Mara nyingi huwa naona marais, uzinduzi mahari fulani, matamasha na sehemu nyingi hutumia red carpet kama kuonyesha ni inshu VIP kwa maana nyingi inshu ya hadhi ya juu.
Swali langu kwanini watumie red carpet na sio blue, black, green e.t.c?
Mara nyingi huwa naona marais, uzinduzi mahari fulani, matamasha na sehemu nyingi hutumia red kapeti kama kuonyesha ni inshu VIP kwa maana nyingi inshu ya hadhi ya juu,
Swali langu kwa nn watumie red capet na sio blue,black, green e.t.c????
Hadi sasa hakuna MTU mwenye uhakika sana wa chanzo cha matumizi ya "Zulia jekundu", lakini imekuwa ikiaminika kuwa historian yake ilianza kwenye mchezo 'igizo' wa Agamemnon uliondikwa na mwandishi was Kigiriki Aeschylus mnano 458BC.
Katika igizo hilo , Agamemnon anakaribishwa nyumbani na mkewe Clytemnestra akiwa anatokea Troy, katika ukaribisho huo Clytemnestra alimtandikia mumewe zulia rangi nyekundu (rangi za miungu) .
Kwa namna moja au nyingine inaaminika kuwa utaratibu huo uliendelea kurithiwa miaka hadi miaka , na umekuwa ukitumiwa mahususi kwa watu wenye kutambulika katika jamii.
katika miaka ya usasa , matumizi yake inaaminika yalianza mwaka 1902 wakati ambapo New York Central Railroad walikuwa wakitumia zulia LA ranging jekundu kama njia ya kuwaelekeza watu wakati wa kupanda ndege.
Matumizi mengine yamekuwa ni kwa ajili ya ukaribisho wa watu mashuhuri ambapo huwa wanafanya kitu kinaitwa "Red Carpet Walk" imekuwa ikielezwa ni namna ya kuonesha ukarimu au umuhimu kama ule wa kifalme.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.