Nina gari mitsubishi canter tani 3.5. natafuta kazi ya kubeba mizigo

Jul 7, 2013
12
15
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Mimi nipo Dar es salaam, nina gari canter, box body freezer, yenye uwezo wa kubeba mizigo ya baridi na ya kawaida.

Natafuta kazi halali popote hapa Tanzania bara iwe ya tender au trip za kawaida za kupakia mizigo. Yoyote anaefahamu chimbo ambalo lina mzunguko wa kazi naomba tufahimishane.

Gari ni nzima ya uhakika. Nitashukuru sana tukiweza kupeana michongo ya kazi.
 
Nina kazi yakusambaza bidhaa za madukani kama sukari,unga,mafuta nk.

Kama utaiweza nicheki
 
Nenda ferry kuna kazi ya kubeba Ice cubes na kuzipeleka pale.

Kama gari ipo vizuri nenda Tanga mjini au Pangani kuna kazi ya kubeba samaki kupeleka Muheza,Korogwe,Mombo mpaka Arusha. Mbeya kuna deals za kubeba samaki Rukwa kwenda Mbeya mjini wanatumia Pick up
 
Asante sana wakuu kwa hizo connection. Nakaribisha maoni zaidi ili iwe faida kwa wengine pia. And then itakuwa rahisi mtu kufanya choice wapi aende akafanye kazi. Asanteni
 
Nenda ferry kuna kazi ya kubeba Ice cubes na kuzipeleka pale.

Kama gari ipo vizuri nenda Tanga mjini au Pangani kuna kazi ya kubeba samaki kupeleka Muheza,Korogwe,Mombo mpaka Arusha. Mbeya kuna deals za kubeba samaki Rukwa kwenda Mbeya mjini wanatumia Pick up
Hii imekaaje huku, naomba unielekeze vizuri.
 
Back
Top Bottom