JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,114
- 3,541
Salamu wanajamvi!
Tatizo la nchi yetu kiuchumi ni kubwa kuliko wengi wetu tunavyo dhani.Uchumi wa nchi yetu kila wakati unakutana na dhoruba kali labda kwasababu wachumi wetu mahali fulani wanakosea kufikiri vizuri.
Hivi unawezaje kupanga bei elekezi ya bidhaa fulani bila kujiridhisha kwa hakika kama uzalishaji na upatikanaji wa bidhaa husika sokoni uko vizuri?Leo hii bei ya sukari katika baadhi ya maeneo imefika tshs 3000/ kwa kilo moja yaani shs 1200 zaidi ya bei elekezi.
Kulinda viwanda vya ndani wakati uzalishaji wake wa bidhaa ni hafifu ni kurudisha nyuma maendeleo.Wazo hili linatoka wapi? mbona viwanda vingine vya ndani havilidwi dhidi ya bidhaa kutoka nje?Viwanda vya sabuni, mafuta ya kupikia, viwanda vya nguo nk mbona viliachwa kupambana na nguvu ya soko bila kulindwa na serikali? Inakuwaje leo serikali inaturudisha nyuma kewa kisingizio cha kulinda viwanda vya ndani?
Marekani ina viwanda vya kila aina ya bidhaa lakini hawajawahi kuzuia bidhaa zenye ubora unao hitajika kuingia ndani ya marekani kwa kisingizio cha kulinda viwanda vya ndani.Nchi yeyu inapakana na nchi nyingi zinazo zalisha sukari na kama wafanya biashara wangeruhusiwa kuingiza bidhaa hii kutoka katika nchi hizi nauhakika bei ya sukari ingekuwa shs 1200 tu.