Dhambi isiyokuwa na msamaha (unforgiven sin)

Watakatifu Bora ni wale walioko duniani si walio kufa. Nafsi haifi ila roho hufa, ni maandiko matakatifu sio mimi .
 
💯
 
Kumkufuru Roho mtakatifu ni nini?

Kumkufuru ni kitendo cha kutukana kwa kujua, kukejeli kwa kujua na kupotosha kwa makusudi kwa mlengo wako chochote kibaya kuhusu utendaji wa ROHO MTAKATIFU

Pia ifahamike kuwa roho mtakatifu sio kitu ni nafsi hai (personality) kamili

Kwa mujibu wa biblia ni kuwa hakuna mtu awezaye kumkufuru Roho mtakatifu isipokuwa yule anayemjua sana (deep intimacy relationship with him) akaaamua kumkana kwa makusudi

Kitabu cha waebrania 6:1-7 kinaeleza hatua 6 ambazo mtu huwa anakuwa amefuzu katika ushirika wa ndani juu yake na Roho mtakatifu akivuka hizo hatua 6 alafu akaja akakana kuhusu UUNGU WA MUNGU NA KUYATUKANA MATUKUFU HUWA HASAMEHEWI[emoji120]
 
FUMBO... Awezaye KULIFUMBUA ni ROHO MTAKATIFU.

UKISHINDWA kulifahamu hili FUMBO, jitahidi kuishi kadili ya maagizo ya MUNGU.

Ubarikiwe.
 
Kwa sisi tunaoamini kwenye "Godhead"
Kwamba kuna MUNGU BABA, YESU KRISTO (MUNGU MWANA( na ROHO MTAKATIFU.

Tunaamini hawa wana lengo (aim) moja la kuhakikisha wote tunarudi mbinguni.

Ila wana kazi tofauti na moja ya kazi ya Roho Mtakatifu ni "kusafisha" (santicify) ,kutakatisha mtu ambae aliomba msamaha kwa Mungu Baba kupitia jina la YESU ,then kama msamaha wake umekubaliwa hawa MUNGU Baba na YESU Kristo wanaachia kazi ya iusafisha dhambi kwa huyu Roho mtakatifu.

So,kujibu swali lako,kwa nini Yesu alisema kumkufuru Roho mtakatifu ni dhambi isiyosamehewa ulimwengu huu wala ujao?

Jibu ni kwamba ,huwezi kumtukana Mtu anayekuosha dhambi zako.

Hapa Yrsu anajaribu kusema huwezi kuja kwake kutubu ama kuomba msamaha kwa kumtukana roho mtakatifu.

Hata Yesu akikusamehe itabidi yule yule uliyemtukana aanze kukusafisha kitu ambacho ni kinyume na sheria za mbinguni. (Eternal Laws).
 
Mkuu, hapa lazima kwanza ujue; roho mtakatifu ni nani/nini, anatendaje kazi zake, ni kazi gani anatenda kwetu wanadamu.
Baada ya hapo unaweza kujua kwanini Yesu Kristo alisema haya maneno.
Kwa ufupi tunaongozwa na utashi wa Roho Mtakatifu ambapo tunapata hekima, maarifa, busara na mapaji mengineyo.
Unapokwenda kinyume na haya yaani kutenda; uovu, dhuluma, ukatili, uongo, kubambika makosa na mengineyo maana yake ni kuwa umemkufuru Roho Mtakatifu na adhabu yake ndio Yesu Kristo anasema kamwe hutasamehewa.
Enyi watawala na wenye madaraka acheni uovu wenu na matendo yenu machafu kwani kiyama chenu kitakuwa cha mateso makali milele!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…