Dhana ya Utawala Bora, nini maana yake?

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
20201124_175214_0000.png
Utawala ni matumizi ya mamlaka ya kisiasa, kiuchumi au vinginevyo katika kusimamia masuala ya nchi kwenye ngazi zote.​

Utawala bora ni matumizi ya mamlaka ambayo yanakuwa na uwazi, uwajibikaji, ushirikishaji wa watu, ufanisi, tija, uadilifu usawa na unafuata utawala wa sheria.

Ili kutekeleza dhana ya utawala bora mambo yafuatayo lazima yazingatiwe: •Matumizi sahihi ya dola,
•Matumizi mazuri ya rasilimali kwa faida ya wananchi,
•Matumizi mazuri ya madaraka yao,
•Kujua na kutambua madaraka waliyonayo na matumizi yake,
•Madaraka yanatumika kulingana na mipaka iliyowekwa na katiba na sheria.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom