Dhana ya Polisi Jamii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dhana ya Polisi Jamii

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by hovyohovyo, Jul 23, 2012.

 1. hovyohovyo

  hovyohovyo JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 540
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Wanajf. Said Mwema anafahamika kwa kusisistiza dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi. Ninachojiuliza, ni kwa kiasi gani amewafanya raia wawe na imani na watendaji wa jeshi hili?, Rushwa kwa mfano ya polisi usalama barabarani, kero za Polisi 'tigo", kashfa mabalimbali za jeshi kutumika kwa maslahi ya chama tawala, kuwashughulikia wapinzani nk. Haya yote kwa maoni yangu yanafanya dhana nzima iwe ngumu kufanikiwa.

  Hivi majuzi nilishuhudia kisa cha wanakijij wakishangilia baada ya kuona polisi akipigwa na mbabe mmoja wa kijij. Askari huyu anafahamika kwa usanii na kuonea watu pale kijijini, lakini siku ya siku akakumbana na jamaa ambaye hakukubali. Alipoambiwa na askari twende huku amevutwa suruali anakanyagia vidole gumba tu, akaona huu utoto. Kujitetea kuwa aachwe ajitembelee mwenyewe, kosa kwa askari. akaanza kushushiwa kipigo. Jamaa akaona shida yote ya nini na 'mikono' naiweza?? Akaanza kumtandika askari kama mtoto mdogo. Kilichonishangaza ni baada ya kuona watu wakishangilia, badala ya kwenda kumwokoa askari. Wengi wao walimsifia raia. Nikajiuliza. je hii dhana ya ulinzi shirikishi na polisi jamii itawezekana vp kama bado watu wanaliona jeshi kama 'oppressive' na 'kero'?
   
Loading...