Dhamira yangu Kisiasa Ndani ya Chama Changu CHADEMA!

Dhamira yangu Kisiasa Ndani ya Chama Changu CHADEMA!

Huna kazi ya kufanya wewe...

Mtu mwenye kazi ya kufanya hawezi kuwekeza maisha yake kwenye siasa magumashi za Chadema. Huna tofauti na kijana Ben Saanane aliyewadiasppoint wazazi wake waliomsomesha kwa gharama kubwa...
Kama sina kazi ya kufanya kama ambavyo tunajua kwamba sasa tatizo la ukosefu wa ajira ni tatizo pana! unadhani ni nani wa kwanza anaepaswa kulaumiwa kama si serikali ya CCM! je! Wewe umeshafanya jitihada kiasi gani kuhakikisha unatusaidia watu tusio na kazi za kufanya kama sisi ! "Mnafiki wewe ling'oe kwanza hilo boriti katika jicho lako ndipo utakapokiona vyema kile kibanzi katika jicho la mwenzako" (mt........):doh: Na Ben Saanane anaingia je hapa sasa! inaonekana unamgwaya sana huyu jamaa ndio maana unamtajataja hata sehemu asipohusika.
 
Last edited by a moderator:
Mshafanya tafiti kujua ni wanachama wangapi wataichagua cdm au na wewe unakurupuka tu bila tafiti yoyote et cdm watachukua nchi....
Umeelewa mada mkuu! yaani sijui unachounga mkono hapa ni nini na unachopinga ni nini! haudhani kama wewe ni mtu unaye sutana na nafsi yako mwenyewe?
 
Mkuu na mimi nipo kuichangia Chadema kwa taaluma yangu na uzoefu wangu kwenye kufanikisha sera zao na kuwasaidia angalau hata kwa kuwakosoa. Hususani hapo watakopolewa madaraka na kwenda kinyume na matarajio ya wananchi.

Wana faida moja kubwa; kuna kiwango duni cha kisiasa kilichowekwa na CCM; pia kuna kiwango duni cha utendaji wa serikali inayoongozwa na CCM hatuwatarajii washuke au wawe sawa na kiwango hicho.

Wajue kuwa sisi wengiine tutawalinganisha kwa mbadala wa klisiasa za kidemokrasia na utendaji makini ambao wametuaminisha tofauti na kukatishwa tamaa na CCM.

Hadi sasa wamejitosheleza kwa umakini.

I am a proud M&E global consultant in the Communications and Transport Sectors. Right now I am on a project with The World Bank in Africa.

Mkuu Mimibaba vita ya Kagera si tuliipigana wote Kamanda ?
I am proud to here now your rocking in that Direction
 
Last edited by a moderator:
Mbona umeanza kujihami wakati hata sijasoma pumba zenyewe?
Nasikia sasa hivi lumumba wanalipa 10,00tshs tofauti na 7,00tsh za hapo awali! hili ni kweli? wewe kwa maoni yako kulikuwa na haja ya ongezeko hilo?
 
betlehem
Katika point yako ya kwanza kama ulivyosema utawashauri viongozi wako wakichukua nchi wafanye mambo mazuri na kuachana na siasa za mipasho. Mimi ningekushauri uanze kazi hiyo mapema sana na uwashauri viongozi wako waachane na siasa ulizoziita za 'MIPASHO'. Katika wakati wangu wa uhai tangu kuanzishwa vyama vya upinzani hapa Tanzania, sijawahi ona siasa za mipasho kama inavyoendelea katika kipindi hiki. Pia ni matumaini yangu hilo umeliona na ndio maana hisia za ushauri zimekujia haraka. Anza hilo mapema kwakuwa mnaowakati mrefu tu wa kurekebisha mambo. Ila matumaini yako 2015, lol! Umejipata matumaini mfu hataivo ni haki yako.

Pia Hilo maamuzi bila utafiti ni sawa kabisa na pia anza nalo mapema pia. Kwani hata hapo kilipochama chenu kina maamuzi ambayo yakitolewa bila utafiti maisha ya mtanzania kwa namna moja au nyingine yanaathirika. Mfano kugomea miswada mbalimbali bungeni na kupelekea kupitishwa bila hata kuangaliwa madhaifu na uthabiti wake ambapo jambo hili wanalifanya mara nyingi kwa ufasaha upinzani.
 
Last edited by a moderator:
betlehem
Katika point yako ya kwanza kama ulivyosema utawashauri viongozi wako wakichukua nchi wafanye mambo mazuri na kuachana na siasa za mipasho.
Dah! mkuu; umeamua uyapindue maneno yangu juu chini tena bila ya woga wowote licha ya kuwa unajua na unajua wazi kuwa watu wote wanaona na wataendelea kuona nilichoandika! Dar kweli ninyi wenzetu mmebalilika nafsi mpaka rohu zenu. Yaani hata chembe ya aibu!
Mimi ningekushauri uanze kazi hiyo mapema sana na uwashauri viongozi wako waachane na siasa ulizoziita za 'MIPASHO'.
Juzi kulikuwa na mjadala juu ya mswaada wa katiba mpya. Wakati akichangia mjadala huo; Hamisi Kigwangala (CCM), alichochangia alisema Mbowe anatembea kama Bibi harusi hakugusia kabisa mswa mpaka anamaliza mchango wake.Je wewe unavyojua; Kigwangala ni CHADEMA?Lusinde alitumia muda wake mwingi kueleza ni kwa jinsi gani yeye alivyo mwanasiasa mkubwa na wa kuheshimika.Hivi huyu naye CHADEMA?
Katika wakati wangu wa uhai tangu kuanzishwa vyama vya upinzani hapa Tanzania, sijawahi ona siasa za mipasho kama inavyoendelea katika kipindi hiki.
Mimi nimetoa mifano; sasa na wewe hebu toa mifano ili hoja yako iwe ya kweli.
Pia ni matumaini yangu hilo umeliona na ndio maana hisia za ushauri zimekujia haraka. Anza hilo mapema kwakuwa mnaowakati mrefu tu wa kurekebisha mambo. Ila matumaini yako 2015, lol! Umejipata matumaini mfu hataivo ni haki yako.
Unajua maana ya mipasho? Huhisi kwamba hiki ulichoandika hapa ndio mipasho yenyewe ninayozungumzia! hebu soma tena uzi kama hujaelewa.

Pia Hilo maamuzi bila utafiti ni sawa kabisa na pia anza nalo mapema pia. Kwani hata hapo kilipochama chenu kina maamuzi ambayo yakitolewa bila utafiti maisha ya mtanzania kwa namna moja au nyingine yanaathirika. Mfano kugomea miswada mbalimbali bungeni na kupelekea kupitishwa bila hata kuangaliwa madhaifu na uthabiti wake ambapo jambo hili wanalifanya mara nyingi kwa ufasaha upinzani
Unaongea hoja nzuri ila kwa staili ya kejeli ila kwa kuwa tunafahamu dhamira yenu katika nchi hii; hatushangai pale mnapoamua kuikwamisha mipango yote yenye nia njema kwa taifa hili.Siku moja huenda mkauona ukweli na kuamua kuufuata.
 
Hata hao viongozi walio vuruga vyama vya upinzani kama Marando wanafanya watu wakose imani
 
betlehem
Dah! mkuu; umeamua uyapindue maneno yangu juu chini tena bila ya woga wowote licha ya kuwa unajua na unajua wazi kuwa watu wote wanaona na wataendelea kuona nilichoandika! Dar kweli ninyi wenzetu mmebalilika nafsi mpaka rohu zenu. Yaani hata chembe ya aibu!

Hapo nimepindua nini mimi?.
By Juzi kulikuwa na mjadala juu ya mswaada wa katiba mpya. Wakati akichangia mjadala huo; Hamisi Kigwangala (CCM), alichochangia alisema Mbowe anatembea kama Bibi harusi hakugusia kabisa mswa mpaka anamaliza mchango wake.Je wewe unavyojua; Kigwangala ni CHADEMA?Lusinde alitumia muda wake mwingi kueleza ni kwa jinsi gani yeye alivyo mwanasiasa mkubwa na wa kuheshimika.Hivi huyu naye CHADEM

Mimi nimetoa mifano; sasa na wewe hebu toa mifano ili hoja yako iwe ya kweli. Unajua maana ya mipasho? Huhisi kwamba hiki ulichoandika hapa ndio mipasho yenyewe ninayozungumzia! hebu soma tena uzi kama hujaelewa.

Unaongea hoja nzuri ila kwa staili ya kejeli ila kwa kuwa tunafahamu dhamira yenu katika nchi hii; hatushangai pale mnapoamua kuikwamisha mipango yote yenye nia njema kwa taifa hili.Siku moja huenda mkauona ukweli na kuamua kuufuata.

Tatizo vijana wengi wa chadewa mmekaa kimabishana.
 
Tatizo vijana wengi wa chadewa mmekaa kimabishana.
Basi samahani kama nimekukwaza.Basi mifano niliyoitoa ya Kigwangala na mwenzake tujifanye kama hatujaiona ili tusikwazane.Any way tu assume kwamba waliongea facts. Hapo natumai utakuwa umeridhika sasa.Halafu japo hatuna vielelzo sehemu ambayo chadema wamekuwa wakifanya ngonjera kama wenzao; basi tuwalaumu tu hivyo hivyo na kuwakatisha tamaa ili watutambue sisi nani. Nadhani hapo tutaenda vyema. sijui unasema je!
 
Mkuu nakutakia kila la heri na labda nikuhakikishie kwamba CHADEMA hawajawahi kupuuza hoja za maana hata mara moja , tanganyika itajengwa na wenye moyo .
 
Hongera sana mkuu betlehem kwa dhamira yako hiyo safi yenye lengo la kusaidia wengi. Tutakupa tu ushauri kwa kadri tutakavyokuwa tunapata mawazo mapya. Hayo uliyosema unaanza nayo kwa sasa ni mazito na ya muhimu mno. La msingi usije ukakata tamaa kabla hujakamilisha hayo uliyoyapanga kuyafanyia kazi.
 
Last edited by a moderator:
Katika point yako ya kwanza kama ulivyosema utawashauri viongozi wako wakichukua nchi wafanye mambo mazuri na kuachana na siasa za mipasho.
Dah! mkuu; umeamua uyapindue maneno yangu juu chini tena bila ya woga wowote licha ya kuwa unajua na unajua wazi kuwa watu wote wanaona na wataendelea kuona nilichoandika! Dar kweli ninyi wenzetu mmebalilika nafsi mpaka rohu zenu. Yaani hata chembe ya aibu!
Mimi ningekushauri uanze kazi hiyo mapema sana na uwashauri viongozi wako waachane na siasa ulizoziita za 'MIPASHO'.
Juzi kulikuwa na mjadala juu ya mswaada wa katiba mpya. Wakati akichangia mjadala huo; Hamisi Kigwangala (CCM), alichochangia alisema Mbowe anatembea kama Bibi harusi hakugusia kabisa mswa mpaka anamaliza mchango wake.Je wewe unavyojua; Kigwangala ni CHADEMA?Lusinde alitumia muda wake mwingi kueleza ni kwa jinsi gani yeye alivyo mwanasiasa mkubwa na wa kuheshimika.Hivi huyu naye CHADEMA?
Katika wakati wangu wa uhai tangu kuanzishwa vyama vya upinzani hapa Tanzania, sijawahi ona siasa za mipasho kama inavyoendelea katika kipindi hiki.
Mimi nimetoa mifano; sasa na wewe hebu toa mifano ili hoja yako iwe ya kweli.
Pia ni matumaini yangu hilo umeliona na ndio maana hisia za ushauri zimekujia haraka. Anza hilo mapema kwakuwa mnaowakati mrefu tu wa kurekebisha mambo. Ila matumaini yako 2015, lol! Umejipata matumaini mfu hataivo ni haki yako.
Unajua maana ya mipasho? Huhisi kwamba hiki ulichoandika hapa ndio mipasho yenyewe ninayozungumzia! hebu soma tena uzi kama hujaelewa.<br />
<br />
Pia Hilo maamuzi bila utafiti ni sawa kabisa na pia anza nalo mapema pia. Kwani hata hapo kilipochama chenu kina maamuzi ambayo yakitolewa bila utafiti maisha ya mtanzania kwa namna moja au nyingine yanaathirika. Mfano kugomea miswada mbalimbali bungeni na kupelekea kupitishwa bila hata kuangaliwa madhaifu na uthabiti wake ambapo jambo hili wanalifanya mara nyingi kwa ufasaha upinzani
Unaongea hoja nzuri ila kwa staili ya kejeli ila kwa kuwa tunafahamu dhamira yenu katika nchi hii; hatushangai pale mnapoamua kuikwamisha mipango yote yenye nia njema kwa taifa hili.Siku moja huenda mkauona ukweli na kuamua kuufuata.

Umemjibu vyema sana mkuu, na hata wapindishe ukweli vipi hawatakwamisha hata kidogo nguvu ya mabadiliko.
 
Tatizo vijana wengi wa chadewa mmekaa kimabishana.

Ni mabishano yenye kujenga na sio ninyi CCM mnaobishana kwa lengo la kupotosha. Mmeshindwa kushawishi watanzania sasa mnaamua kuwapotosha. It like " If u can't convince them, then confuse them" Ndipo mlipofikia sasa CCM. Kamwe hamtaweza kupingana na nguvu ya mabadiliko. Ref. Satta wa Zambia
 
Mkuu kwa taarifa nilizonazo ni kwamba CHADEMA ina mkakati mathubut wa kufundisha siasa na kuongeza uwezo wa viongozi wake waliopo na wanaotarajiwa kuwa viongozi ndani ya chama na nchi kwa ujumla.Zoezi hilo lilishaanza na inasemekana linaendelea kwa ufanisi mkubwa isivyokawaida.Taarifa zinasema vijana wana ari kubwa ya kujifunza na ni wepesi kuelewa.Utafiti unaonesha chadema ina vijaja wengi sana kwa sasa wenye weledi na uwezo wa kuwa viongozi. BAVICHA nayo inaonekana inaratibu kwa karibu na umakini mno maandalizi ya rasilimali watu hii. Hili ni jambo la kutia matumaini kwa kweli .Mwisho wa yote sisi ni wamoja. Taifa letu ni moja.CHADEMA ni moja, Lengo la chama ni moja ;Kuitoa nchi hapa ilipo na kuipeleka hatua kadhaa mbele. Natumai tutaweza kwa nia zetu safi na ushirikiano wetu.

Naona tuboreshe mbinu alizo tumia kumwondoa mkoloni mweupe sasa tuziboreshe tutumie kumwondoa mkoloni mweusi
 
W akuu salama!

Hapa nchini kumekuwa na tatizo kubwa sana la wanasiasa wengi kufanya kazi zao kishabiki, na kwa kusoma hisia za watu Fulani tu kwa wakati na kisha kutekeleza au kototekeleza mambo kadhaa yenye athari kwa jamii.Hali hiyo imepelekea kutopewa kipaumbele na kuto kutekelezwa kwa mambo mengi ambayo yangeweza kuwa na tija kubwa sana kwa taifa letu, na wakati mwengine wanasiasa kutekeleza mambo yenye athari mbaya kabisa kwa taifa letu (Emotional decisions).

Kwa maoni yangu tatizo hili ambalo limekuwa likiikumba serikali ya CCM (ambayo ndio iko madarakani); Kwa kiasi kikubwa limekuwa likisababiswa na kukosekana kwa watafifi mahiri na washauri wa masuala ya kisiasa kwa upande mmoja na kukosekana kwa wanasiasa wenye uwezo kwa upande mwengine. Jumla ya yote hayo ndio mzizi hasa wa tatizo la msingi.

Binafsi; baada ya kujiunga na CHADEMA, nina dhamira moja kubwa sana ambayo nakusudia kutumia uwezo wangu wote kuhakikisha naitekeleza katika kipindi cha uhai wangu wote uliobakia.Pamoja na mambo mengine; Nakusudia kutumia muda mwingi kufanya tafiti na tathmini na kishwa kuwashauri viongozi wa chama changu kwa maslahi ya chama na watanzania kwa ujumla.

Nimeamua kuwa nitatumia muda wangu na akili yangu katika eneo hili kwa sababu zifuatazo;

1. CHADEMA ndicho chama kinachoelekea kuchukua nchi ndani ya miaka miwili ijayo; Hivyo nisingependa kuwaona viongozi wangu wa CHADEMA wakishika nchi kisha nao wakakumbwa na mzimu wa kufanya mipasho badala ya kufanya siasa adhimu!

2. Maamuzi ya wanasiasa yana athari kubwa mno kwa nchi; Hivyo ikitokea wakiwa wanafanya maamuzi bila kufanya tafiti kama inavyotokea sasa hapo ndipo unapoona madhara makuu yakitokea na ni kwa kuwekeza jitihada katika eneo hili kutakakopelekea kufanya maamuzi sahihi na yenye maslahi kwa taifa.

3. Utafiti wangu umenionesha kuwa CHADEMA ina rasilimali watu ya kutosha yenye uwezo mkubwa wakuongoza; Hivyo kwa mimi si muhimu kuongeza nguvu katika eneo hili bali eneo jengine muhimu ili kuhakisha kwamba chama chetu hiki safi kinakuwa vizuri kwenye maeneo yote.

4. CHADEMA wameonesha nia ya kutaka kuyafahamu na kuyashughulikia kwa umakini yale wananchi wanayoyahitaji. Hivyo ni vyema kwa wale tunaoweza; tukawekeza nguvu zetu kusaidia kwa kadiri ya uwezo wetu na katika eneo ambalo kila mtu anaweza.

5. Kazi hii kimsingi ni kazi inayo mlazimisha mtu kufikiri kwa lazma. Kwa kadiri mtu anavyofikiri; ndivyo akili yake hukua zaidi; hivyo kwa kufanya kazi hii, sio tu kwamba nitakisaidia chama changu na hivyo kuisaidia nchi yangu, bali pia nitakuwa nikinufaika kwa kuongeza elimu na ufahamu wangu.

N.B.

Ikumbukwe kwamba CHADEMA ni taasisi inayofanya kazi kwa ushirikiano wa hali ya juu. Ni taasisi iliyojaa mifumo mingi ambayo yote hufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa mno. Ni ushauri wangu basi kwamba huu ni wakati wa kila mtanzania kuchangia kwa uwezo wake kusaidia kwa pale atakapoweza na kwa jinsi alivyojaaliwa na muumba wake ili hatimae tuweze kukiimarisha chama chetu hiki na hatimae tuweze kulijenga taifa letu kwa manufaa ya kizazi hiki na kizazi kijacho.

Eeeeee! Mwenyezi Mungu Tusaidie! Eee Mwenyezi Mungu tusaidie..............!

Mkuu Betlehem tupo pamoja sana na sie wengine tupo ndani ya hii serikali kwa hiyo kuhusu rasilimali watu imeenea kila idara na wizara za serikali tuna kadi zetu makabatini
 
Ni vision nzuri ila kumbuka unatakiwa umanage vizuri politics kwani si kila utakachoshauri kitakubaliwa.

Mara nyingi "We don't see things as they are, we see things as we are."
-Anais Nin
 
Back
Top Bottom