Dhambi haiwezi kuisha

Ugoromkali

Member
May 4, 2021
57
23
Habari zenu wana gt, ok tusipoteze muda twende moja kwa moja kwenye mada husika.
Ni hivi, kulingana na habari za kuhusu dini mbalimbali hapa duniani karibia dini zote hususani dini za kiislamu na kikristo kumeandikwa katika vitabu vya dini hizo kuwa kutakuwa na siku ya mwisho (kiyama) na hapo kila kitu kitafutika katika uso wa dunia na wale waliotenda mema watakwenda peponi na wale waliofanya mabaya watakwenda motoni milele!
Sasa swali langu ni hili, katika vitabu mbalimbali vya dini tajwa hapo juu tunaona vimeelezea mwanzo wa binadamu kuwa aliumbwa akiwa kamili bila pungufu lolote lakini baadae akakengeuka na kutenda dhambi kupitia shetani😳
Swali la msingi hapa ni kuwa kama hapo kabla ilikuwa hakuna dhambi na baadae ikaja kuwepo, je itashindikana vipi kutokea dhambi nyingine baada ya hukumu? Achana na wale watakaokuwa motoni nazungumzia wale watakaokuwa peponi je hakuna watakaokengeuka tena na kutenda dhambi? Au kule peponi shetani atakuwa hayupo kuweza kumdanganya binadamu tena?
Nawasilisha
 
Umeelewa swali?
Labda kama hujauliza ulichouliza.

Nakufafanulia kidogo

Mbinguni hakutakuwa na nafasi ya kukengeuka huko kwa sababu;
1. Mbinguni hakuna dhambi wala possibility ya kutenda dhambi huko.
2. Watakaoingia huko watakuwa wameoshwa na kutakaswa kabisa.
3. Shetani hatokuwepo, ameandaliwa sehemu yake special (kwenye ziwa la moto) ambapo wote wanaofata matendo yake watatupwa pamoja nae.

Nakuombea uwe mmoja wa watakaoingia katika raha ya milele mbinguni.

Hope umeelewa sasa.
 
Back
Top Bottom