Dhana ya gari automatic hazifai kwa biashara ya kubebea mizigo

jacquejaytee

Member
Jan 20, 2014
44
24
Wakuu habari ya leo,

Kuna dhana kuwa gari za kubebea mizigo kama kirikuu na zile mini canter hazitakiwi ziwe automatic,ni lazima ziwe manual.

Hii ikoje kitaalam na je ni kweli magari ya automatic hayawezi biashara ya kubeba mizigo?
 
Ni bora umpe dereva dala dala ya Auto akuletee elfu 90 kuliko umpe dala dala ya manual akuletee laki. Madereva wengi wanatumia gia kubwa sehemu ambayo alitakiwa atumie gear ndogo hivyo kuichosha engine mapema. Kwenye auto, hawezi kufanya hivyo. Hii hupelekea gari kudumu zaidi.
 
Sina uzoefu sana ila kuna fundi aliniambia Automatic gear box inahitaji umakini sana tofauti na hizi manual hasa kama unapanda milima mara kwa mara
 
Shida kubwa ni madereva na wala sio gear box automatic.

Automatic zipo kwenye dumper za migodini za tani 100,hadi 150 sasa kirikuu au canter itakuwaje haifai?.
Watu wamezoea gari za kulazimisha gia hilo ndio tatizo.

Na automatic ukiijulia wala haina tatizo ni gari nzuri tuu.

Hakikisha throttle pedal unaikañyaga taratibu kama hautaki utaona gari inavyobadilisha gia kwa rotation kati ya 1200/1400 hapo gari yako utaiona ilivyonyepesi na hats unywaji wa MAFUTA unakuwa mzuri kabisa.
 
Wakuu habari ya leo,

Kuna dhana kuwa gari za kubebea mizigo kama kirikuu na zile mini canter hazitakiwi ziwe automatic,ni lazima ziwe manual.

Hii ikoje kitaalam na je ni kweli magari ya automatic hayawezi biashara ya kubeba mizigo?

Zipo gari automatic za kubebea mizigo lakini gearbox zake si kama hizi za automatic nyingi unazoziona kwenye gari ndogo.
 
Hayo maneno ya vijiweni achana nayo. Siku hizi gari nyingi kubwa zinakuja na mfumo wa automatic transmission kwa ajili ya kumpunguzia dereva uchovu na kuongeza ufanisi wa gari.

Scania, Man Diesel, Mercedes Benz za kubeba tani zaidi ya 30 ni automatic.
Gearbox za automatic zina makundi zaidi ya 10

Zipo ambazo haizfai kwa kubebea mizigo na zipo ambazo zinafaa.
 
Shida kubwa ni madereva na wala sio gear box automatic.

Automatic zipo kwenye dumper za migodini za tani 100,hadi 150 sasa kirikuu au canter itakuwaje haifai?.
Watu wamezoea gari za kulazimisha gia hilo ndio tatizo.

Na automatic ukiijulia wala haina tatizo ni gari nzuri tuu.

Hakikisha throttle pedal unaikañyaga taratibu kama hautaki utaona gari inavyobadilisha gia kwa rotation kati ya 1200/1400 hapo gari yako utaiona ilivyonyepesi na hats unywaji wa MAFUTA unakuwa mzuri kabisa.
automatic za magari makubwa na mitambo ni tofauti ki mfumo. na za gari ndogo.
kwenye gati ndogo zinatumia fluid (torque converter ) kweye magari makubwa zinatumia dry clutch
 
Ni kweli mkuu hilo , gear box ya Scania opticruise kuna pedal ya clutch na unaitumià kuondoka Na kusimama tuu, ila kwa zile za zf as tronic Kama za iveco na daf cf hizo HAZINA kabisa pedal za clutch, tukija kwenye actors power shift clutch unatumia juu kweñye gear lever.
 
Ni bora umpe dereva dala dala ya Auto akuletee elfu 90 kuliko umpe dala dala ya manual akuletee laki. Madereva wengi wanatumia gia kubwa sehemu ambayo alitakiwa atumie gear ndogo hivyo kuichosha engine mapema. Kwenye auto, hawezi kufanya hivyo. Hii hupelekea gari kudumu zaidi.
Sijaona Dereva wa daladala anayetumia gear namba 1 yaaani hawa jamaa Kwenye kusimama ni namba 2 Kwenye kutoka ataingiza namba 2 Kwa kifupi wako hivyo pia kuondoka na Gia kubwa inatokana na uchakavu wa engine hasa diesel engines zinakuwa nzito Sana kuchanganya ndiyo maana madereva wa daladala wanagonga Gia namba 2..
 
Asikwambie mtu gari ya kazi ni manual. Hizi auto zinasumbua sana. Mwaka 2014 niliwahi kununua Mitsubishi Canter automatic baada ya mwaka nilibadili gear box nikaweka manual transmission na gari mpaka leo inapiga mzigo bila shida
 
Back
Top Bottom