Dhana ya maendeleo.

Shayu

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Messages
544
Likes
874
Points
180
Shayu

Shayu

Platinum Member
Joined May 24, 2011
544 874 180
Dhana ya maendeleo imelala kwa watu. Iko kwenye kuwekeza katika watu na kuwapa uwezo, imelala katika maarifa. Watu wakiendelea ( wakiwa na skills na knowledge za kutosha) ndizo zinazofanya waendelee. Kuendelea kuelekea wapi? Kwenye kujitegemea kwao au kwa maana nyingine ( To unleash their fullest pontential). Tunapopanda mmea wa waridi tunajua mwisho wake ni kutoa maua waridi kama haujafanikiwa kufika huko haujakamilika na vile vile kwa taifa mwisho wake ni kujitegemea kwake. Kujitegemea ni kufikia ukuaji wake wa mwisho. Watoto wa wanyama na binadamu huzaliwa na mwisho wa ukuaji wao ni kujitegemea. Vile vile kwa taifa ni hivyo hivyo.

Yaani kuwa na watu wenye skills za kutosha za kutufanya kutumia tunachozalisha kwa mikono yetu. Huo ndio unapaswa kuwa mwelekeo wetu kama taifa. Ni lazima na ni muhimu kuwekeza kwa watu ni lazima tuwe na strategy. Na mipango hii inawezekana kama tukiwa na watu royal na commited to the cause.

Development ya nchi huendana na ukuaji wa kiakili wa watu ni issue ya kujitambua pia, je watu wanajitambua? Je wana uwezo gani wa kuzalisha? Watu wakiwa na uwezo wa kuzalisha na kutengeneza vitu ambavyo tunatumia wenyewe tutakuwa tunapiga hatua.

Kuna issue ya uzalendo na utaifa inaingia hapa pia. Sasa hivi watu wetu wamegawanyika sana hawana malengo ya pamoja. Kila mtu anafuata njia yake no national goals. People are so selfish. Vyama vya siasa vina selfish agendas. Tunawezaje kwenda mbele kama taifa? Bila ya kuwa na umoja na bila ya kuwa na malengo ya kitaifa yanayo tuunganisha? Tumebaki kuwa na ushabiki na kushabikia watu. Hakuna vision. Hakuna solid national goals. Sitaki kutukana lakini na observe ujinga mwingi usio na maana. We are not rational anymore hatujui tunapoenda. Hakuna national goals. Kama ziko zipo vitabuni wananchi hawazijui hawajaunganishwa nazo.

Wanapaswa kuzijua na ku perfom their national duty. But haziko solid in their hearts. Mapenzi kwa taifa hili yaneshuka kwa kiwango cha ajabu ubinafsi umetamalaki. Umoja wa nchi umepungua. Ili tukue na tujitegemee tunapaswa kuzalisha.

Tunapaswa kuzalisha wenyewe vitu kama silaha, magari, vifaa vya hospitali, mabarabara yetu nk, hatuwezi kusema tunajitegemea kama asilimia 90% tunavyotumia hatujazalishi vinatoka nje. Pesa yote tunayopata tunatoa nje. Inayoingia ndani ni kidogo mno tutakuaje? We import more than we export. We do not work enough.

Bado ukuaji wetu wa kusuasua. Na kwahiyo tutaendelea kuwa soko la mataifa ya nje kwasababu hatuzalishi na hatuna ziada.

Hatuwezi kuongelea uchumi bila ya watu kuzalisha. Watu lazima wazalishe ili tuongelee uchumi, lakini pia ili tujitegemee. Ili tusimame kwa miguu yetu miwili.

Asilimia hamsini sasa hivi ya budget yetu inategemea misaada na mikopo hili ni tatizo. Hatuwezi kupinga wanapotuita sisi ni nchi maskini kwasababu hatuwezi kusimama kwa miguu yetu. Lakini tatizo hili sio kwamba halisuhulishiki, linaweza kutatuliwa. Linahitaji umoja wetu na utayari wetu. Tuna nguvu ya kulitatua. Lakini kwa huku kugawanyika kwetu na kwa kukosa malengo ya pamoja huenda ikawa ndoto.

Sent from my SM-J530F using JamiiForums mobile app
 
Mother Confessor

Mother Confessor

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2016
Messages
12,291
Likes
25,749
Points
280
Mother Confessor

Mother Confessor

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2016
12,291 25,749 280
Ni ndoto kweli kwa nchi kama yetu hii,.sera na mipango ya maendeleo ipo lakini likija suala la utekelezaji kitaifa,kila mtu anageukia sera ya chama/taasisi yake binafsi...
 
Shayu

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Messages
544
Likes
874
Points
180
Shayu

Shayu

Platinum Member
Joined May 24, 2011
544 874 180
Kuna udhaifu mkubwa bado. Tunahitaji kurekebisha baadhi ya mambo na kubadilika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mother Confessor

Mother Confessor

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2016
Messages
12,291
Likes
25,749
Points
280
Mother Confessor

Mother Confessor

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2016
12,291 25,749 280
Kuna udhaifu mkubwa bado. Tunahitaji kurekebisha baadhi ya mambo na kubadilika.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakika,.kama tunahitaji kuendelea kweli kama Taifa,.lazima tuache kuishi kwa mazoea kwenye mambo yenye kuleta tija kwa wananchi na nchi kwa ujumla wake,.
 
Rev. Kishoka

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
4,505
Likes
419
Points
180
Rev. Kishoka

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
4,505 419 180
Shayu,

Naomba nipanue wigo wa mada yako ambayo nafikiri kimtazamo unaendana na mawazo niliyo nayo.

NItajaribu kujenga hoja yangu kwa kuangalia vitu viwili: maendeleo na uchumi.

Watanzania tunaaminishwa kuwa Chama au mwanasiasa atatuletea maendeleo; je maendeleo ni nini? ni kitu gani? na iweje chama cha kisiasa, serikali au mwanasiasa aweze kutuletea maendeleo? je Maendeleo kwa vyama vya siasa, serikali na mwanasiasa ni kitu gani? je kwa mwananchi, maendeleo ni kitu gani?

Juzi akipokea Airbus ya Pili, Rais alisema anataka Tanzania iwe kama Ulaya, akatuhamasisha kuwa Tanzania itakuwa kama ulaya, na zaidi ni msisitizo wake kuwa maendeleo na mabadiliko ya Tanzania yatakayofanyika na yanayofanyika ni kutokana na matakwa yake (si maamuzi ya wengi)!

Je hapo tunafafanuaje maana ya maendeleo? Je maendeleo ni vitu? mfano magari, nyumba, ndege, vivuko, na kadhalika? je leo kila mwananchi tukimpa atupe orodha ya vitu vitano ambavyo atasema ndio muhimu kwa maendeleo yake wote watakuwa na jibu linalofanana?
Mfano: kumletea Mtu maji ya bomba ni maendeleo versus mtu kutembea maili moja kuchota maji mtoni au kisimani? je maji ni maendeleo? je mtu anaelewa umuuhimu wa maji kwa maisha yake? je lishe, afya, usafi na furaha ya moyo? vina sehemu gani kwenye mfumo wa maendeleo wa mtu?

Tuje kwenye uchumi: Viashiria vinavyosemwa na Serikali na hata Chama Tawala ni kuwa Tanzania iko kwenye nchi zenye uchumi wa kati wenye ukuaji wa hali ya juu na tuko karibu kuingia daraja la kati la nzhi zinazoendelea. Je viashiria hivi ni uahlisia wa kweli wa Mtanzania?

Je upimaji wetu wa uchumi wa IMF, WB na bajeti kusema uchumi unakua kwa 7% mwaka huu, unatumia vipimo na viashiria gani? maana kama kimahesabu ya jumla ya GDP na GNP tunaonekana tunaneemeka, lakini Mtanzania anazama kwenye ufukara (not even umasikini), tunawezaje kusema uchumi unakuwa?

Je tunapima uchumi kutumia government purchasing and borrowing powers? what about mwananchi? je pato la mwananchi linaongezeka vipi ikiwa uchumi wa nchi unakuwa? je purchasing power imeongezeka au kuwa stable kwa miaka 5 iliyopita au purchasing power na savings zake zinasuasua?

Je kwa tafsiri zte za kukua kwa uchimi wa tiafa na maendelo, idadi ya wategemezi wa Serikali imepungua? nikiwa na maana watu wenye kutegemea ruzuku, kupata huduma za bure za serikali wenye utegemezi. je idadi ya wanaojitegemea imeongezeka kutokana na kukua huku kwa uchumi na hatua za maendeleo ya Taifa/

Kumradhi kama maoni yangu ni mapana mno au nimetoka nje ya wigo wa hoja yako kuu.
 
Dhana ya maendeleo na uchumi ni vitu viwili vinavyoendana kimsingi. Hakuna maendeleo bila uchumi kukua.Na uchumi ni CAPITAL. Hapa hatuwezi kuzungumzia uchumi bila uzalishaji au kwa maana nyingine kazi zinazopelekea kwenye uzalishaji.

Hakuna chama au mwanasiasa anayeweza kuwaletea maendeleo watu. Watu hujiletea maendeleo wenyewe kwa kujituma na kufanya kazi. Infact serikali haina hela ya kuwaletea wananchi maendeleo wanategemea pesa kutoka kwa wananchi katika mfumo wa kodi. Kufikiri kwamba wao serikali wanaweza kuleta maendeleo bila juhudi za wananchi ni dhana ya kijinga. Kuendeleo kwetu na hata kujitegemea kwetu kunategemea sana wananchi kuliko serikali. Aina ya wananchi taifa iliyonayo ndio ina determine future ya nchi itakuwaje. Serikali ni mratibu tu na kazi ya kiongozi ni kuleta mwamko na kuuza tu maono yake au yao kama chama na kubadili fikra za wananchi, kuweka malengo na dira ambayo wananchi wataifuata lakini perfomance ni ya wananchi wenyewe. Wananchi ndio wanao perfom; ndio watendaji wakuu wa kile ambacho serikali inafikiria kutenda. Na kwakeli kama nchi ikifanikiwa na kuendelea sifa zote hupaswa kurudi kwa wananchi ambao kila siku huhenyeka kwenye kilimo, biashara na kazi nyingine za ukuaji uchumi na serikali huja tu kufuata kodi. Kuendelea kwa nchi kunategemea perfomance ya wananchi katika uzalishaji.
 
Nakubali Tanzania inaweza kuwa kama ulaya na pengine zaidi ya ulaya lakini sio kwa juhudi zake mwenyewe. Anahitaji kujitolea kwa wananchi kufanikisha hilo na pia ili kufanikisha hilo ni lazima kujenga umoja wa nchi, kuua makundi ambayo yapo sasa hivi na kuunda taifa lenye fikra na nia zinazofanana. Hakuna taifa litakaloshindwa kama wakiwa na lugha moja na dhamira moja. Na hata tena malengo ya kitaifa yajulikane kwa watu wote hadi shuleni na wananchi wajuzwe kuhusu utaifa na majukumu yao. Bila utaifa hatuwezi kuendelea...
 
Shayu

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Messages
544
Likes
874
Points
180
Shayu

Shayu

Platinum Member
Joined May 24, 2011
544 874 180
Je hapo tunafafanuaje maana ya maendeleo? Je maendeleo ni vitu? mfano magari, nyumba, ndege, vivuko, na kadhalika? je leo kila mwananchi tukimpa atupe orodha ya vitu vitano ambavyo atasema ndio muhimu kwa maendeleo yake wote watakuwa na jibu linalofanana?
Mfano: kumletea Mtu maji ya bomba ni maendeleo versus mtu kutembea maili moja kuchota maji mtoni au kisimani? je maji ni maendeleo? je mtu anaelewa umuuhimu wa maji kwa maisha yake? je lishe, afya, usafi na furaha ya moyo? vina sehemu gani kwenye mfumo wa maendeleo wa mtu?
Kununua ndege sio maendeleo, kuwa na watu wenye uwezo wa kuunda ndege ni maendeleo. Kununua magari sio maendeleo, kuwa na watu wanaounda magari ni maendeleo, vile vile kwa vivuko nk. Kwahiyo ili tuendelee tunapaswa kuwekeza kwenye skills za watu ili waweze kuunda hivyo vitu. Tukiwa na watu hao tutajiita tumeendelea. Sasa hivi tuna import kila kitu. Nadhani harakati zetu ni muhimu zielekezwa huko.

Maendeleo ya watu lazima yaletwe na watu wenyewe. Na ukuaji na maendelea ya nchi huenda sambamba na ukuaji wa kiakili wa wananchi wa nchi husika. Maendeleo ya binadamu is just nothing but uvumbuzi wake. Na wale waliogondua zaidi waliendelea zaidi na ku conquer other nations. We are small because of that.
 
Shayu

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Messages
544
Likes
874
Points
180
Shayu

Shayu

Platinum Member
Joined May 24, 2011
544 874 180
Mfano: kumletea Mtu maji ya bomba ni maendeleo versus mtu kutembea maili moja kuchota maji mtoni au kisimani? je maji ni maendeleo? je mtu anaelewa umuuhimu wa maji kwa maisha yake? je lishe, afya, usafi na furaha ya moyo? vina sehemu gani kwenye mfumo wa maendeleo wa mtu?
Hili linaweza kuwa sio maendeleo na linaweza kuwa maendeleo. Kumletea mtu maji ni kumuondolea tabu yake. Hayo yote lishe, afya, usafi na furaha ya moyo ni mambo ambayo hufanya maisha kuwa yenye unafuu. Ni zao la uwezo wa akili ya binadamu kutawala mazingira yake kwa kutumia maarifa na akili.
 
Shayu

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Messages
544
Likes
874
Points
180
Shayu

Shayu

Platinum Member
Joined May 24, 2011
544 874 180
Je upimaji wetu wa uchumi wa IMF, WB na bajeti kusema uchumi unakua kwa 7% mwaka huu, unatumia vipimo na viashiria gani? maana kama kimahesabu ya jumla ya GDP na GNP tunaonekana tunaneemeka, lakini Mtanzania anazama kwenye ufukara (not even umasikini), tunawezaje kusema uchumi unakuwa?
Sikubaliani sana na vipimo vyao. kwasababu wanasema tunakua kiuchumi wakati kujitegemea kwetu bado ni kudogo.
 
Shayu

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Messages
544
Likes
874
Points
180
Shayu

Shayu

Platinum Member
Joined May 24, 2011
544 874 180
e kwa tafsiri zte za kukua kwa uchimi wa tiafa na maendelo, idadi ya wategemezi wa Serikali imepungua? nikiwa na maana watu wenye kutegemea ruzuku, kupata huduma za bure za serikali wenye utegemezi. je idadi ya wanaojitegemea imeongezeka kutokana na kukua huku kwa uchumi na hatua za maendeleo ya Taifa/
Hii inategemea ukubwa wa uzalishaji na utoaji huduma/ kiwango cha pesa au pato taifa inaloingiza. Watu kujitegemea inategemea na hili pia. Serikali haiwezi kuhudumia watu vyema kama pato lake ni dogo. Ajira mpya hutegemea uzalishaji, na uwepo wa ajira mpya hupunguza wategemezi. Na hii yote hutegemea watu wangapi wenye uwezo na akili ya kufanya kazi wanatimiza wajibu wao. Kwasababu sio serikali peke yake inawajibika kutoa ajira. Sisi pia wenye uwezo wa akili na nguvu ya kufanya kazi tunawajibika kutoa ajira kwa wengine.
 
Shayu

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Messages
544
Likes
874
Points
180
Shayu

Shayu

Platinum Member
Joined May 24, 2011
544 874 180
Tuje kwenye uchumi: Viashiria vinavyosemwa na Serikali na hata Chama Tawala ni kuwa Tanzania iko kwenye nchi zenye uchumi wa kati wenye ukuaji wa hali ya juu na tuko karibu kuingia daraja la kati la nzhi zinazoendelea. Je viashiria hivi ni uahlisia wa kweli wa Mtanzania?
Kama nilivyosema mwanzo kuendelea kwa taifa ni kujitegemea kwake, kama chochote tunachofanya hakitupelekei kwenye kujitegemea kwetu, hayo sio maendeleo.

Hatuko kama taifa kunywa na kula mkate tu. Tunahitaji kuheshimiwa na kuheshimiwa kwetu ni kujitegemea kwetu. Tunahitaji kuonyesha wengine tuna brain kama wao walivyo na brain.

nadhani nimejibu baadhi ya hoja zako.
 
hearly

hearly

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2014
Messages
22,609
Likes
29,437
Points
280
hearly

hearly

JF-Expert Member
Joined Jun 19, 2014
22,609 29,437 280
Dhana ya maendeleo na uchumi ni vitu viwili vinavyoendana kimsingi. Hakuna maendeleo bila uchumi kukua.Na uchumi ni CAPITAL. Hapa hatuwezi kuzungumzia uchumi bila uzalishaji au kwa maana nyingine kazi zinazopelekea kwenye uzalishaji.

Hakuna chama au mwanasiasa anayeweza kuwaletea maendeleo watu. Watu hujiletea maendeleo wenyewe kwa kujituma na kufanya kazi. Infact serikali haina hela ya kuwaletea wananchi maendeleo wanategemea pesa kutoka kwa wananchi katika mfumo wa kodi. Kufikiri kwamba wao serikali wanaweza kuleta maendeleo bila juhudi za wananchi ni dhana ya kijinga. Kuendeleo kwetu na hata kujitegemea kwetu kunategemea sana wananchi kuliko serikali. Aina ya wananchi taifa iliyonayo ndio ina determine future ya nchi itakuwaje. Serikali ni mratibu tu na kazi ya kiongozi ni kuleta mwamko na kuuza tu maono yake au yao kama chama na kubadili fikra za wananchi, kuweka malengo na dira ambayo wananchi wataifuata lakini perfomance ni ya wananchi wenyewe. Wananchi ndio wanao perfom; ndio watendaji wakuu wa kile ambacho serikali inafikiria kutenda. Na kwakeli kama nchi ikifanikiwa na kuendelea sifa zote hupaswa kurudi kwa wananchi ambao kila siku huhenyeka kwenye kilimo, biashara na kazi nyingine za ukuaji uchumi na serikali huja tu kufuata kodi. Kuendelea kwa nchi kunategemea perfomance ya wananchi katika uzalishaji.
Hili bandiko lako linaturejesha kule kule kwenye hoja elekezi iliyopo kwenye mada yako ", inayosema tunahitaji taifa lenye watu wenye skills taifa lenye watu wazalishaji zaidi kuliko wanunuzi wa rasilimali zitokazo nje "..... Nashukuru

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Forum statistics

Threads 1,250,892
Members 481,523
Posts 29,749,792