PhD zingine zina kwashikor au Stunted na wasting ndani ya siku 1000 za utotoni. Ukizingatia alizaliwa huko milimani,naogopa kama alipata lishe boreAiseeee!!!
Baada ya kujua kuwa Mkuu anapenda PhD,naona umeamua kutafuta fursa avae. PhD za kujitoa akili na kulamba viatu.
Mei mosi ni siku ya wafanyakazi. Kueleza shida,changamoto,mafanikio,maombi,mapendekezo na mustakabali wa wafanyakazi ni dhambi!? Je kuongelea mafanikio ya serikali yasiyohusiana na siku hii ndio halali!? Kuongelea mambo ya chama/vyama siku hii ni sahihi!?
Kwanza hiyo PhD yake ni ya nini? Elim duniani au elim akhera? He seems punguani!Ukimsomaga huko FB utadhani sio msomi, nilipoona jina Yahaya Msangi, my mind told me this, "this guy is not new to you" ndio sasa nimemkumbuka. Anyway, nadhani kwasasa kwa Africa hakuna kazi inalipa kama kazi za siasa; yaani sio udaktari, uinjinia, uwana sharia nk, siasa in Africa ndio mambo yote na ni kazi ambayo hata mjinga anaifanya bila shida yoyote.
Huu ndio ukweli....TUBADILIKETUCTA zile hotuba za kudai nyongeza MEI MOSI achaneni nazo. Sasa zama nyingine. Msiimbe kaswida kilabuni! Msiimbe kwaya sokoni! Hailipi tena siku hizi.
Halafu kichekesho ni watu walewale wanaodai hawana ajira ndio wanaolalamika mshahara kutoongezwa!! Walau kwa sasa tuitumie MEI MOSI kudai ongezeko LA nafasi za ajira (employment creation), hifadhi ya jamii (social protection for all), ajira bora na zenye utu (decent work) na ajira zinazojali mazingira (green jobs).