Dhana ya mabadiliko

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Unapodai mabadiliko katika nchi , wewe kwanza umebadilika ?. Je unatabia ambazo zina reflect raia anayewajibika na mwema? Hili ni swali ambalo wote tunapaswa kujiuliza, tunaopenda na kuhitaji mabadiliko katika serikali yetu na katika nchi.


Kwa sababu swali hili litakuwa ndio msingi wa mabadiliko makubwa zaidi katika nchi yetu na katika jamii yetu.


Naamini mabadiliko huanza na mtu binafsi kwa kubadili mtazamo wake . Huwezi kubadili jamii yako kama mtazamo wako mwenyewe haujabadilika. Ili ubadili nchi ni lazima wewe mwenyewe ubadilike.


Changamoto ambazo zinatukabili kama taifa na katika jamii yetu zitabadilika tu kama tutabadili mtazamo wetu ambao ndio msingi wa tabia zetu na matendo yetu.


Kama hutendi haki ukiwa raia wa kawaida huwezi kutenda haki ukiwa kiongozi. Viongozi wanatoka miongoni mwetu na ili tupate viongozi bora ni lazima sisi wenywe tutambue changamoto zetu na tubadilike.


Kuna tabia ambazo ni vikwazo kwa maendeleo yetu ni lazima tuzijue na tuwe tayari kukabiliana nazo katika ngazi ya chini. Lakini kuna tabia ambazo ni vikwazo kwa mahusiano yetu nazo lazima tuzijue. Kwasababu hatuwezi kuendelea kama hatuna mashirikiano mazuri.


Tunapodai mabadiliko katika nchi ni lazima kwanza tujiangalie wenyewe. Na kuona ni vitu gani ambavyo wewe binafsi unapaswa kubadilika uwe raia bora na anayewajibika kwa taifa lake, jamii yake na familia yake lakini pia mwenye mahusiano mazuri na wengine.Halafu baadae ndio tuiangalie serikali na kuinyooshea kidole. Kisha tuiambie serikali wewe huwajibiki umeshindwa !


Maisha yako yamejaa utapeli na wizi na wewe unasema unataka mabadiliko ni yapi hayo? UNAVUTA BHANGI, UNAJIUZA NA KULA UNGA. Hufikirii kwanza unahitaji kubadilika wewe kwanza.


Angalia kwenye familia yako ni nini hakiko sawa ? Angalia mahusiano yako na majirani zako badilisha huko kwanza. Alafu iambie serikali wewe serikali hufanyi kazi sawa sawa.


Katika nchi yeyote raia wana haki na wajibu. Unapaswa kutimiza wajibu wako kwanza kabla ya kudai haki. Lazima kuwe na balance ya vitu hivi viwili.


Kama tunataka kubadili taifa hili kwanza tuanze ngazi ya mtu binafsi tubadilike.

Swali la kujiuliza tunalalamika kila siku kuhusu ufisadi lakini ufisadi unaanza katika ngazi ya tabia ya mtu binafsi na mahusiano yake na wengine. Uchoyo, ubinafsi na kujiangalia mwenyewe badala ya jamii na taifa.
Kwahiyo kama tunataka mabadiliko hii isiwe katika serikali peke yake lakini ziwe ni harakati za kubadili mtazamo wa jamii nzima. Na kujenga upya mahusiano yetu kama taifa.

There will be no significant change kama watu wenyewe kwa ujumla wake kama hawatobadilika na kama hawatajitambua kuhusu utaifa wao. SO WE MUST RAISE CONSCIOUSNESS ya watu kujitambua kuhusu utaifa kinyume na ubinafsi. Ni lazima tuangaliane kama watu wa taifa moja ambao wana malengo ya pamoja na watu wetu wawe tayari ku sacrifice sehemu ya maisha yao kwaajili ya utaifa na maendeleo ya taifa kwa upana wake.
 
Somo gumu sana hili mkuu, hongera kwa kulianzisha

Nina jamaa ninawafahamu kwa asilimia 92, walikuwa ni wafuasi wa mabadiliko ila nyumba zao, magari yao na maisha yao ni full ufisadi!

wengi wahubiri wa mabadiliko ni wapigaji tu

wengi walioko CCM, CDM ni wezi kabisa wala hawafai
 
Back
Top Bottom