Dhana ya Ukomo wa Uongozi Inadumaza Afrika

Goodrich

JF-Expert Member
Jan 29, 2012
2,091
1,177
Binafsi huwa siamini katika ukomo wa muda wa uongozi.

Mimi nadhani kama kiongozi ni mbovu au dhaifu hapaswi au sio lazima kukaa miaka 5 au 10 madarakani, eti amalize muda wake.

Na kama kiongozi ni mzuri, jasiri, mzalendo, mwenye kuipenda nchi yake, na kupendwa na wananchi sio lazima aondoke baada ya miaka 10, eti muda wake umeisha.

Na mbaya zaidi dhana hii hutumiwa na mataifa makubwa kwa Afrika tu, na sio Ulaya, wala Uchina.

Nadhani jambo la muhimu ni kuwa na mfumo thabiti na huru wa uchaguzi na wa kuwajibisha viongozi.

Ukomo wa uongozi kwa Afrika unalinda viongozi wabovu, na wakati huohuo kuondoa viongozi wazuri kwa kigezo cha muda.

Sio kila tunachoambiwa na wazungu ni sahihi.
 
Afrika bado hatujawa na mifumo inayoweza kuwapa nafasi wananchi kuidhibiti serikali. Tume za uchaguzi huwa kama kitengo cha serikali iliyopo madarakani.
Kwa maana hiyo, ni vyema kuwa na ukomo kikatiba.
 
Ni kweli kabisa,
Sisi waafrika tumekuwa watu wa kuiga kila kitu au kufuata maelekezo ya wazungu.
Walitumia sababu hiyohiyo kumuondoa Gadaffi
 
Ukiruhusu hili nchi za Afrika zitageuka kuwa nchi za Kifalme.
 
Kinachotakiwa ni mfumo huru wa uchaguzi na namna bora ya kuiwajibisha serikali.

Kiongozi mbovu hamalizi mwaka, na kiongozi mzuri anaendelea kugombea na kuongoza kwa ridhaa ya wananchi
 
vipi umetumwa na mbowe kuja kutetea baada ya kunyofoa kinyemela kipengele cha ukomo wa uongozi chadema? au?

Binafsi huwa siamini katika ukomo wa muda wa uongozi.

Mimi nadhani kama kiongozi ni mbovu au dhaifu hapaswi au sio lazima kukaa miaka 5 au 10 madarakani, eti amalize muda wake.

Na kama kiongozi ni mzuri, jasiri, mzalendo, mwenye kuipenda nchi yake, na kupendwa na wananchi sio lazima aondoke baada ya miaka 10, eti muda wake umeisha.

Na mbaya zaidi dhana hii hutumiwa na mataifa makubwa kwa Afrika tu, na sio Ulaya, wala Uchina.

Nadhani jambo la muhimu ni kuwa na mfumo thabiti na huru wa uchaguzi na wa kuwajibisha viongozi.

Ukomo wa uongozi kwa Afrika unalinda viongozi wabovu, na wakati huohuo kuondoa viongozi wazuri kwa kigezo cha muda.

Sio kila tunachoambiwa na wazungu ni sahihi.
 
vipi umetumwa na mbowe kuja kutetea baada ya kunyofoa kinyemela kipengele cha ukomo wa uongozi chadema? au?

We kweli Abunuas, unaota CDM muda wote.

Hapa tunaongelea uongozi wa kitaifa, sio vyama, wala ubunge wala udiwani.
 
Last edited by a moderator:
Nilikuwa nahisi hili jambo kinanitatiza pekee yangu kumbe kuna watanzania wenzangu hili linawagusa kwakweli..........mimi nadhani kiongozi kama magufuli anatakiwa kupewa muda zaidi ya ambao umeainishwa katika katiba yetu tukufu........mtu kama kikwete alitakiwa kuishia mwaka 2008........maana hakuwa na faida......kama vile RWANDA inavyomutaji kagame kwa muda wa ziada hadi pale atapoanza kuchuja then atafutwe kiongozi mpya.........
 
Binafsi huwa siamini katika ukomo wa muda wa uongozi.

Mimi nadhani kama kiongozi ni mbovu au dhaifu hapaswi au sio lazima kukaa miaka 5 au 10 madarakani, eti amalize muda wake.

Na kama kiongozi ni mzuri, jasiri, mzalendo, mwenye
kuipenda nchi yake, na kupendwa na wananchi sio lazima aondoke baada ya miaka 10, eti muda wake umeisha.

Na mbaya zaidi dhana hii hutumiwa na mataifa makubwa
kwa Afrika tu, na sio Ulaya, wala Uchina.

Nadhani jambo la muhimu ni kuwa na mfumo thabiti na huru
wa uchaguzi na wa kuwajibisha viongozi.

Ukomo wa uongozi kwa Afrika unalinda viongozi wabovu, na wakati huohuo kuondoa viongozi wazuri kwa kigezo cha muda.

Sio kila tunachoambiwa na wazungu ni sahihi.
Huna haja ya kulaumu wazungu, Katiba za kuweka ukomo wa uongozi tunatunga wenyewe. Tatizo baada ya kutunga, viongozi walewale waliotunga, muda ukikaribia kwisha wanaanza kushawishi kubadili Katiba ili kuondoa ukomo wa Uongozi. Hatuna uwezo wa kuheshimu Katiba zetu. Marekani wana ukomo na nchi nyingi za Ulaya hazina
ukomo wa uongozi lakini wanaheshimu Katiba zao. Tatizo ni sisi si wazungu.
 
''Beat Job'' Acha kuwazia Ujuha. unataka kutuletea masuala ya kifalme. kwa misingi ya chaguzi zetu hata akiwa bomu atachakachua na kujifanya anapendwa hadi kifo kimtenganishe na uongozi, wakati huo makabwela tutakuwa more than malofa.
 
Huna haja ya kulaumu wazungu, Katiba za kuweka ukomo wa uongozi tunatunga wenyewe. Tatizo baada ya kutunga, viongozi walewale waliotunga, muda ukikaribia kwisha wanaanza kushawishi kubadili Katiba ili kuondoa ukomo wa Uongozi. Hatuna uwezo wa kuheshimu Katiba zetu. Marekani wana ukomo na nchi nyingi za Ulaya hazina
ukomo wa uongozi lakini wanaheshimu Katiba zao. Tatizo ni sisi si wazungu.

Lini uliwahi kutunga katiba, au hata kuipigia kura ?
 
Back
Top Bottom