DHL Africa: Lake "Malawi" has more Fish species

kadoda11

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
21,453
20,740
kampuni ya kimataifa ya kusafirisha mizigo na vifurishi yenye makazi yake ktk nchi kadhaa africa,DHL,kupitia official page yake ya facebook,inalitambua ziwa nyasa kama ziwa Malawi.

wajuvi wa masuala ya kimataifa,hii kitu imekaaje?.

ina athari gani kwa Tanzania?
2356f1304c5f56370fd18fae9bbf383a.jpg

link :
story.php
 
Sisi tupo tu.. ndio maana mlima kilimanjaro wanasema uko kenya,...
nilikuwa nasoma comment za ndg zangu watz kwenye hiyo picha,wamekasirika sana.

wanajaribu kuwaelimisha wamalawi,nao wamalawi wamekomaa kudai ziwa haliitwi Nyasa Bali ni ziwa Malawi.

kwa maana hiyo eti DHL wapo sahihi.

kama hii kampuni ina ofisi nchini,basi wafanyakazi wake wajiandae kupoteza ajira.maana sipati picha reaction ya serikali hii itakuwaje.
 
Hili ziwa kwa upande wa Malawi si linaitwa ziwa Malawi!!?

Yawezekana uchunguzi wao wameufanyia huku hivyo haina sababu ya kuliiita Nyasa
 
ziwa langu nililo ogelea nilipo kuwa kijana mdogo ndio linaondoka aiseee.
 
Hili ziwa kwa upande wa Malawi si linaitwa ziwa Malawi!!?

Yawezekana uchunguzi wao wameufanyia huku hivyo haina sababu ya kuliiita Nyasa
kwenye ramani ya Africa,linatambulika kwa jina gani mkuu?

hudhani DHL wamekosea?
 
Ngoja niitafute ramani kwanza.

Lakini ninacho kumbuka mimi nikuwa hilo ziwa kila sehemu lina jina lake hata kwa upande wa Mozambique linaitwa ziwa Niassa (nisahihishwe kama nimekosea jina) hivyo DHL hawana kosa kama wamefanyia utafiti wao tokea Malawi.
 
basi sawa.
 
Lake Malawi, also known as Lake Nyasa in Tanzania and Lago Niassa in Mozambique, is an African Great Lake and the southernmost lake in the East African Rift system, located between Malawi, Mozambique and Tanzania.Hizi ni taarifa zilizopo Wikipedia.
 
DHL office in Malawi wataita ziwa Malawi...

DHL office in Tanzania wataita ziwa Nyasa..

Majibu ndio hayo hapo juu, hatutaki ujinga, sbb Malawi na Dunia inatujua sisi ni nani, huu uhuni hatutaki, tutawafanya mishikaki naapa, na haitatokea kamwe wazuie raia wetu kuvua Ziwa Nyasa au wao Malawi ku patrol Ziwa Nyasa lote kuwa ni lao, watabakia kubweka bweka tu ktk media mbalimbali kama mbwa muoga.. sisi tunawacheki tu, keleb moja, full flat wote mishikaki:
 
nilikuwa nasoma comment za ndg zangu watz kwenye hiyo picha,wamekasirika sana.

wanajaribu kuwaelimisha wamalawi,nao wamalawi wamekomaa kudai ziwa haliitwi Nyasa Bali ni ziwa Malawi.

kwa maana hiyo eti DHL wapo sahihi.

kama hii kampuni ina ofisi nchini,basi wafanyakazi wake wajiandae kupoteza ajira.maana sipati picha reaction ya serikali hii itakuwaje.

Huko Malawi ziwa kwa lugha yao ni Nyasa. Hivyo kwa kiasi fulani it makes sense kuliita ziwa kwa jina lolote kuliko ziwa nyasa maana ukisema nyasa inamaana "ziwa ziwa":(. Zikomo!
 
DHL office in Malawi wataita ziwa Malawi...

DHL office in Tanzania wataita ziwa Nyasa..

Majibu ndio hayo hapo juu, hatutaki ujinga, sbb Malawi na Dunia inatujua sisi ni nani, huu uhuni hatutaki, tutawafanya mishikaki naapa, na haitatokea kamwe wazuie raia wetu kuvua Ziwa Nyasa au wao Malawi ku patrol Ziwa Nyasa lote kuwa ni lao, watabakia kubweka bweka tu ktk media mbalimbali kama mbwa muoga.. sisi tunawacheki tu, keleb moja, full flat wote mishikaki:
Kwa nini ziwa victoria linaitwa victoria kwenye zote liliopo East Afrika? Hata Idd Amin hakuwahi kuliita ziwa Uganda? Shida nini kwenye hili ziwa malayawi/nyasa.
 
Kwa upande wa Malawi hata wangeliita Lake China sawa tuu
Umenena vizuri
Wakiwa upande wa Malawi hata wakiliita Ziwa Uingereza, Ziwa Malkia, Ziwa Prince Charles hakuna neno
Ila wakiwa hapa nyumbani Tanzania jina ni Ziwa Nyasa
Ova!.
 
mkuu official page ya kampuni ambayo ofisi zake zipo ktk nchi mbili tofauti zenye mgogoro wa kidiplomasia haitakiwi kujiingiza ktk ktk jambo ambalo linabishaniwa na nchi hizo.

kwa maslahi mapana ya kampuni, DHL wamekosea unless otherwise wanapata faida fulani kupitia huu mgogoro.
ni mtazamo wangu tu.
 
Zamani hii nchi ya malawi ilikuwa ikiitwa Nyasa(Nyasaland), hivyo wakati huo hili ziwa halikuwa linaitwa ziwa malawi. Baada ya kubadili jina kutaka nchi ya Nyasa (Nyasaland) na kuiita malawi wakabadili na jina likaitwa ziwa malawi. Mfano sisi zamani nchi yetu ilikuwa inaitwa Tanganyika na kuna ziwa Tanganyika. Baada ya kubadili jina na kuitwa Tanzania na ziwa pia tungebadili jina liitwe ziwa Tanzania, kitu ambacho hatukufanya. Hata kama tungebadili jina la ziwa upande wa Tanzania tusingewalazimisha na Wakongo nao waliite ziwa Tanzania. Sisi tunaendelea kuliita ziwa nyasa baaaasi.
 
kwenye ramani ya Africa,linatambulika kwa jina gani mkuu?
hudhani DHL wamekosea?

Huko Malawi ziwa kwa lugha yao ni Nyasa. Hivyo kwa kiasi fulani it makes sense kuliita ziwa kwa jina lolote kuliko ziwa nyasa maana ukisema nyasa inamaana "ziwa ziwa":(. Zikomo!

Hata Malawi ziwa hili lilikuwa likijulikana kwa jina la 'Lake Nyasa'
Na jina 'Lake Nyasa' ndilo jina liliochwa na mkoloni Mwingereza
Mawalawi ndio waliobadili jina na kuliita 'Lake Malawi' ili liendane na jina jipya la nchi yao
Kwa hiyo ukitazama ramani zote za kale hasa za mkoloni mwingereza na mjerumani jina utakalo kutana nalo ni 'Lake Nyasa'
Pamoja na Malawi kuliita 'Lake Malawi' sisi Tanzania na Msumbiji tuliendelea kutumia jina 'Lake Nyasa', Na wenzetu wa msumbiji kwa kilugha chao Nyasa ni Niassa
Hivyo wakitaka kusema 'Lake Nyasa' wanasema 'Lago Niassa'
 
Zamani hii nchi ya malawi ilikuwa ikiitwa Nyasa(Nyasaland), hivyo wakati huo hili ziwa halikuwa linaitwa ziwa malawi. Baada ya kubadili jina kutaka nchi ya Nyasa (Nyasaland) na kuiita malawi wakabadili na jina likaitwa ziwa malawi. Mfano sisi zamani nchi yetu ilikuwa inaitwa Tanganyika na kuna ziwa Tanganyika. Baada ya kubadili jina na kuitwa Tanzania na ziwa pia tungebadili jina liitwe ziwa Tanzania, kitu ambacho hatukufanya. Hata kama tungebadili jina la ziwa upande wa Tanzania tusingewalazimisha na Wakongo nao waliite ziwa Tanzania. Sisi tunaendelea kuliita ziwa nyasa baaaasi.
Naona tumegongana, vizuri lakini na wewe kuwapa darasa
 
Back
Top Bottom