meningitis
JF-Expert Member
- Nov 17, 2010
- 8,349
- 4,674
mara nyingi kwa siku za karibuni tumesikia kampeni ya kipolisi inayoenda kwa jina la polisi jamii.kampeni hii pamoja na mambo mengine imelenga kujenga ukaribu wa polisi na raia ili kuzuia uhalifu.kampeni ilitakiwa kuwa kiunganishi na sio ukuta kati ya polisi na raia.
Vilevile kumekuwepo na ongezeko la ripoti za matukio ya polisi kuwatwanga raia risasi zinazopelekea vifo au majereha.mifano ni pamoja na arusha,tarime,mbeya,dodoma,iringa na leo hii songea.
Kuna taarifa kadhaa kulingana na vyombo vya habari mbalimbali zimeonyesha mafanikio ya polisi dhidi ya uhalifu yametokana na taarifa zinazotolewa na raia wema.
Ukijaribu kufuatilia utekelezaji wa dhana hii unaonyesha mafanikio kwa raia kutimiza wajibu wao......lakini jeshi la polisi halijafanya hivyo,bado jeshi la polisi linataka kuonekana wao ndio wao,kwa maneno mengine polisi hawajaonesha ushirikiano kwa raia.
Je tatizo ni elimu ya watendaji wa polisi?
je tatizo ni siasa za nchi yetu?
Je tatizo ni viongozi(waziri wa mambo ya ndani,IGP,RPCs)