Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,653
Leo ningependa tujiulize wote kwa pamoja ni nini haswa maana ya elimu ? Tujiulize, tutafakari, tujaribu kupata majibu, ni nini haswa maana ya elimu? Na kwanini watu wanapelekwa shule ? Na kwanini tunaamua kupeleka shule watoto wetu? Na ni kwanini taifa hupeleka watu wake shule.
Ni nini maana ya elimu?
pengine tunaweza kufikiri elimu ni maarifa kazi peke yake ambayo yatatupatia kipato. Lakini elimu ni zaidi ya hapo tulipozoea. Ya kwamba tunaenda shule kusudi tupate kazi kusudi tupate pesa kwaajili ya matumizi yetu ya kila siku.
Elimu ni ukuzaji wa ufahamu za binadamu (enlightment ). Ukuzaji wa ufahamu huu ambao unapaswa kumpelekea binadamu na kumfanya binadamu kutenda katika usahihi , ili kumfanya binadamu awe binadamu bora zaidi na mwenye kuzalisha na mwenye faida kwake binafsi kwa taifa lake na kwa familia yake.
Aweze kuangalia familia vizuri na ku manage familia yake vizuri. awe na mahusiano mazuri na jamii inayomzunguka na awe pia na mahusiano mazuri na taifa lake na aweze kuwa mtu bora na mzalishaji kwa taifa lake. Ndio msingi wa elimu.
Elimu sio skills za kazi peke yake. Lakini ukaacha mambo mengine ya msingi anbayo ni kukuza ufahamu wa binadamu ( Elinlightment) ya akili ya binadamu. Ili aweze ku act katika usahihi.
Aweze awe na uwezo wa kuchanganua kati ya sahihi na potofu na aweze kufuata jambo ambalo ni sahihi. Mtu huyu ni mtu ambaye mwenye elimu. Mwenye uwezo wa kufahamu na kuchanganua mambo na kutenda katika usahihi.
Mwenye uwezo wa ku manage familia yake vizuri, mwenye uwezo wa kuwa na mahusiano mazuri na jamii inayomzunguka, mwenye uwezo wa kuwa raia bora na mtu bora ambaye anazalisha katika taifa lake.
Hatuwezi kuwapa watu elimu bila kuangalia tabia za watu wetu. Ni muhimu elimu yetu pamoja na kuangalia skills za kazi za watu wetu lakini ijenge tabia zao. Ili ziwe na manufaa kwa taifa sio hasara. Kama tunawapa skills za kazi watu wetu lakini wanakuwa hawana manufaa kwa taifa letu basi hiyo elimu ina kasoro iangaliwe upya.
Elimu bora ni ile inayomfanya mtu kutenda katika usahihi. Ni elimu ambayo sisi kama taifa tunapaswa kuijenga. Na watoto wetu watakuwa wenye akili kama wakipata elimu kama hiyo. Ni elimu ambayo itawalinda dhidi ya maangamizi, itawalinda dhidi ya uovu.. Lakini pia itawapa skills za kazi.
Kwahiyo tukitengeneza watu kama hao tutapata viongozi wazuri, tutapata watu wenye skills mbalimbali wazuri lakini pia waaminifu na wenye maadili na nidhamu ya kutosha.
Vinginevyo elimu ambayo unampa tu mtu skills za kazi pasipo mambo mengine yaliyojazia hapo ni sawasawa na kutwanga maji kwenye kinu. Elimu bila maadili ni sawasawa na mtu bila kingo. Haitokuwa na faida. Itakufa tu.
Maana ya elimu ni kuondokana na matendo ya kijinga yasiyo na faida. Dhana ya elimu ni kuondokana na ujinga. Na tunapima faida ya kitu kutokana na matokeo ya kila matendo tunayofanya. Ili twende mbele kama taifa lazima tuelimike. Tuachane na ujinga na tutende katika usahihi.
Kwahiyo ni uhimu sana tunapowapa skills za kazi na tunapotoa elimu kuangalia tabia na dihamu za watu wetu. Nidhamu huleta mwelekeo iwe kwa taifa au kwa mtu binafsi.