Dhana ya kifo na wosia

Dhana ya kifo na wosia

Kimsingi, wasia ni mwendelezo wa nia ya mtu aliyehai hata baada ya kufa kwake, na ndiyo njia pekee ya kuhakikisha kuwa nia na makusudio ya mtu yanahifadhika. Kuandika wasia si kujitabiria kifo, bali ni kuchukua tahadhari ya amana ns haki. kwani hakuna ajuae atakufa katika mazingira gani.
Amana na haki nyingi za watu zimepotea kwa sababu ya vifo vya ghafla na vifo vya ajali kwani wahusika hawakuweka uwezekano kuwa wangefariki dunia katika mazingira hayo.
 
Wosia sio kifo ila iwe siri kwani kama umeandika kwa mtoto wako unaempenda ,, mama akijua unaweza kupigwa chini kiaina ili apete na mwanae
 
Wosia si mpaka uone unakaribia kufa, mtu yeyote age 18+ anayemiliki mali anaweza andika wosia namna mali zake zitumike au zigawanywe mara tu akifa.
Ni jambo jema kuandika wosia, japo si lazima.
Hivyo wosia sio kujikatia tamaa bali ni kujali ulichonacho
 
Hebu fikiria kuwa siku haupo watoto wako wakaanza kuuana kwa kugombania urithi, unajisikiaje?
 
Umeanza vizuri kuwa "tumezaliwa na tutakufa" ila ukamalizia vibaya na hoja za uchuro.

Ni busara binadamu yeyote kupanga jinsi utakavyotaka urithi wako utumike kwa manufaa na malengo mahsusi pindi unapokufa. Haina maana kuwa wasia ni kiashiria cha kifo.

Wapo wengi tu waliandika wosia na badae walioandikwa kwenye wosia kama wanufaika au wasimamizi wakafa kabla ya muandika wosia.

Wosia ni njia nzuri ya kuendeleza malengo au ndoto zako pindi ufapo. Mfano Marehemu Nobel, alitaka pesa yake itumike kuwa zawadia wanaofanya mema duniani ndio maana tuna tuzo kuu ya NOBEL PRIZE.
mkuu respect....hivi una kamfano kidogo kuhs mtu alieandika wosia then hakufa , matokeo yake alowaandikia wakamtangulia ?
 
wengi mmejibu kwenye faida za wosia.

yeye kauliza kuna uhusiano gani kati ya wosia na kufariki kwa mtu siku chache tu baada ya kutoa wosia.

me mwenyewe nasubiri jibu, mana nimeshughudia wazee wengi siku chache tu baada ya kutoa wosia walifariki.
umenipata vyema mkuu
 
Uhusiano wa kuacha wosia na kufa ni vile mtu huona kile anachokiacha kitaleta mtafaruku hivo hueka ushahid wake wa mgawo wamali zake kiuandishi au vyovyote aonavyo inafaa


Au huamua tu kua mali zake zitumike vipi, nimeshuhudia cases nyingi sana za namna hii

Anko wangu ameshagawa mali zake japo yu hai ana haumwi hata kope na amesema miongoni mwa mali zingine zigawiwe mayatima na mskitini zitolewe kama waqfu tunangoja tu ahad ifike maneno yafanye kazi

Kufa kupo hakukimbiliki haijalishi umeandika au la

Na asilimia kubwa ya wanaoacha wosia ni wale familia zao zina mikanganyiko mingi sana
thanks kwa majibu murua
 
Back
Top Bottom