliopoteza maisha kutokana na mali zao hasa nyumba kuuzwa mnadani na madalali katili sana tena kwa bei Poa ....katika hali kama hii dalali anavuna laana kwa kuchuma pesa ya dhambi! Mnunuzi naye anachuma laana kwa kununua mali ya thamani kwa bei Poa
Kuna wale ambao ni matapeli wa kawaida kazi yao ni kucheza michezo hawa hata mali zao zikinadiwa hakuna shida kabisa lakini hawa wengine walioshindwa kurejesha mikopo yao kwa kushindwa kwa sababu za wazi hawa ni wa kuhurumia mali zao
Nikiaangalia nyuma na kuwakumbuka kina BLUE na Majembe waliotamba enzi zao na kupata mahela mengi ya dhuluma! Nikiaangalia nyuma na kuwakumbuka wale waliokuwa vinara wa kununua mali za minada kwa bei ya kutupa na kuuza kwa faida kubwa nabaki na mshangao mkubwa ...cha dhuluma hakina Baraka nunua Leo mali ya mnada lakini Kumbuka kesho inakusubiri
CC: tetee