Dhana ya ndoa na matokeo yake

Karim Mussa

Member
May 6, 2019
21
5
MAANA YA DHANA YA NDOA.
Ni ile hali ya mwanaume na mwanamke kuishi pamoja na kushea kila kitu pamoja huku wakiwa au kupewa hadhi ya mume na mke katika jamii, ambao wameiishi pamoja kwa miaka miwili pamoja au zaidi ya miaka miwili, Kama kifungu cha 160 kifungu kidogo cha Kwanza cha sheria ya ndoa ambayo imefanyiwa marekebisho mwaka 2010 kinavyoelezea kuhusiana na maana ya dhana ya ndoa.

Dhana ya ndoa ambayo inathibitika kwa ushahidi kamili wa watu kukaa kama pamoja zaid ya miaka miwili na kushea kila kitu pamoja huku jamii ikawatambua kama mke na mume kwa hadhi waliopata kwenye jamii hiyo, hiyo dhana ya ndoa itakuwa dhana inayostahiki (REBUTTABLE PRESUMPTION) na uhalali wa dhana hiyo itakuwa ni ndoa (DULY MARRIAGE), na kinyume yake ya dhana hiyo ya Ndoa itakuwa ni dhana isiyostahiki (IRREBUTTABLE PRESUMPTION) kama kifungu cha 159 cha sheria ya ndoa ambayo imefanyiwa marekebisho mwaka 2010 kinavyoelezea.

DHANA YA NDOA INAREKEBISHIKA
Matatizo au ugomvi katikaa maisha ya ndoa hayaepukiki lazima kutakuwa na kutoelewana baina ya wanadhana hao, lakin hawawezi chukua jukumu la kutengana kwa mara tu wanapokoseana, bali wanatakiwa kukuaa chini na kutatua matatizo au ugomvi wao ili waishi kwa amani na upendo kama awali, ila wakiona wao wenyewe hawawezi kutatua tatizo yao kwa sababu moja au nyingine, basi wanatakiwa kwenda katika taasisi za usuluhishaji wa ndoa mfano BARAZA LA KATA, ili wapate suluhisho na warudi kukaa kama awali kwa upendo na amani, ili kama mungu akiwajaalia wafunge ndoa kabisa.

Na kama ikishindikana kuwasuluhisha basi taasisi walioenda kupeleka matatizo yao na kujaribu kuwasuluhisha litatoa amri yake ya kuwa mgogoro uende mahakamani kwa ajili ya masuluhisho au maamuz mengine .

DHANA YA NDOA INAVUNJIKA
Ndio dhana ya ndoa inavunjika iwapo imeshindikanika kurekebishika kabisa matatizo yao na kupata suluhisho baina ya wanadhana hao wa ndoa na, mahakama itakuwa msuluhisho wa mwisho kwa hiyo dhana ya ndoa ya wanadhana hao, na mahakama itasuluhisha matatizo ya wanadhana hao wa ndoa kwa namna mbili, moja ni kuivunja kabisa na ya pili ni kuwatenganisha kwa muda ili kuwaangalia Kama wataondoa tofauti zao na kurudi kukaa pamoja kama awali, endapo itathibitika kuwa dhana hiyo ya ndoa ni dhana inayostahiki (REBUTTABLE
PRESUMPTION), kama kifungu cha 160 kifungu kidogo cha pili cha sheria ya ndoa ambayo imefanyiwa marekebisho mwaka 2010 kilivyoelezea.

MATOKEO YA DHANA YA NDOA KUVUNJIKA .
Siku zote kila kitu huwa na matokeo, matokeo hayo huweza kuwa chanya au hasi kwa wahusika kwa namna moja au nyingine,

Kimfano wanadhana ya ndoa wakabahatika kupata watoto katikaa maisha yao ya dhana ya ndoa, hii inaweza kuwa na matokeo hasi kwa watoto kwa kuwasababishia matatizo kama wanadhana hao wa ndoa wakiachana Kama watoto mwenyewe ni wadogo, matatizo yenyewe ni:

(1) kukosa raha ya kulelewa na wazazi wote wawili,
Maamuz ya mahakama ni kuvunja dhana ya ndoa au kuwatenganisha kwa muda kwa lengo la kujitazamia kama watarudiana, Sasa kama wazazi watakuwa wametenganishwa, watoto nao kama watakuwa chini ya umri wa miaka 7, watakuwa na mama hivyo kukosa malezi ya baba, na baba ataamuriwa kuleta malezi kwa wanawe, kama kifungu cha 160 kifungu kidogo cha pili cha sheria ya ndoa ambayo imefanyiwa marekebisho mwaka 2010 kinavyoelezea.

(2) matatizo ya kisaikolojia (psychological problem)
Mtoto anaweza pata matatizo ya kisaikolojia( psychological problem) kwa kuona kuwa kuna vitu anavikosa sana na hasa matatizo ya kisaikolojia (psychological problem) yanakuja kwa mtoto kwawaza sana, na hivyo humpelekea kufeli au
kushuka kiuwezo wake wa kimasomo yote sababu kubwa ni utengano wa wazazi ambao ndio utakaomsababishia kuwa au kupata matatizo ya kisaikolojia (psychological problem) ambayo yanamadhara makubwa sana.

MWENYE JUKUMU LA KUWATUNZA WATOTO KAMA DHANA YA NDOA ITAVUNJIKA
Jukumu la kuwatunza watoto na kuwapa mahitaji yao yote huwa ni kwa baba, ndiye mwenye wajibu wa kuwatunza watoto wake, kama kifungu cha 160 kifungu kidogo cha pili cha sheria ya Ndoa ambayo imefanyiwa marekebisho mwaka 2010 kinavyoelezea.

Ila kama watoto wapo chini ya umri wa miaka 7, watakaa na mama, na kama wapo juu ya miaka 7 basi wazazi wanatakiwa wakubaliane ni wapi watoto watakaa, ikishindikana basi mahakama italazimika kuwahoji watoto na kutaka kujuaa ni sababu zipi huwafanya wao wakae kwa mzazi fulani? na kumuacha mzazi fulani? au nisababu ipi inayompekekea yeye kukaa na mzazi fulani na kumwacha mzazi fulani? Kisha baada ya hapo mahakama itatoa uamuz wapi watoto watakaa.

MGAWANYO WA MALI WALIZOCHUMA PAMOJA ENDAPO WANADHANA YA NDOA WAKIACHANA.
Mgawanyo wa mali utakuwa kama inavyoelezea kifungu cha 160 kifungu kidogo cha pili cha sheria ya ndoa ambayo imefanyana ya ndoa, mwanamke atakuwa na haki ya kupata matunzo ambayo yatamsaidia yeye katikaa maisha yake, hii ni kutokana na kesi ya BI HAWA MUHAMMAD CASE, ambayo kesi hii ilileta mchango mkubwa wa mwanamke kupata matunzo hata kama hajachangia, kwa sababu mwanamke ndiye anaebaki nyumbani na kufanyaa shughuli zote za nyumbani, hachilia mbali na kufanyaa shughuli zote za nyumbani hufanya vitu vingine vingi vinavyomfanya mwanaume akili yako kutulia na kupata mawazo mengi ya jinsi gani afanye ili apate mali nyingi, kwa sababu ya hayo mwanamke anatakiwa kupata matunzo hata kama hajachangia kitu (namaanisha kuchangia kipesa).

Na kama mwanamke pia kuchangia upatikanaji wa mali hizo kifedha na kimawazo, basi mahakama itagawanya mali hizo kwa kadri ya ushahidi wakila muhusika juu ya uchangiaji huo wa mali zilipotikana wakati wa maisha yenu ya dhana ya ndoa, kama kifungu cha 160 kifungu kidogo cha pili cha sheria ya ndoa ambayo imefanyiwa marekebisho mwaka 2010 kinavyoelezea.

Kama una maoni ushauri mawazo usikose kuweka na Kama una maswali usikose kuuliza kwani kuelewa kwako ndio mwanzo wa jamii pia kuelewa.

Kama una mengi zaidi basi wasiliana nami katika nambari yangu 0755 395572 na kwenye Email yangu: karimbinmussa@gmail.com
Imeandikwa na kuletwa kwenu na Karim mussa
.
 
Back
Top Bottom