Dharau

konda : cheke cheke! abilia nauli

abiria: mi mwalimi

konda: onyesha kitambulisho

mwalimu: (anashika mfukoni) hiki hapa

konda (anakichukua kile kitambulisho na kukikodolea macho pande zote mbili)....

konda: (anarudisha kitambulisho) sasa mbona umekalia siti

mwalimu : kwan kuna tatizo?

konda: hebu wapishe waliolipa nauli wakae

mwalimu: (kwa hasira) hebu acha kunizaliliasha kijana

konda: (akimuangalia mwalimu usoni) hivi we unaona ni haki kukaa wakati alielipa nauli amesimama?

mwalimu (kimya)

konda: kwanza nyie walimu nina hasira na nyie sana

mwalimu (kwa ghadhabu) hasira?

konda: eeh kwanza mlinichapa sana bado nifeli.... na leo unapanda gari yangu huna nauli..

abiria wengine: hahahahahaha

konda: dah yani sipendi kupakia hizi chenga kubwa

mwalimu: nani chenga?

konda : yan wewe ni chenga kuliko huyo mwanafunzi unaemfundisha

mwalimu: (kwa tabasamu la aibu) kivipi?

konda : we umekalia siti hujalipa hata mia lakin dogo kasimama na amelipa 200..

konda (kwa kejeli) sasa sema wewe na dogo nan chenga?

mwalimu (kwa hasira anafungua pochi na kutoa sh 5000 ) kata mia nne yako mbwa wewe.


MAKONDA WAZO LAKO NI GUMU KUTEKELEZEKA LABDA MWALIMU AWE NA ROHO YA JIWE
 
Hii Nchi ina kazi!! Na kazi yenyewe wala hakuna anayeijua
 
Umeona eeeeh. Dawa ni kuwapa Transport allowances na sio kuwadharirisha kama wanavyofikiria.
 
[emoji25] [emoji25] [emoji25] [emoji25] [emoji25] [emoji25]
 
mwalimu anapogeuzwa sehemu ya dhihaka mitandaoni
 
daaah kweli mwalimu anadharirishwa sana angali yeye ndo mzalishaji wa fani nyingine
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…