Dhana ya wanawake kulipiza kisasi katika ndoa

Apr 23, 2016
67
195
Watumishi mbarikiwe sana

Nimetumwa kuja kwenu kuwakumbusha wajibu wenu katika ndoa

Kumekuwepo na wimbi kubwa la akina dada kutoka nje ya ndoa zao kwa ajili ya kulipa kisasi baada ya kuwashika au kuwafuma waume zao wakizini nje, hii ni kinyume na fundisho la Biblia na imekatazwa

Kwa mujibu wa mathayo 19:9
Biblia inamruhusu mtu aliefunga ndoa kumtaliki mwenzi wake ikiwa tu mwenzi huyo amefanya uasherati

Hilo humaanisha kuwa baada ya uzinzi kufanyika mwenzi asie na hatia ana haki ya kuamua iwapo ataendelea kuishi na mwenzi asie mwaminifu au kuomba/kutoa talaka
Huu ni uamuzi wa mtu binafsi wagalatia 6:5

Kwa muktadha huu mwanamke hapaswi kulipa kisasi kwa kutembea nje pia bali kama mumewe amekua msumbufu kwa uzinzi kupita kiasi na ameonywa mara kadhaa bila kuacha basi mke aombe talaka anaruhusiwa kwa mujibu wa maandiko,
Lakini Hali kwa sasa imekua tofauti katika nyumba nyingi, mke anasalitiwa na mume, kisha na yeye anakwenda kutafuta farijiko nje, kwa nn kutoka hutaki halafu mwisho wake unatembea nje na kisha kufumaniwa ambapo ww sasa ndio ukaonekana ulie shindikana kushinda mumeo

Kama umemfuma mme wako na unadhani unahitaji faraja nje ni vema ukatoka kuliko kuanza kushindana kwa dhambi

MUNGU huchukia talaka, hili linapaswa kuwa jambo la mwisho kabisa, kusamehe kunapaswa kutangulizwa mbele, juhudi kubwa za kusameheana zinapaswa kuchukuliwa, cha ajabu akina dada wengi atakubali mbele ya wasuluhishi kuwa amesamehe lakini baadae anatoka nje kulipiza kisasi, sasa ulisamehe nini?

Madhara ya mke kulipiza kisasi huwa ni makubwa hii ni pamoja kuleta ndani mtoto wa nje na kumsingizia mumeo, siku ambazo mwanamke yupo salama ni chache kulinganisha na alizo salama, kama anafanya zinaa na huyo mfariji wake mara kwa mara chances za kubeba mimba ya nje ni kubwa, pia upendo utapoa kwa mumewe, mwanamke haendi nje kwa kutamani, akienda nje ni wazi amempenda huyo mzinzi mwenzie kutoka moyoni, hivyo chances za mgogoro zaidi kwenye ndoa ni kubwa

Pia, Kuna kufumaniwa, nimeeleza kuwa mwanamke akienda nje ni wazi amempenda huyo hawara kutoka ndani hivyo hupoteza umakini na kuchanganyikiwa na penzi jipya la nje, mwisho wake ni mauti, nadhan wote mmesikia wake za watu wakikutwa na mauti guest, wengine wakiuawa kwa kuchinjwa kama kuku baada ya kufumwa na waume zao wakizini, wengine wamesababisha vifo vya wale wanaofumwa nao ikiwa ni pamoja na kulawitiwa

Sasa basi huna sababu ya kukutwa na masahibu yote haya, mme wako anaposaliti ndoa yako muendee MUNGU nae atakufungulia njia, epukana na marafiki wanaoweza kukushauri kutafuta faraja nje wakikudanganya kwamba hata wao walifanya hivyo wenzi wao walipozini, faraja pekee iko kwa MUNGU, mtafute MUNGU kwa nguvu zote nae atakushindia

Mbarikiwe sana
 
The days of getting mad are pretty much done and over with.

Now it's all about getting even.

So don't get mad, get even!
 
Asante mchungaji kwa kutukumbusha,lakini tambua hakuna kitu muhim km amani ya moyo,ukiikosa unajiona bora ufe.kuchepuka hatupendi na ni dhambi lakin amani itapatikanaje??ikiwa kila siku ni karaha unamuona kabisa mwenzako haeleweki.na ukisema tutoke na hao watt itakuwaje??endelea kutoa neno mchungaji lakin huku hali ni mbaya,waelimishe hao me kwanza mana ndo chanzo cha matatizo yte
 
Mtumishi umesema vizuri, ubarikiwe, somo la uzinzi kwa wanaume katika ndoa tumelizungumza mara nyingi katika majukwaa mbali mbali na ndio chanzo cha vurugu katika ndoa, ndio maana mwanzo kabisa nimekiri kuwa wanawake hulipiza kisasi baada ya wanaume wao kuchepuka kwanza, hivyo ni somo linalojitegemea litakua na siku yake
Naomba wanawake mjitahidi sana kuwa wavumilivu maana nyie ndio mmeshikilia nyumba zetu, ndio nguzo, mwanamke akiyumba ndani ya ndoa basi nyumba hamna hapo tena
 
Pole sana.. tulia kwenye ndoa yako.. mkuki kwa nguruwe.. kwa binadamu...
 
Asante mchungaji kwa kutukumbusha,lakini tambua hakuna kitu muhim km amani ya moyo,ukiikosa unajiona bora ufe.kuchepuka hatupendi na ni dhambi lakin amani itapatikanaje??ikiwa kila siku ni karaha unamuona kabisa mwenzako haeleweki.na ukisema tutoke na hao watt itakuwaje??endelea kutoa neno mchungaji lakin huku hali ni mbaya,waelimishe hao me kwanza mana ndo chanzo cha matatizo yte
Dawa ya moto sio moto mamii. Yeah ukiamua kuchepuka utapata amani ya moyo kwa muda tuu lakini hautakua umesolve tatizo ...zaidi ya kuambulia magonjwa, aibu n.k

The best solutions ya mwanaume mchepukaji ni kukaa kuchunguza nn chanzo then kutatua

Vilevile kumuombea Mume wako.
 
Nimekuelewa kakangu.lakini tambua mume anauma kupita maelezo,na mpk ifikie mke kuchepuka tambua amevumilia mengi.hakuna namna,mpango wa kando kuleta amani ndo mambo yte
 
mtumishi nimekuelewa sana ila nilitaka niwakumbushe jambo moja ambalo hapa hujalizungumzia

katika kitabu cha 1kor 7:10-11 inaagiza watu waliooana wasiachane na ikiwa wameachana(kwa sababu ya uasherati) bas wanaagizwa kutokuolewa tena au kuoa tena, kwahyo sio kwamba tu utampa talaka bali pia ukubali kubaki hivo mpk labda mwenzako akifariki ndio unaweza kuruhusiwa kuoa au kuolewa tena.

Ndio maana ndoa nyingi hasa hizi za kikristo kiapo chake ni mpk kifo kiwatenganishe..

Kitu cha msingi hapa ni kujiandaa kisaikolojia kuwa na uwezo wa kusamehe...

#Ndoa na iheshimiwe na watu wote
 
Similar Discussions

9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom