Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,265
- 21,443
Maneno yaliyotamkwa na Jaji Bernard Luanda, mwenyekiti wa jopo la majaji lililoshughulika na rufaa ya serikali dhidi ya dhamana ya Lema ni mazito sana na suala hili halipaswi kuachwa likapita kirahisi. Kimsingi, yaliyosemwaa na jaji, kulingana na IPP Media, ni kwamba;
Maneno ya jaji Luanda kwa niaba ya majaji wenzake, Jaji Stella Mugasha na Jaji Kipenka Mussa ni mazito sana. Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka kushutumiwa kwa maneno mazito kama hayo inabidi Waziri wa Sheria, Mwanasheria Mkuu na Mkurugenzi wa Mashitaka wote wajiuzuru mara moja ili kupisha tume huru kuchunguza nani alikuwa nyuma ya unajisi huu wa taaluma ya sheria na matumizi mabaya ya ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini.
Mtu yeyote atakaepatikana kuhusika na unajisi huu wa sheria na matumizi mabaya ya ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka kunyima haki anapaswa kuchukuliwa hatua bila kujali ana madaraka gani nchini. Hata kama itadhihirika Raisi alihusika basi itabidi utaratibu wa "impeachment" au hatua yeyote inayofanana na hiyo zichukuliwe.
- Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka inachafua mahakama nchini
- Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka inawafanya wanasheria wote nchini hawana akili
- Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka imetia najisi taaluma ya sheria nchini
- Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) alitenda hila ili Lema anyimwe dhamana
- Lema alinyimwa dhamana bila sababu za msingi kwa lengo la Mkurugenzi wa Mashitaka kumnyima haki
- Inatia shaka kama ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka ina watu wanaojua sheria