Dhambi ambazo huwezi tubu peke yako bila kushirikisha watumishi wa Mungu

ACHA KUPOTEZA MUDA KUWATISHA WATU, fanyeni toba iliyo ya kweli mtasamehewa.

Haya, assume unatubu kwa mchungaji au padre alafu yeye ametoka kufanya dhambi kama yako na hajatubu?
Nimeandika wazi kabisa,

Nenda mtafute mtumishi wa Mungu wa Kweli aliyeokoka mwenye BUSARA ya Mungu.

Mbona mada Iko wazi, mnatafuta pa kujifichia?

Yesu alikwisha Sema, yaliyofanyika sirini, yatawekwa yote wazi, na pia imeandikwa, azifichaye dhambi hatafanikiwa.

Mungu ameelekeza, dhambi tajwa ni LAZIMA uhusishe Mtumishi wa Mungu wa Kweli aliyeokoka.

Na Kwa kuwa hujalazimishwa, ni hiari Yako kuamua.

Amen
 
Acha kudanganya watu. Kujua biblia na kuichambua haikufanyi ujitungie vitu ambavyo havipo huku ukirecall mistali ya biblia..
Labda utufafanulie, kwani biblia moja ina Agano la kale na Agano jipya?? Vitabu si vingejipanga tu bila kuvi categories agano la kale na agano jipya??
 
Pole sana, umenisikia nikifundisha watu kufanya uchafu?
Ndio,

Unapingana na mada, kwamba kwako,

Mtu akizini, au ameua mtu, au ni mchawi,

Wakijifungia na kutubu binafsi, unasema inatosha.
 
Ndio,

Unapingana na mada, kwamba kwako,

Mtu alizini, au ameua mtu, au ni mchawi,

Wakijifungia na kutubu binafsi, unasema inatosha.
Kwa hiyo mtu akipingana na hiyo imani yako potofu ndiyo anakuwa mzinzi?
 
Kipi kimetungwa hapo?

Huamini zilizotajwa hapo ni DHAMBI?
 
Kwa hiyo mtu akipingana na hiyo imani yako potofu ndiyo anakuwa mzinzi?
Yaeza kuwa,

Narudia tena, dhambi hapo juu, bila kumshirikisha Mtumishi wa Mungu wa Kweli Aliyeokoka,

Sahau Mbingu.

Njia ya Mbinguni, ni nyembamba sana, ila njia ya Kuzimu ni Pana, na waendao huko hujifariji, pombe kidogo Haina shd, wengine ukiwauliza why mnavaa marozali, au why mnapigia magoti sanamu, unajibiwa ni Ishara tu, wengine ni Wachungaji na wanazini na waumini na wanatubishana gizani na kesho wanarudi kuzini.

Mimi nakuambia, moto unawahusu wote wataopuuza ujumbe wa Mungu.

Amen
 
Huyu Mungu anayehitaji kubembelezwa ni out of character na superior-being, hio ni moja mbili yaani ameteua watu ili wawe wawakilishi wake ? (delegation) ili iweje ?

Hio ni process tu ya kibinadamu ya baadhi ya watu kujifariji kwamba wao ni wateule kuliko wengine...

Anyway whatever tickles your fancy..., to each their own....
 
Narudia tena, Yesu Kristo pekee ndiye mpatanishi kati mwanadamu na Mungu, tena ndiye anayetuombea kwa Baba. Acheni utapeli wa kuwafanya watu watoe sadaka ya ukombozi, huo ni wizi.
 
Narudia tena, Yesu Kristo pekee ndiye mpatanishi kati mwanadamu na Mungu, tena ndiye anayetuombea kwa Baba. Acheni utapeli wa kuwafanya watu watoe sadaka ya ukombozi, huo ni wizi.
Mimi nimemaliza.
 
Yeah!......Kuna dhambi ambazo muhusika mwenyekwe ni vigumu kuomba na kusikilizwa maana maagano aliyonayo hayaruhusu hayo, mfano uchawi/ushirikina, uuaji hapo lazima mtumishi amuongoze muhusika sala ya toba na kumtakasa kwa damu ya Kristo.
hiyo damu ya kristo munaitoa wapi kama sio kudanganyana
 
Narudia tena, Yesu Kristo pekee ndiye mpatanishi kati mwanadamu na Mungu, tena ndiye anayetuombea kwa Baba. Acheni utapeli wa kuwafanya watu watoe sadaka ya ukombozi, huo ni wizi.
Majizi kama yalivyo majizi mengine
 
Reactions: len
Ni dhambi nakubali kabisa. Ila hizo complication za kutafuta mtu aliye okoka kwelikweli umweleze shida yako unatudanganya na unawakwamisha watu wengine ambao wanatamani kumrudia Mungu wao
Huo ndio UKWELI,

Hakuna nayemkwamisha sababu sijajitungia hayo, ni Mungu mwenyewe ndo anaelekeza hivyo.

Dhambi tajwa hapo juu Zina maagano na mikataba ya kipepo, zingine zinahusisha NDOA BATILI kati ya mtenda dhambi na Pepo, hivyo mfungwa hawezi jifungua pingu mwenyewe,

Kama una mashaka na viongozi ulionao, nenda sehemu ingine, upate msaada.
 
Huyo mtumishi unamuelezea dhambi ulizofanya au inakuwaje?
Ndio, unamshirikisha, ndomana ni LAZIMA awe ameokoka, mwaminifu,muadilifu, mtunza Siri.

Ikiwa Hana sifa hizo, usimshirikishe, tafuta mwenye sifa husika, usifungwe na mipaka ya dini.

Ubarikiwe
 
Kama kweli mbingu ipo,, basi tutafika tukiwa tumechoka mnoo..
Halafu naomba unitajie ni kifungu gani wameclassify ipi ni dhambi kubwa na ipi ndogo maana mimi najua kwa Mungu dhambi zote ni sawa isipokua kumkufuru roho mtakatifu
 
Mbingu ipo na ndimo Mungu anamokaa.
Kuhusu dhambi, hakuna dhambi, zote zilichukuliwa na Yesu,
Dhambi ya kumkufuru roho ni mtu kutokuamini ya kwamba Mungu alimtoa mwanaye kama ondoleo la dhambi ili kila aaminie asife bali aishi
 
Kama kweli mbingu ipo,, basi tutafika tukiwa tumechoka mnoo..
Halafu naomba unitajie ni kifungu gani wameclassify ipi ni dhambi kubwa na ipi ndogo maana mimi najua kwa Mungu dhambi zote ni sawa isipokua kumkufuru roho mtakatifu
Dhambi zote ni sawa,

Bt zipo dhambi zilizotajwa hapo juu, utaratibu wa kutubu pekeako ni ngumu.

Mfano, umezini na mume wa mtu, halafu umebaini kuwa huyo ni DHAMBI, niambie utatubu pekeako na mzinzi mwenzio chumbani na mkakubaliana kuacha bila kumwomba radhi muibiwa mume au mke?
 
Umwombe radhi muibiwa Tena… you can’t be serious 🧐
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…