pastor masumbuko
Member
- Apr 23, 2016
- 67
- 195
Watumishi mbarikiwe sana
Nimetumwa kuja kwenu kuwakumbusha wajibu wenu katika ndoa
Kumekuwepo na wimbi kubwa la akina dada kutoka nje ya ndoa zao kwa ajili ya kulipa kisasi baada ya kuwashika au kuwafuma waume zao wakizini nje, hii ni kinyume na fundisho la Biblia na imekatazwa
Kwa mujibu wa mathayo 19:9
Biblia inamruhusu mtu aliefunga ndoa kumtaliki mwenzi wake ikiwa tu mwenzi huyo amefanya uasherati
Hilo humaanisha kuwa baada ya uzinzi kufanyika mwenzi asie na hatia ana haki ya kuamua iwapo ataendelea kuishi na mwenzi asie mwaminifu au kuomba/kutoa talaka
Huu ni uamuzi wa mtu binafsi wagalatia 6:5
Kwa muktadha huu mwanamke hapaswi kulipa kisasi kwa kutembea nje pia bali kama mumewe amekua msumbufu kwa uzinzi kupita kiasi na ameonywa mara kadhaa bila kuacha basi mke aombe talaka anaruhusiwa kwa mujibu wa maandiko,
Lakini Hali kwa sasa imekua tofauti katika nyumba nyingi, mke anasalitiwa na mume, kisha na yeye anakwenda kutafuta farijiko nje, kwa nn kutoka hutaki halafu mwisho wake unatembea nje na kisha kufumaniwa ambapo ww sasa ndio ukaonekana ulie shindikana kushinda mumeo
Kama umemfuma mme wako na unadhani unahitaji faraja nje ni vema ukatoka kuliko kuanza kushindana kwa dhambi
MUNGU huchukia talaka, hili linapaswa kuwa jambo la mwisho kabisa, kusamehe kunapaswa kutangulizwa mbele, juhudi kubwa za kusameheana zinapaswa kuchukuliwa, cha ajabu akina dada wengi atakubali mbele ya wasuluhishi kuwa amesamehe lakini baadae anatoka nje kulipiza kisasi, sasa ulisamehe nini?
Madhara ya mke kulipiza kisasi huwa ni makubwa hii ni pamoja kuleta ndani mtoto wa nje na kumsingizia mumeo, siku ambazo mwanamke yupo salama ni chache kulinganisha na alizo salama, kama anafanya zinaa na huyo mfariji wake mara kwa mara chances za kubeba mimba ya nje ni kubwa, pia upendo utapoa kwa mumewe, mwanamke haendi nje kwa kutamani, akienda nje ni wazi amempenda huyo mzinzi mwenzie kutoka moyoni, hivyo chances za mgogoro zaidi kwenye ndoa ni kubwa
Pia, Kuna kufumaniwa, nimeeleza kuwa mwanamke akienda nje ni wazi amempenda huyo hawara kutoka ndani hivyo hupoteza umakini na kuchanganyikiwa na penzi jipya la nje, mwisho wake ni mauti, nadhan wote mmesikia wake za watu wakikutwa na mauti guest, wengine wakiuawa kwa kuchinjwa kama kuku baada ya kufumwa na waume zao wakizini, wengine wamesababisha vifo vya wale wanaofumwa nao ikiwa ni pamoja na kulawitiwa
Sasa basi huna sababu ya kukutwa na masahibu yote haya, mme wako anaposaliti ndoa yako muendee MUNGU nae atakufungulia njia, epukana na marafiki wanaoweza kukushauri kutafuta faraja nje wakikudanganya kwamba hata wao walifanya hivyo wenzi wao walipozini, faraja pekee iko kwa MUNGU, mtafute MUNGU kwa nguvu zote nae atakushindia
Mbarikiwe sana